Monday, May 18, 2015

NDC YAFANYA UTHAMINISHAJI WA MALI ZA WANANCHI WA MCHUCHUMA NA LIGANGA ILI KULIPA FIDIA






Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi  wa pili kutoka kushoto akiwa amebeba Mkaa wa Mawe unaopatika katika machimbo ya Mchuchuma katika Wilaya ya Ludewa,wa kwanza kushoto ni Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo filikunjombe,wa tatu kutoka kushoto Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe  Fedrick Mwakalebela na Mkuu wa wilaya ya Njombe Bibi Salah Dumba




Mbunge wa  Ludewa Deo Filikunjombe  akiongea na Mkuu wa  Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi wakiwa wanatoka kukagua Makaa ya Mawe kwenya Mgodi wa Mchuchuma.






Shirika la Taifa La Maendeleo ( NDC) limezindua zoezi la Uthaminishaji wa Mali za Wananchi walio ndani ya Maeneo ya Mradi wa chuma cha Liganga katika      Wilaya ya Ludewa.
Kaimu Mkurugenzi wa ( NDC) Mlingi Mkocha amesema kuwa zoezi hilo la Uthamini wa Mali za wananchi litachukuwa miezi miwili mpaka kukamilika kwake ili kuendelea kuendelea kwa hatua za malipo kwa watu ambao wataamishwa maeneo yao kupisha uchimbwaji wa madini hayo.
Mkocha alisema kuwa  inakisiwa kuna tani milioni 126 za madini ya chuma zilizohakikiwa zinaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa kiwango cha tani milioni 2.9 kwa mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo aliwataka  watalaam watakaofanya uthamini wa mali za wananchi kuwa waaminifu na makini ili kutenda haki kwa kila mwananchi anayefanyiwa uthamini wa mali zake bila kuomba wala kupokea rushwa
Nchimbi alisema kuwa kazi hiyo ni muhimu na itaepusha migogoro  kama itatendwa kwa haki,vilevile aliwataka NDC na wawekezaji kutoa ajira kwa wananchi wa Ludewa na Njombe kwani wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi.

Mbunge  wa Jimbo hilo Deo Filikunjombe akiwahutubia wanachi wa kijiji cha Mkomang’ombe aliwataka washirikiane na wawekezaji katika kazi mbalimbali katika wilaya hiyo kwani itasaidia kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.

Mradi huo wa Chuma wa Liganga unatekelezwa  na Serikali ya Tanzania na China ,gharama za uwekezaji katika mradi huu zinakadiriwa kuwa na Dola za Marekani bilioni 1.8





















Popular Posts