Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi wa pili kutoka kushoto akiwa amebeba Mkaa wa
Mawe unaopatika katika machimbo ya Mchuchuma katika Wilaya ya Ludewa,wa kwanza
kushoto ni Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo
filikunjombe,wa tatu kutoka kushoto Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Fedrick Mwakalebela na Mkuu wa wilaya ya
Njombe Bibi Salah Dumba
Mbunge wa Ludewa Deo
Filikunjombe akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi wakiwa
wanatoka kukagua Makaa ya Mawe kwenya Mgodi wa Mchuchuma.
Shirika la Taifa La
Maendeleo ( NDC) limezindua zoezi la Uthaminishaji wa Mali za Wananchi walio
ndani ya Maeneo ya Mradi wa chuma cha Liganga katika Wilaya ya Ludewa.
Kaimu Mkurugenzi wa (
NDC) Mlingi Mkocha amesema kuwa zoezi hilo la Uthamini wa Mali za wananchi
litachukuwa miezi miwili mpaka kukamilika kwake ili kuendelea kuendelea kwa
hatua za malipo kwa watu ambao wataamishwa maeneo yao kupisha uchimbwaji wa
madini hayo.
Mkocha alisema
kuwa inakisiwa kuna tani milioni 126 za
madini ya chuma zilizohakikiwa zinaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa
kiwango cha tani milioni 2.9 kwa mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Njombe
Dk.Rehema Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo aliwataka watalaam watakaofanya uthamini wa mali za
wananchi kuwa waaminifu na makini ili kutenda haki kwa kila mwananchi
anayefanyiwa uthamini wa mali zake bila kuomba wala kupokea rushwa
Nchimbi alisema kuwa
kazi hiyo ni muhimu na itaepusha migogoro
kama itatendwa kwa haki,vilevile aliwataka NDC na wawekezaji kutoa ajira
kwa wananchi wa Ludewa na Njombe kwani wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi.
Mbunge wa Jimbo hilo Deo Filikunjombe akiwahutubia
wanachi wa kijiji cha Mkomang’ombe aliwataka washirikiane na wawekezaji katika
kazi mbalimbali katika wilaya hiyo kwani itasaidia kuleta maendeleo katika
wilaya hiyo.
Mradi huo wa Chuma wa
Liganga unatekelezwa na Serikali ya
Tanzania na China ,gharama za uwekezaji katika mradi huu zinakadiriwa kuwa na
Dola za Marekani bilioni 1.8
No comments:
Post a Comment