Mamlaka ya Maji Mkoa
wa Njombe(NJUWASA) imepokea kiasi cha
fedha 2.6 ( 2,577,138,890.00) bilioni kutoka Wizara ya Maji toka mwaka 2013 kwa ajili ya kuboresha
hudumaya maji katika Mji wa Njombe.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Njombe Mhandisi, Daudi
Majani amesema kuwa mpaka sasa fedha hizo zimetumika kujenga chanzo cha
maji cha Nyenga,matanti matatu ya maji
na utandazaji wa mabomba ya maji ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika
mwisho wa mwezi wa saba mwaka huu.
Alisema kuwa mpaka sasa Ujenzi wa kidakio cha maji
umekamilika na ujenzi wa matanki matatu
yaliyopo katika maeneo ya Airport,Kambalage ,Igeleke na Nzengelendete na kila tank linauwezo wa ujazo wa lita
135,000 kila mojaHatua inayoendelea sasa ni utandazaji wa mabomba ya maji
katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Njombe .
Mradi huo ukikamilika utawezesha kufanya mji wa Njombe
kuongeza upatikanaji wa maji kutoka
asilimia 55 hadi 80 na kufanya
mji huo kuondoka na huwaba wa maji .
Majani amesema hayo jana kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa
Njombe Dk.Rehema Nchimbi alipotembelea vyanzo vya maji na kuangalia mtandao wa
maji katika mji wa Njombe.
Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka Halmashuri za mji wa Njombe
kushirikiana na mamlaka ya maji Mkoa wa Njombe kuakikisha wanatoa elimu kwa
wananchi waliopo kwenye vyanzo vya maji ili kutunza vyanzo vya hivyo.
No comments:
Post a Comment