Tuesday, June 23, 2015

Urais 2015: Mwanamke wa 5 ajitosa kuchukua fomu CCM



















 Mwananmke mwingine  ambaye ni kada wa CCM, Ritta Ngowi amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
 
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu jana makao makuu ya CCM mkoani Dodoma Ngowi alisema akifanikiwa kuwa rais  ataanzisha kituo kikubwa cha kuwahudumia wastaafu, walemavu, wasiojiweza na vijana.
 
Kingine atakachofanya ni kuendeleza mazuri yaliyofanywa na marais waliopita, lakini zaidi akiweka mkazo kwenye masuala ya elimu na kukuza uchumi.
 
Aidha Ritha anafanya ,  idadi ya wanawake waliojitosa mbio za urais kufikia watano kati ya 39 waliochukua fomu hadi sasa.
 
Wanawake wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa (NIMR), Dk Mwele Malecela, Balozi Amina Salum Alli na Monica Mbega.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts