Zaidi ya
wachina elfu sita (6,000) wanatarajiwa kuingia katika Mkoa wa Njombe kwenye
sekta ya madini hasa makaa ya mawe na
Chuma kwenye eneo la Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa.
Hayo yamesemwa jana
kwenye Ukumbi wa Lutheran Makambako na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi
alipokuanaongea na watumishi wa Halmashuri ya Mji Makambako,alisema kuwa Mradi
wa Linganga na Mchuchuma unatarajiwa
kuanza kuchimbwa makaa ya m awe na chuma hivi karibuni utatoa ajira zaidi ya
Elfu thelathini (30,000) zikiwepo za
wazawa na wageni.
Kutokana na hilo
amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji Makambako hasa sekta ya Ardhi
kuakikisha wanaweka mipango mizuri ya matumizi ya ardhi na kupima viwanja ili
kuwavutia wawekezaji mbalimbali katika ujenzi wa Hoteli za kisasa na halmashuri
kuakikisha wanaboresha miundombinu ya Maji na barabara .
Dk .Nchimbi alisema kuwa mpaka sasa shirika la maendeleo ya
Taifa (NDC) limeanza mchakato wa uthamini
wa mali za wananchi ili waweze kulipwa fidia kupisha mradi huo.
Aliwataka wananchi wa
Makambako na Njombe kwa Ujumla kujiandaa na ujio wa wageni mbalimbali
kwa kufuga kuku ,Ng’ombe pamoja na mifugo mingine ili kuweza kuwauzia wageni hao na kuongeza kipato
cha familiya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako Hanana Chesco Mfikwa alisema kuwa wanajiandaa kwa kuwapokea wageni hao kwa
kuakikisha wanaweka mipango mizuri ambayo itasaidia wageni kuwekeza zaidi
katika eneo la Makambako.
No comments:
Post a Comment