WIKI moja kabla ya kwisha kwa muda wa warudisha fomu kwa makada wa CCM
waliojitokeza kuwania kupitishwa na chama hicho kuwania urais wa
Tanzania, ni wanachama sita tu kati ya 39 ndio waliorudisha fomu mpaka
sasa.
Kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa urais ndani ya
CCM, mwisho wa kurudisha fomu ni Julai 2, mwaka huu ambapo kila
aliyechukua fomu anatakiwa kuwa na wadhamini 450 kutoka mikoa 15 ambapo
mitatu iwe ya Zanzibar.
Idadi ya wanachama waliojitokeza mwaka huu inaonekana kuwa ni kubwa,
mara tatu zaidi ya waliojitokeza mwaka 2005 ambapo wagombea walikuwa 11,
ingawa Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyeibuka kidedea na kutetea tena
ushindi wake mwaka 2010.
Waliorudisha fomu ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Makamu
wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Makongoro Nyerere (Mbunge wa Afrika
Mashariki), Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli, Waziri wa Kilimo, Chakula
na Ushirika, Steven Wassira na Balozi Ally Karume.
Wengine waliojitokeza kuchukua fomu ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
Mawaziri wakuu wa zamani, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Pia wamo Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri
wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Mbunge
waSengerema, William Ngeleja, Mkazi wa Musoma mkoani Mara, Boniface
Ndengo na mkulima kutoka Kijiji cha Mjimtala Wilaya ya Kasulu, Kigoma,
Idelphonce Bilohe na Balozi Augustino Mahiga.
Wengine ni Dk Hans Kitime, Dk Mwele Malecela, Mbunge wa Nzega Dk
Hamis Kingwangala, Balozi Amina Salum Ally, Naibu Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, Mtumishi wa CCM, Amos
Siyantemi, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, Wakili Mwandamizi Godwin
Mwapongo, Peter Nyalile, Leonce Mulenda, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino
Ramadhani na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro.
WanaCCM wengine wanaoutaka Urais ni Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani, Monica Mbega, Patrick
Chokala, Joseph Chagama, Malick Malupu, Ritha Ngowi na mwanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Mzumbe, Amos Robert.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment