Monday, June 22, 2015

Lowassa Azidi Kupata Mapokezi Makubwa

WAZIRI Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina lake katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.

Lowassa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.

"Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu". alisema Lowassa.

Lowassa aliwasili Mkoani Ruvuma mapema  jana mchana akitokea Mkoani Iringa kwaajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea kufunga barabara kuu ya mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya paa la  jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza nao.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment

Popular Posts