Umati wa watu wakisubiri kutambua maiti za watu waliofariki katika ajali ya basi la Majinja Express katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya Mufindi.
Baadhi ya ndugu waliopoteza ndugu zao katika ajali ya basi la Majinja Express wakilia kwa uchungu mara baada ya kujua kuwa moja wa ndugu zao wamefariki dunia.
Mmoja wa majeruhi ambaye jina lake halijatambulika akiwa katika hospitali ya wilaya Mufindi kwa matibabu zaidi.
Mmoja wa majeruhi ambaye hali yake mbaya akipakizwa katika gari la wagonjwa kupelekwa kwa matibabu zaidi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.
Umati wa watu wakiwa katika eneo
la tukio mara baada ya ajali kutokea eneo tukio ambapo ajali ya basi la
Majinja limepoteza watu 42 katika ajali hiyo.
(Picha na Denis Mlowe)
Mpaka
saa hizi naambiwa na watu wa Iringa idadi ya waliokufa katika ajali
hiyo ni 42 na maiti 32 ambazo hazijitambuliwa zimefikishwa hospitali ya
mkoa wa Iringa kutoka Mafinga.
Moja wa mashuhuda wa
ajali hiyo Jackson Manga alisema kama dereva wa basi hilo angezingatia ishara
za taa kali alizokuwa akiwashiwa na dereva wa roli hilo kwa vyovyote vile ajali
hiyo isingetokea.
Manga alisema katika
eneo hilo lenye mteremko wa wastani, roli lilikuwa likipandisha na basi
lilikuwa likishuka.
Alisema ukaidi wa
dereva wa basi ulisababisha dereva wa roli aingie katika shimo kubwa katika
eneo hilo hali iliyosababisha ashindwe kulimudu gari hilo kabla ya kuvaana uso
kwa uso na basi hilo.
“Baada ya kuvaana,
kontena la futi 40 lililokuwa limepakiwa katika roli hilo liliruka juu na kwa
kishindo kikubwa, kubamiza na kufunika basi hilo,” alisema.
Mmoja wa majeruhi wa
basi hilo, Kevin Humphrey ambaye kalazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi
alisema; “tulisikia mshindo mkubwa baada ya basi letukugongana na roli hilo na
mshindo huo ulisababisha na kontena iliyotoka kwenye roli hilo na kupiga juu ya
basi letu.”
No comments:
Post a Comment