UZEMBE
wa dereva wa basi Mitsubishi Fuso, mali ya kampuni ya Another G Trans lenye
usajili Namba T.927 CEF, Nicolaus Magula (30) umesababisha abiria 23 wapoteze
maisha na wengine 34 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea juzi Jumapili
mjini Mafinga.
Ajali
hiyo ilitokea Majira ya saa 1.45 usiku katika eneo la Kinyanambo A, barabara
Kuu ya Iringa Mbeya baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na na roli aina ya Scania lenye namba za usajili
T.916 AQM likiwa na tela namba T 965 BEH, mali ya kampuni ya Bravo Logistics
(T) Ltd ya Dar es Salaam.
Wakati
ajali hiyo ikitokea, wakazi wa Mafinga na Tanzania kwa ujumla bado wanakumbuka
ajali nyingine iliyotokea katika eneo la Changarawe, mjini Mafinga miezi mitatu
iliyopita (Machi 11, mwaka huu) ikuhusisha roli Scania namba T 689 APJ mali ya
Cipex Company na basi Scania namba T 438 CED na kusababisha vifo vya watu 50.
Akizungumza
na wanahabari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Pudenciana Protas
alisema; “wakati basi hilo lenye uwezo wa kupakia abiraia 65 lilikuwa likitokea
Iriinga kuelekea Njombe, roli hilo lililokuwa likiendeshwa na Rogers Wales mwenye
miaka 39, Msambaa mkazi wa Mwanza lilikuwa likitokea barabara kuu ya Mafinga
kuelekea Iringa.”
Protas
alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo aliyekosa
umakini na kutaka kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari.
Alisema
miili ya marehemu na majeruhi hao ilikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya
Mufindi ya mjini Mafinga, mapema baada ya ajali hiyo kutokea.
Alisema
miili 12 ya watu waliokufa imekwishatambuliwa na kuwataja kuwa ni pamoja na Lucas
Pancras, Blasto Samila, Dickson Luvanda, Albert Silla (askari wa Ruvu JKT), Eva
Mbalinga, Khadija Mkoi (4), Clemence Mtati, Mohamed Lalika, Castory Mwakiamba,
Damiana Myala na Silo Nziku ambao wote walikuwa katika basi hilo na dereva wa
roli hilo Rogers Wales.
Alitaja
majeruhi wa ajali hiyo waliokuwa katika basi hilo kuwa ni pamoja na Emma
Lupembe (35), Veronica Simba (20), Shafia Ally (24), Mariamu Mbise (23), Anita
Makwela (24), Benita Sagara (18), Bertha Mkoi (27), Rahel Mavika (18),, Selina
Fulgensi (23), Maria Mwenda (17), Ndipako Mbilinyi (28), Alexander Mkakazi
(28), Meshack Kibiki (44), Simoni Jumbe (22), Jerry Lutego (36), Enock Kanyika
(18) na Yusuph Lulandala (22).
Wengine
ni Deogratias Kayombo (21), Petro Mwalongo (21), Paul Chahe (21), Kennedy
Msemwa (28), Emanuel Anthony (21), Mode Shilazi (21), Godfrey Kanyika (39),
Boniface Bosha (20), Ambiana Meshack (35), Martha Kanyika (30), Melika Tonga
(2.5), Yusuph Luhumba (34) na Damiana Kuyala (42).
Protas alisema majeruhi
wengine wanne, wanaume wawili na wanawake hawajatambuliwa majina yao kwasababu
walikuwa hawaongei
No comments:
Post a Comment