Dar er Salaam. Mshambuliaji Mrisho Ngassa
aliyesajiliwa na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini hivi
karibuni, jana aliibuka katika mazoezi ya timu yake ya zamani Yanga.
Ngassa alisajiliwa na Free State Stars kwa mkataba
wa miaka minne mwishoni mwa mwezi uliopita na alirudi nchini kwa ajili
ya kuitumikia Taifa Starsiliyokuwa ikicheza dhidi ya Uganda katika mechi
ya kuwania kufuzu kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza
ligi za ndani (CHAN), ingawa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilimzuia
kwani ameishasajiliwa nje ya ligi ya Tanzania.
Gazeti hili lilimshuhudia mshambuliaji huyo
akifanya mazoezi na Yanga mwanzo mwisho na alipomaliza mashabiki wa
klabu hiyo walilisukuma gari lake mpaka nje geti wakionyesha mapenzi kwa
mchezaji huyo.
Ngassa ameitumikia Yanga kwa mafanikio kabla ya kuamua kuachana nayo na kwenda kusaka ulaji katika klabu ya Free State.
Ngassa alisema ameamua kufanya mazoezi na Yanga kwani bado iko moyoni mwake na hakuondoka kwa ubaya.
“Hapa kama niko nyumbani, kwani hii ni timu iliyo
moyoni mwangu hivyo kama niko Dar es Salaam sioni ubaya kufanya mazoezi
na Yanga kwani naamini kuna siku nitarudi hapa,”alisema Ngassa.
“Najiweka fiti wakati nikisubiri klabu yangu
initumie tiketi ya kurudi Afrika Kusini maana walinipa ruhusa ya kuja
Dar es Salaam kwa ajili ya timu ya Taifa, lakini nikazuiwa kucheza mechi
na Uganda,” alisema Ngassa.
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Ngassa kwani aliifungia Yanga mabao manne tu licha ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Aprili
No comments:
Post a Comment