Tuesday, April 22, 2014

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE KATIKA TARAFA YA LUPEMBE

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain (mst) Aseri Msangi amemwagiza Mkurugenzi wa halmashuri ya wilaya ya Njombe kuakikisha barabara kutoka  Ikondo mpaka Ukalawa tarafa ya lupembe inatengenezwa na kuakikisha inapitika wakati wote.

Captain Msangi alisema hayo jana alipokuwa anakagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya halmashuri ya Njombe,ambapo alikagua miradi ya Barabara,Miundombinu ya Madarasa na Mahabara.

Msangi alisema kuwa barabara ya Lupembe inayaopitia Ikondo mpaka Ikalawa ni muhimu kwa wanananchi wa Lupembe kutoka na barabara hiyo kutumika kupita magari yanayokusanya zao la Chai kutoka kwa wananchi kwenda kiwanda cha Ikanga kilichopo Lupembe.

Mkurugenzi wa halmashuri hiyo Bwana Paulo Malala,alisema kuwa tayari halmashauri yake imeshomba fedha ya dharula kutoka Ofisi ya  Waziri Mkuu -TAMISEMI kiasi cha shilingi Million miambili (200,000,000) kwa ajili ya matengenezo ya barabara hiyo.



Picha zote zinzonyesha Hali ya barabara ya Lupembe -Ukalawa yenye Kilometa 40




No comments:

Post a Comment

Popular Posts