Tuesday, April 8, 2014

ANAFUNZI WATATU WA SHULE YA MSINGI IBUMI WILAYANI LUDEWA NJOMBE WAFA MAJI



ANAFUNZI WATATU WA SHULE YA MSINGI IBUMI WILAYANI LUDEWA NJOMBE WAFA MAJI
RPCKamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea kwa vifo wa watoto hao Wilayani Ludewa

Na Steven Ngole Njombe

 Wanafunzi Watatu  wa Shule ya Msingi Ibumi Wamefariki dunia Baada ya Kujaribu Kuogelea katika Dimbwi la maji  Wilayani Ludewa.

Kufuatia Tukio Hilo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Vifo Vya Wanafunzi Watatu wa Shule ya Msingi Ibumi Wilayani Ludewa Baada ya Kujaribu Kuogelea Kwenye Dimbwi la Maji Wakati wa Kitoka Shuleni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Aprili Tatu Mwaka Huu Majira ya Saa Kumi Jioni Ambapo Watoto Hao Walipita Kwenye Dimbwi Hilo Lililokuwa Likitumika Kwa Ajili ya Kufyatulia Tofali na Kujaribu Kuongelea.

SACP Ngonyani Amewataja Watoto Waliofariki Kuwa ni Kasbeth Kasbeth Miaka 6 Ambaye Alikuwa Hajaanza Shule,Noeli Msemwa Miaka 8 Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza na  James Haule  Miaka 9 Mwanafunzi wa Drasa la Pili  Wote Walikuwa Wanafunzi  Katika Shule ya Msingi Ibumi Wilayani Ludewa.

Akielezea Tukio Hilo Kamanda Ngonyani Amesema Katika Tukio Hilo Walikuwa Watoto Wanne Ambaye Mmoja Kati Yao

Alikimbia Kutoa Taarifa Baada ya Kuona Wenzake Wanazidiwa na Maji Alikimbia Kutoa Taarifa.

Katika Hatua Nyingine Kamanda Ngonyani Ametoa Wito Kwa Wananchi Kuchukua Tahadhari Zaidi Katika Kipindi Hiki Ambacho Mvua Zinaendelea Kunyesha na Kuwataka  Wananchi Kufukia Mashimo Yote Ambayo Yanahifadhi Maji Ili Kuepusha Vifo Viunavyoweza Kuepukika.

Matukio ya Vifo Vitokanavyo na Ajali ya Maji Yamekuwa Yakiendelea Kutokea Katika Mikoa Maeneo Mbalimbali  Mkoani Njombe Ambapo Wahanga Wakubwa wa Matukio Haya ni Watoto.

No comments:

Post a Comment

Popular Posts