DAVID MOYES
Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester
United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex
Ferguson kustaafu.Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa
ligi kukamilika Mancheseter united ina nafasi ya saba kwenye
jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi
Liverpool.Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano
ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban
miaka ishirini.
No comments:
Post a Comment