Dodoma. Mjumbe wa Bunge la Katiba, Mchungaji
Peter Msigwa amemvaa Askofu Donald Mtetemela na kumtaka avae rasmi
magwanda ya Chama cha Mapinduzi (CCM).Akizungumza na gazeti hili, Msigwa ambaye pia ni
Mbunge kupitia Chadema alisema Askofu Mtetemela alionyesha upendeleo wa
wazi kwa CCM alipokuwa akichangia bungeni mjini Dodoma Alhamisi
iliyopita.
Katika mchango wake, Askofu Mtetemela alikemea
tabia ya wajumbe wa Bunge hilo kuwakashifu waasisi wa Taifa aliosema
wana heshima kubwa kwa jamii na mbele za Mungu.
Hata hivyo, Msigwa alisema:“ Askofu ameonyesha upendeleo wa wazi wazi japokuwa anasema anasimamia katikati (hana upande kisiasa). Hakuona kejeli, ubaguzi na matusi yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Bunge?”Mchungaji Msigwa alisema yeye ni mchungaji lakini amejitokeza wazi kusimamia Chadema tofauti na askofu huyo ambaye ameonyesha wazi upande anaousimamia wa CCM, wakati awali walidhani ni mtu mwenye msimamo wa kati.

“Mimi sina ugomvi kama ameamua kuwa mwanasiasa
kama mimi lakini awe wazi kwa kusimama na kujionyesha wazi upande
aliopo,”alisema. Kauli ya Askofu Mtetemela Katika mchango wake, Askofu Mtetemela alilieleza
kukerwa na kauli ya Profesa Lipumba kuliita Bunge la Maalum la Katiba
kuwa linafanana na kundi ovu la Italahamwe.“Nasikitika kwamba sijaweza kumuona yeye binafsi
Profesa Lipumba ili niweze kumwambia masikitiko yangu, na naamini ni
masikitiko ya wengine. Mshtuko wangu ni kwamba alilinganisha Bunge hili
na kundi la Intarahamwe la Rwanda,” alisema. Alibainisha kwamba kihistoria inajulikana
Intarahamwe ni wauaji, hivyo sio busara kabisa kuwafananisha wajumbe wa
Bunge Maalumu na kundi hilo.
“Hatuko hapa kumuua mtu yeyote, kutuita sisi
wauaji si jambo jema, ni baya lakini pia kauli hiyo inaweza kufufua
maumivu ya wenzetu wa Rwanda ambao hawataki hali hiyo ijirudie tena
katika nchi yao,” alisema. Alieleza kuwa kauli hiyo pia inaweza kuibua hisia
tofauti hata kwa Serikali ya Rwanda inayoweza kufikiri kuwa Tanzania
inalifanyia mzaha jambo lililowaumiza kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment