Watu 11 wamepoteza maisha papo
hapo na mwingine mmoja kufariki dunia akiwa njiani akipelekwa
hospitali ya rufaa ya Bugando,baada ya kutokea ajali mbaya ya gari
iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lililokuwa likitokea
Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.
Basi hilo liligonga nyumba kisha
kupinduka leo saa tano na dakika 10 asubuhi katika barabara ya Mwanza –
Mara katika kijiji cha Yitwimila kata ya Kiloleli wilaya ya Busega Mkoani
Simiyu.
Mbali na watu 12 kufariki dunia pia
watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa ni
mwendo kasi wa sasi hilo ambapo dereva wa alishindwa kumudu gari hilo likiwa
katika kasi na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na
kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amesema miongoni
mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume
7.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema
kabla ya kutokea kwa ajali hiyo basi hilo lilianza kuyumba na kusababisha
kugonga nyumba iliyokuwa kando kando ya barabara hiyo.
Mganga mkuu wa Hospitali ya
Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Dk Athuman Pembe alithibitisha kupokea majeruhi 60
pamoja na maiti 11.
Amesema kati ya majeruhi hao
25 hali zao siyo nzuri wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Bugando
jijini Mwanza, na kwamba hali za majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo
zinaendelea vizuri na tayari wengine wameanza kuruhusiwa.
Jeshi la polisi mkoani Simiyu
limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment