Thursday, April 10, 2014

WANANCHI ITULAHUMBA WILAYANI WANGING'OMBE WAMFUKUZA AFISA MTENDAJI LEO

Wananchi wa Kijiji cha Itulahumba Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Leo Walitoa Muda wa Saa Mbili Kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji Hicho Bwana Batista Msemwa Kuhama Kijijini Hapo Kwa Madai Ya Kuwa Tangu Alipohamia Kikazi Kijijini Hapo Hakuna Kazi Alizozifanya.

Mapema Leo Wananchi Hao Walikusanyika Nyumbani Kwa Afisa Mtendaji Huyo Wakimtaka Aondoke Haraka Iwezekanavyo Kabla Ya Wao Kuchukua Maamuzi Magumu ya Kumuondoa Kwa Nguvu Kwa Madai ya Kuwa Tangu Ahamishiwe Kijijini Hapo Hakuna Kazi Alizozifanya Kwa Kuwa Walishamkataa Tangu Awali.

Kumkataa Afisa Mtendaji Huyo Kulitokana na Kile Kinachodaiwa Alisikika Kwenye Vyombo Vya Habari Kuwa Anatuhumiwa Kufuja Mali za Kijiji cha Itambo Hivyo Tangu Serikali Imuhamishie Kijijini Hapo Wananchi Walimkataa Mbele ya Afisa Mtendaji wa Kata na Diwani Kitu Ambacho Hadi Sasa Bado Ameendelea Kuwepo Kijijini Hapo Bila Kazi Yoyote,Na Hapa Wananchi Hao Wanasema.

Uplands Radio Imefanikiwa Kuzungumza na Afisa Mtendaji Huyo Bwana Batista Msemwa Ambaye Amekubali Kuondoka Kijijini Hapo Huku Akakanusha Tuhuma za Wananchi Hao Kama Anavyoeleza,

Tangu Mwezi Septemba Mwaka Jana Wananchi Hao Walipo Muondoa Madarakani Mwenyekiti wa Kijiji Hicho na Kumkaimisha Bwana Shaibu Mahegele Ndipo Walipomkataa na Afisa Mtendaji Huyo Ambaye Aliendelea Kuishi Kijijini Hapo Bila Kufanya Kazi za Kijiji.

Hali Hiyo Imetajwa Kusababisha Uhalifu na Wizi Mkubwa Kijijini Hapo Kutokana na Kukosekana Kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji Ambaye ni Msimamizi wa Amani Kijijini Hapo..


 




 


 

 FISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA BATISTA MSEMWA AKIWA NDANI YA NYUMBA YAKE AKIJADILI HALI ITAKAVYOKUWA BAADA YA WANANCHI KUFIKA NYUMBANI KWAKE GHAFRA WAKIWA KUNDI KUBWA

 
 HAWA NI WANANCHI WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA WAKIWA KATIKA NYUMBA YA MTENDAJI HUYO
 

No comments:

Post a Comment

Popular Posts