KILIMANJARO
WATUMIWA SUGU WA KUCHAKACHUA VIROBA VYA
KONYAGI WASHINDWA DHAMANA NA KURUDISHWA RUMANDE.
WAELEZEWA NI WATU HATARI SANA WAIOFAA
KUACHILIWA KWA DHAMAN
WANATUHUMA KILA PEMBE YA NCHI IKIWEMO DAR ES
SALAAM
YAELEZWA, KONYAGI FEKI WANAZOTENGENEZA
ZIMEATHIRI WATANZANIA WENGI
BAADHI YA WAMILIKI WA MABAA WALIOHUDHURIA
MAHAKAMANI HAPO WAMETOA RAI KWA WANANCHI KUACHA KUNUNUA KONYAGI VICHOCHORONI NA
BADALA YAKE KWENYE MABAA HALALI AU MADUKANI
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Moshi, leo imefurika mamia ya
wananchi waliokwenda kushuhudia watuhumiwa sugu wa utengenezaji wa konyagi feki
na bidhaa nyingine mbalimbali na kuzibandika nembo za TRA ambayo inadiwa
kudhuru maelfu ya watanzania.
Hata hivyo mahakama ya mkazi moshi imewaachia kwa dhamana
watuhumiwa hao nane ambao wanakabiliwa na tuhuma za kutumia alama za biashara
za makampuni mengine kwa nia ya kutapeli.na
kujipatia pesa kinyume cha utaratibu.
Watuhumiwa hao ni Yusuph George, Richard Leonard, Preygod
Urassa, Mohamed Rashid, Greyson Jonathan, George Kisivani, Hagai Nelson na
Jackson Shayo, ambao wanatuhumiwa kwa pamoja kwa
kutumia kwa nia ya kutapeli alama ya biashara ya Konyagi
kinyume cha sheria huku wakijua wazi ya kuwa alama hiyo ni ya kibiashara ya
halali ya kampuni ya Tanzania Distilleries Limited.
Watuhumiwa hawa wana kesi mbalimbali ikiwemo ile ya
kutumia nyaraka za mamlaka ya mapato nchini TRA ikiwemo mihuri yenye namba za
kodi ya mapato jambo ambalo linadaiwa kuikosesha serikali mapato mengi.
Wakili
wa serikali Julius Semali ameiambia mahakama ya mkazi Moshi kuwa watuhumiwa hao
ni hatari na kwamba wanakabiliwa na kesi za namna hiyo
maeneo mbalimbali hapa nchini.
Singida wana kesi ya namna hii na ambayo itaendelea tena
Aprili 30, 2014, Ilala wanatafutwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka
za TRA wakati Arusha wanatafutwa kwa kukiuka dhamana na kutoroka mwaka 2012.
Pamoja na kupewa dhamana kwenye kesi hiyo huko Moshi,
bado hakimu aliamuru warudishwe rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya
dhamana.
Kesi hii imevutia wammia ya wakazi ambapo miongoni mwao
ambao ni wafanyabiashara za mabaa wametoa wito kwa wananchi kuepuka kunywa
konyagi vichochoroni kutokana na madhara ambayo wameshapata watu wengi.
No comments:
Post a Comment