Monday, August 11, 2014

RPC NGONYANI WA NJOMBE APATA AJALI NA BODYGAD WAKE AFARIKI PAPO HAPO



 Hilo ndio gari la RPC Ngonyani baada ya ajali

 


 

 Muonekana wa Gari la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe BAADA YA AJALI USIKU HUKO TANWATT, KIBENA  Njombe.Picha na Gabriel Kilamlya


Taarifa ambazo zimetufikia katika chumba chetu cha habari muda huu zinasema kwamba kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani amepata ajali mbaya ya gari usiku wa kuamkia leo akitoka Makambako kuelekea Njombe

Kwa mujibu wa taarifa ajali hiyo imesababisha kifo cha "body guard" wa kamanda Ngonyani ajulikanaye kama H580 PC Geroge kufariki dunia papo hapo, huku kamanda Ngonyani na dereva wake Nwaka Seme wakinusurika na kwa sasa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Njombe

Akizungumza na mwandishi wetu Katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe Muuguzi wa Zamu Bi.Neda Chelesi Amesema Kuwa Ajali Hiyo Imetokea Maeneo ya TANWATT Karibu na Jengo la TANSEED Kibena Usiku wa Kuamkia leo Agosti 9 Mwaka Huu na Kwamba Katika Ajali Hiyo Amepokea Majeruhi Wawili na Maiti Moja

Chanzo cha ajali hiyo inayodaiwa kutokea majira ya saa tano usiku hakijafahamika na  taarifa zaidi utazidi  kupata endelea kutufuatilia.

KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  pamoja na dereva wake Nuaka Seme  wamelazwa katika hispitari ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea  kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia  jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.

Akiongea na vyombo vya habari  huku akipatiwa matibabu katika hospitari ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP Yahaya  rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hanaruhusa Kamanda Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa nne za usiku katika barabara ya  Makambako hadi Njombe.

Aidha Jeshi la Polisi  limesema kuwa  katika ajali hiyo aliyefariki dunia ni George  Stephano  Matiko (24)



 H580 Pc George  Enzi za uhai wake.
Nuaka Sema aliyekuwa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili PT 2058  alisema kuwa kutokana  gari hilo la mizigo kukaa katikati ya barabara walishindwa kupishana kwa wakati na kuligonga kwa nyuma na baadae kukutana uso kwa uso na nguzo ya umeme iliyowasababishia ajali.

"ghafla niliona gari mbele likiwa limewasha taa zote za mbele (full light) likiwa upande wetu na nilivyoona hivyo niliwasha taa kuashiria hatari  na ndipo mwenye gari la mizigo alianza kukwepa kuelekea upande wake na wakati tukipishana mwishoni kwa kuwa lilikuwa refu tulienda tukakwanguana ndipo tulipoteza mwelekeo" alisema dereva huyo.

Aliongeza kuwa " mara baada ya kukwanguliwa tukilikwepa lori tukaigonga nguzo ya umeme na hapo hapo mwenzetu akafariki na tunashukuru sana wafanyakazi wa kampuni ya tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na lile lori hatukuweza kuchukua namba zake na liliendelea na safari".





No comments:

Post a Comment

Popular Posts