Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akifunga mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo viongozi wa elimu ngazi ya mikoa katika masuala ya usimamizi wa fedha za MMES II hivi karibuni katika chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia akiwaasa washiriki wa mafunzo katika masuala ya usimamizi wa fedha za MMES II kutoka mikoa 16 nchini ambao ndio watendaji wakuu katika usimamizi wa elimu, wamo Maafisa Elimu na Afisa Mipango mkoa pamoja na Maafisa Elimu wilaya, Wahandisi na Waweka hazina kutoka halmashauri za mikoa hiyo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa elimu ngazi ya mikoa katika masuala ya usimamizi wa fedha za MMES II wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati wa kufunga mafunzo hayo hivi karibuni katika chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Hawa Ghasia akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji
wa mafunzo usimamizi wa fedha za MMES II kutoka Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, TAMISEMI na chuo cha ADEM pamoja na baadhi ya
wanasemina hivi karibuni Bagamoyo.
Kauli
hiyo imetolewa mjini
Bagamoyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia wakati akifunga mafunzo ya viongozi wa
elimu
ngazi ya mikoa.
Ameongeza
kuwa mafunzo
hayo yanalenga kuboresha ujuzi na utendaji kazi wao ili kukabiliana na
changamoto zilizopo.
Waziri
Ghasia amewasihi
watendaji hao kuwa washirikiane katika kutekeleza majukumu yao ,kwani
lengo ni kufanya kazi kwa
pamoja ambapo
kila mtu anafahamu majukumu yake na mipaka yake ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Katika
hatua nyingine Waziri
Ghasia amesema kuwa kulingana
na Sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012, jumla
ya
watu milioni 14,796,537 ambao
ni sawa
na asilimia 34 wa kuanza za shule za awali, msingi na sekondari
zinazosimamiwa
na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Amefafanua
idadi hiyo
kuwa watu wa umri wa miaka 5 hadi 6 idadi yao ni 2,755,699 ambao ni sawa
na
asilimia 6.32, miaka 7 hadi 13 idadi yao ni 8,341,701 ambao ni sawa na
asilimia
19.12, miaka 14 hadi 17
idadi yao ni
3,699,137 ambao ni sawa na asilimia 8.48.
Ghasia
ameongeza kuwa
taarifa hizo ni muhimu katika kuiwezesha Serikali kupanga mipango yote
ya
kuwaendeleza watu hao katika nyanja zote.
Mafunzo
hayo
yaliwashirikisha Maafisa Elimu na Afisa Mipango wa mkoa 16 pamoja na
Maafisa
Elimu wilaya, Wahandisi, Waweka hazina pamoja na Maafisa Elimu Vifaa na
Takwimu
kutoka halmashauri za mikoa hiyo.
Baadhi
ya mikoa ambayo
watendaji wake walishiriki mafunzo hayo ni Dar es salaam, Pwani,
Morogoro,
Singida, Kigoma, Manyara, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Kigoma, Mwanza,
Shinyanga, Simiyu na Geita.
MWISHO
na fredy mgunda
No comments:
Post a Comment