Thursday, February 19, 2015

Mama aliyeporwa mtoto albino afanyiwa upasuaji wa kichwa



Geita/Dar. Mama wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ambaye alitekwa juzi na watu wasiofahamika mkoani Geita, amefanyiwa upasuaji wa kichwa na jopo la madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) mjini Mwanza.
Mama huyo aliyefahamika kwa jina la Ester Jonas (30), alilazimika kufanyiwa upasuaji huo baada ya kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na watu hao ambao walimteka mtoto wake juzi akiwa amembeba mgongoni nyumbani kwake.
Mkuu wa Kitengo cha dharura cha Hospitali ya Bugando, Dk Darick David alisema mama huyo alifikishwa hapo jana akiwa na hali mbaya kutokana na kuvuja damu nyingi.
“Namkumbuka mwanangu Yohana Bahati,” hayo ni maneno aliyoyasema mama mzazi wa mtoto huyo akiwa hospitalini hapa kwenye chumba namba 903 cha uangalizi maalumu (ICU).
“Kama mnavyomuona hali yake siyo nzuri, hata kuzungumza hawezi, alikatwa panga kichwani jeraha kubwa liko puani, tumelazimika kumfanyia upasuaji wa kichwa ili kusafisha damu iliyokuwa imeganda ndani,” alisema Dk David na kuongeza: “Bado anatatizo kubwa na madaktari bingwa wanaendelea kumchunguza.”
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Profesa Alfred Mteta alisema: “Inasikitisha kuona binadamu unamfanyia unyama binadamu mwenzako, kamwe vitendo hivi haviwezi kukubalika tumempokea mgonjwa huyu na madaktari wanaendelea kumpatia matibabu ili kuokoa maisha yake.”
Mbunge Viti Maalumu
Mbunge wa Viti Maalumu anayewawakilisha watu wenye ulemavu wa ngozi bungeni, Al-Shaymaa Kwegyir ametaka nguvu zinazotumiwa na polisi kuwakamata majambazi, zitumike pia kuwasaka wanaoteka na kuwaua watu wenye ulemavu huo.
Kauli ya Kwegyir imekuja baada ya kuanza kuibuka kwa matukio ya utekaji na kuwaua wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina.
Hivi karibuni, mtoto mwingine mwenye ulemavu wa ngozi mkoani Geita alitekwa na mama yake kucharangwa mapanga. Utekaji huo umetokea ikiwa ni siku 50 sasa tangu kutoroshwa kwa mtoto, Yohana mkoani Mwanza.
“Polisi wana nguvu za kukamata majambazi, kwanini nguvu hiyo isitumike kuwabaini wanaojihusisha na vitendo hivi, tumeanza kuwa na shaka juu ya utendaji kazi wao kuwa unaegemea upande fulani,” alisema Kwegyir.
 
 
Alisema kuna haja ya serikali na polisi kuongeza jitihada ili kumaliza tatizo hilo linaloonekana kushamiri kwa kasi.
“Nilikuwa Nyakato mwezi uliopita, kuna mtoto wa miaka minne alinusurika kunyakuliwa na watu waliokuwa kwenye pikipiki, kwa bahati nzuri mama yake alimuwahi, matukio kama haya yanaashiria kuwa hali ni mbaya,” alisema.
Barwany alia na mfumo
Akizungumzia matukio hayo, Mbunge wa Lindi Mjini (CUF), Salum Barwany ambaye pia ana ulemavu wa ngozi, alidai kutopatiwa ufumbuzi kwa tatizo hilo la utekaji na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kunaashiria kuwa wahusika wakuu wa vitendo hivyo huenda wanafahamika hivyo kuna baadhi ya watu wameamua kuwalinda.
Barwany alisema inashangaza kuona Serikali ikishindwa kulipatia uzito suala hilo kwa kuendelea kuwaacha wahusika wakiendeleza unyama wao.
“Ni jambo la aibu kwa Serikali kushindwa kuchukua hatua, tumeshapiga sana kelele mpaka inafikia hatua tumeamua kumwachia Mungu maana nguvu inapelekwa kwa waganga wa kienyeji, lakini ukweli ni kwamba kuna watu nyuma yao,” alisema Barwany na kuongeza;
“Nashangaa mambo haya yanavyoshika kasi wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu na kama mwelekeo ndiyo huu, basi tusubiri matukio mengi zaidi ya haya.”
Alifafanua kuwa viongozi wengi wa Serikali wamekuwa wakipiga kelele pale tukio linapotokea, baada ya hapo hakuna ufuatiliaji unaoendelea.
Alisema kuthibitisha hilo, hata Bunge mara kadhaa limeshindwa kujadili suala hilo kwa madai kuwa kuna mambo mengine yenye umuhimu zaidi licha ya kutambua kuwa maisha ya walemavu hao yanazidi kuwa hatarini.
Itakumbukwa, Januari 29, 2009, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alimwaga chozi bungeni mjini Dodoma kuonyesha uchungu aliokuwa nao dhidi ya mauaji ya albino yaliyokuwa yameshamiri nchini.
Alitamka wazi kuwa ‘wanaoua albino nao wauawe’.

Maalbino Geita
Chama cha Watu wenye Ulemavu wa Ngoz (Tas) mkoani Geita, kimeyahusiha matukio ya mauji hayo na Uchaguzi Mkuu huku baadhi ya wanasiasa wakitajwa kuhusika.
Kaimu Mwenyekiti wa Tas Mkoa wa Geita, Isaack Timothy akizungumza juzi baada ya tukio la mtoto Yohana Bahati(1) kutekwa Februari 15 saa 2 usiku, alisema suala hilo ni la wazi kwa kila Mtanzania ambaye akitafakari kwa makini anaweza kubaini hivyo.
Makachero kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, wamewasili Geita kuwasaka washukiwa wa utekaji wa mtoto Yohana.
Mtoto huyo mkazi wa kijiji cha Ilelema wilayani Chato mkoani Geita, alitekwa na watu wasiojulikana wakiwa wawili ambao walivamia nyumbani kwa wazazi wake na kumjeruhi mama yake.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Joseph Konyo alithibitisha kuwasili kwa makachero hao ambao wanaungana na wa Geita kuhakikisha mtoto huyo anapatikana.
“Pia tunashirikiana vya kutosha na askari wa mikoa mingine...na wananchi tunaomba watuunge mkono, wakiona kuna mtu wanamtilia shaka labda kwa kuomba maji, au kuuliza njia watoe taarifa…kuna polisi jamii huko. Kila kata na tarafa kuna polisi washirikiane na hao askari,” alisema Konyo.
Konyo alisema familia hiyo, ilikuwa na watoto watatu wenye ulemavu wa ngozi ambao ni pamoja na Shida (11) na Tabu (3) ambao kwa sasa wanahifadhiwa na Serikali ya Wilaya ya Geita.
 
 
 

Ugaidi Tanga: Wasomali Wawili Watiwa Mbaroni



 JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewatia mbaroni watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuwa na asili ya Somalia katika msako unaoendelea dhidi ya kundi la wahalifu wa silaha mkoani Tanga.
 
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mjini hapa, kimeiambia Mpekuzi kuwa watu hao walikamatwa jana saa 5 asubuhi katika eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko, baada ya kuonekana katika eneo hilo wakiwa wanashangaa na hawajui wanakokwenda.
 
Baada ya kuonekana kwa watu hao, wananchi wa kijiji hicho kilicho jirani na Kijiji cha Mleni ambako kundi la wahalifu wa silaha lilijificha, walitoa taarifa kwa polisi ambao walifika na kuwatia mbaroni.
 
“Ni kweli leo (jana) saa tano asubuhi huku eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko kuna watu wawili wenye asili ya Somalia walikamatwa baada ya wananchi kuwaona na kuwatilia shaka, na hivyo kufanikisha kukamatwa,” kilisema chanzo hicho.
 
Wakati huohuo, jeshi hilo linawashikilia watu wawili ambao ni wafanyabiashara na waumini wa dini ya Kiislamu wa Jumuiya ya Answar Suni mkoani hapa kwa tuhuma za kuhusishwa na tukio la kufadhili vikundi vya uporaji wa silaha dhidi ya polisi.
 
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, ndugu wa watuhumiwa hao walidai ndugu zao wamekamatwa na polisi siku tatu zilizopita.
 
“Kuna ndugu zetu wawili wameshikiliwa kwa mahojiano kwa zaidi ya siku tatu na hatujawahi kuwaona kila tukiwapelekea chakula na dhamana imekataliwa, hivyo hali hiyo inatupa wasiwasi mkubwa,” alisema mmoja wa ndugu wa watuhumiwa hao ambaye hakutaka jina lake litajwe.
 
Mbali na matukio ya kukamatwa watu hao, hali ya ulinzi katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo imeimarishwa, hasa katika wodi ambayo askari waliojeruhiwa kwenye tukio la Amboni wamelazwa wakiendelea na matibabu.
 
Mpekuzi  ilimpotafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraser Kashai pamoja na Kamishna Mkuu wa Operesheni na Mafunzo nchini, Paul Chagonja, wote walisema wapo katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama.  
 
SOURCE MPEKUZI
 


Wednesday, February 18, 2015

Rais Kikwete ateua Wakuu wa Wilaya, wengine watenguliwa nafasi zao

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27
*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.

Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).

(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

JUMATANO, FEBRUARI 18, 2015.


==================

Orodha nzima ya wakuu wa Wilaya Soma Hapa Chini
;

Wakuu wa Wilaya waliofariki dunia


NA JINA WILAYA
1. Capt.(mst)JamesC.Yamungu Serengeti
2. AnnaJ.Magoha Urambo
3 MoshiM.Chang’a Kalambo
Wakuu wa Wilaya walio pandishwa cheo
Wakuu wa Wilaya wafuatao wamepandishwa cheo kuwa Wakuu wa Mikoa

NA JINA WILAYA MKOAALIOPANGIWA
1. JohnVianneyMongela Arusha Kagera
2. AminaJumaMasenza Ilemela Iringa
3 Dkt.IbrahimHamisMsengi Moshi Katavi
4 HalimaOmariDendego Tanga Mtwara
5 DaudiFelixNtibenda Karatu Arusha
Wakuu wa Wilaya waliopangiwa majukumu mengine
Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa na watapangiwa kazi nyingine ni hawa wafuatao;

NA. JINA WILAYA
1 Brig.GeneralCosmasKayombo Simanjiro
2 Col.NgemelaElsonLubinga Mlele
3 JumaSolomonMadaha Ludewa
4 MercyEmanuelSilla Mkuranga
5 AhmedRamadhanKipozi Bagamoyo
6 MrishoGambo Korogwe
7. ElinasAnaelPallangyo Rombo
Wakuu wa Wilaya Wanaotenguliwa
Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana nasababu za umri, kiafya na nyinginezo na vituo vyao ni kama inavyoonekana hapa chini:

NA JINA WILAYA
1. JamesKisotaOleMillya Longido
2. EliasWawaLali Ngorongoro
3. AlfredErnestMsovella Kongwa
4. DanyBeatusMakanga Kasulu
5. FatmaLosindiloKimario Kisarawe
6. ElibarikiEmanuelKingu Igunga
7. Dr.LeticiaMosesWarioba Iringa
8 EvaristaNjilokiroKalalu Mufindi
9. AbihudiMsimediSaideya Momba
10. MarthaJachiUmbula Kiteto
11 KhalidJumaMandia Babati
12 EliasiGoroiBoeBoeGoroi Rorya
Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa
Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Wilaya zao niwafuatao;
NA. JINA JINSI WILAYA
1. MariamRamadhaniMtima KE Ruangwa
2. Dkt.JasmineB.Tiisike KE Mpwapwa
3. PololetiMgema ME Nachingwea

NA. JINA JINSI WILAYA
4. FadhiliNkurlu ME Misenyi
5. FelixJacksonLyaniva ME Rorya
6. FredrickWilfredMwakalebela ME Wanging’ombe
7. ZainabRajabMbussi KE Rungwe
8. FrancisK.Mwonga ME Bahi
9. Col.Kimiang’ombeSamwel
Nzoka
ME Kiteto
10. HusnaRajabMsangi KE Handeni
11. EmmanuelJumanneUhaula ME Tandahimba
12. MboniMhita KE Mufindi
13. HashimS.Mngandilwa ME Ngorongoro
14. MariamM.Juma KE Lushoto
15. TheaMedardNtara KE Kyela
16. AhmadH.Nammohe ME Mbozi
17. ShabanKissu ME Kondoa
18. ZeloteStephen ME Musoma
19. PiliMoshi KE Kwimba
20. MahmoudA.Kambona ME Simanjiro
21. GloriusBernardLuoga ME Tarime
22. ZainabR.Telack KE Sengerema
23. BernardNduta ME Masasi
24. ZuhuraMustafaAlly KE Uyui
25. PauloMakonda ME Kinondoni

NA. JINA JINSI WILAYA
26. MwajumaNyiruka KE Misungwi
27. MaftahAllyMohamed ME Serengeti
Wakuu wa Wilaya waliobadilishwa Vituo
Wakuu wa Wilaya wafuatao wamebadilishwa vituo vya kazi kama ifuatavyo;
NA JINA JINSIA WILAYA
ATOKAYO
WILAYA
AENDAYO
1. NyerembeDeusdeditMunasa ME Arumeru Mbeya
2 JordanMungireObadiaRugimbana ME Kinondoni Morogoro
3 FatmaSalumAlly KE Chamwino Mtwara
4 LephyBenjaminiGembe ME DodomaMjini Kilombero
5 ChristopherRyobaKangoye ME Mpwapwa Arusha
6 OmarShabanKwaang’ ME Kondoa Karatu
7 FrancisIsackMtinga ME Chemba Muleba
8 ElizabethChalamilaMkwasa KE Bahi Dodoma
9 AgnesEliasHokororo(Mb) KE Ruangwa Namtumbo
10 ReginaReginaldChonjo KE Nachingwea Pangani
11 HusnaMwilima KE Mbogwe Arumeru
12 GeraldJohnGuninita ME Kilolo Kasulu
13 BiZipporahLyonPangani KE Bukoba Igunga
14 Col.IssaSuleimaniNjiku ME Missenyi Mlele

NA JINA JINSIA WILAYA
16 Bw.RichardMbeho ME Biharamulo Momba
17 Bw.LembrisMarangushiKipuyo ME Muleba Rombo
18 RamadhaniAthumanManeno ME Kigoma Chemba
19 VenanceMethusalahMwamoto ME Kibondo Kaliua
20 GishuliMbegesiCharles ME Buhigwe Ikungi
21 NovatusMakunga ME Hai Moshi
21 AnatoryKisaziChoya ME Mbulu Ludewa
22 ChristineSolomoniMndeme KE Hanang’ Ulanga
23 JacksonWilliamMusome ME Musoma Bukoba
24 JohnBenedictHenjewele ME Tarime Kilosa
25 Dkt.NormanAdamsonSigalla ME Mbeya Songea
26 Dr.MichaelYuniaKadeghe ME Mbozi Mbulu
27 CrispinTheobaldMeela ME Rungwe Babati
28 MagrethEsterMalenga KE Kyela Nyasa
29 SaidAliAmanzi ME Morogoro Singida
30 AntonyJohnMtaka ME Mvomero Hai
31 EliasChoroJohnTarimo ME Kilosa Biharamulo
32 FrancisCryspinMiti ME Ulanga Hanang’
33 HassanEliasMasala ME Kilombero Kibondo

NA JINA JINSIA WILAYA
34 AngelinaLubaloMabula KE Butiama Iringa
35 FaridaSalumMgomi KE Masasi Chamwino
36 WilmanKapenjamaNdile ME Mtwara Kalambo
37 PonsianDamianoNyami ME Tandahimba Bariadi
38 MariamSefuLugaila KE Misungwi Mbogwe
39 MaryTeshaOnesmo KE Ukerewe Buhigwe
40 KarenKemilembeYunus KE Sengerema Magu
41 JosephineRabbyMatiro KE Makete Shinyanga
42 JosephJosephMkirikiti ME Songea Ukerewe
43 AbdulaSuleimanLutavi ME Namtumbo Tanga
44 ErnestNg’wendaKahindi ME Nyasa Longido
45 AnnaRoseNdayishimaNyamubi KE Shinyanga Butiama
46 RosemaryKashindiKirigini
(Mb)
KE Meatu Maswa
47 AbdallahAliKihato ME Maswa Mkuranga
48 ErastoYohanaSima ME Bariadi Meatu
49 QueenMwanshingaMulozi KE Singida Urambo
50 YahyaEsmailNawanda ME Iramba Lindi
51 ManjuSalumMsambya ME Ikungi Ilemela
52 SaveliMangasaneMaketta ME Kaliua Kigoma
53 BituniAbdulrahmanMsangi KE Nzega Kongwa
54 LucyThomasMayenga KE Uyui Iramba

NA JINA JINSIA WILAYA





55 MajidHemedMwanga ME Lushoto Bagamoyo
56 MuhingoRweyemamu ME Handeni Makete
57 HafsaMahinyaMtasiwa KE Pangani Korogwe
58 Dr.NasoroAliHamidi ME Lindi Mafia
59 FestoShemuKiswaga ME Nanyumbu Mvomero
60 SaudaSalumMtondoo KE Mafia Nanyumbu
61 SelemanMzeeSeleman ME Kwimba Kilolo
62 EsterinaJulioKilasi KE Wanging’o
mbe
Muheza
63 SubiraHamisMgalu KE Muheza Kisarawe
64 JacquelineJonathanLiana KE Magu Nzega

Wakuu wa Wilaya wanaobaki katika vituo vyao vya sasa

Wakuu wa Wilaya wafuatao wanaendelea kubaki katika vituovyao vya sasa;
NA JINA JINSIA WILAYA
1 JowikaWilsonKasunga ME Monduli
2 RaymondHieronimiMushi ME Ilala
3 SophiaEdwardMjema KE Temeke
4 Bw.AmaniKiungaduaMwenegoha ME Bukombe
5 Bw.IbrahimWankangaMarwa ME Nyang’wale
6 Bw.RodrickLazaroMpogolo ME Chato
7 Bw.ManzieOmarMangochie ME Geita
8 Bi.DarryIbrahimRwegasira KE Karagwe

9 Lt.Col.BenedictKulikilaKitenga ME Kyerwa
10 ConstantineJohnKanyasu ME Ngara
11 PazaTusamaleMwamulima ME Mpanda
12 PeterToimaKiroya ME Kakonko
13 HadijaRashidNyembo KE Uvinza
14 Dkt.CharlesO.Mlingwa ME Siha
15 ShaibuIssaNdemanga ME Mwanga
16 HermanClementKapufi ME Same
17 EphraimMfingiMbaga ME Liwale
18 AbdallahHamisUlega ME Kilwa
19 JoshuaChachaMirumbe ME Bunda
20 DeodatusLucasKinawiro ME Chunya
21 RosemaryStakiSenyamule KE Ileje
22 GulamhuseinKifuShaban ME Mbarali
23 ChristopherEdwardMagala ME Newala
24 BarakaMbikeKonisaga ME Nyamagana
25 SarahPhilipDumba KE Njombe
26 HanifaMahmoudKaramagi KE Gairo
27 HalimaMezaKihemba KE Kibaha
28 NurdinBabu ME Rufiji
29 MathewSarjaSedoyeka ME Sumbawanga
30 IddHassanKimanta ME Nkasi
31 ChandeBakariNalicho ME Tunduru
32 BibiSenyiSimonNgaga KE Mbinga
33 WilsonElishaNkambaku ME Kishapu

34 BensonMwailugulaMpesya ME Kahama
35 PaulChrisantMzindakaya ME Busega
36 GeorginaEliasBundala KE Itilima
37 FatumaHassanToufiq KE Manyoni
38 Lt.EdwardOleLenga ME Mkalama
39 HanifaMohamedSelengu KE Sikonge
40 SulemanOmarKumchaya ME Tabora
41 MboniMwanahamisMgaza KE Mkinga
42 SelemanSalumLiwowa ME Kilindi

Mabadiliko haya yameanza tarehe 18.02.2015 na ninawatakia woteutendaji kazi mahiri.


Mizengo K. P. Pinda
18.02.2015WAZIRI MKUU

Popular Posts