Monday, July 6, 2015

Dr Shein Apitishwa Kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar

 


Kamati kuu maalum ya chama cha mapinduzi Zanzibar kwa kauli moja imempitisha Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi.
 
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wajumbe wa NEC wa Zanzibar wanounda kamati maalum ya Zanzibar kukutana hapa Zanzibar katika ofisi kuu ya CCM na kuamua kumuidhinisha Dr Shein kugombea tena  kiti hicho cha urais baada ya wajumbe karibu 102  ambao ni aslimia 83  kuridhia Dr Shein agombee.
Awali Dr Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar alilazimika kuondoka ndani ya kikao ili ijadaliwe na wanachama hao ambapo kiti hicho kilishikwa kwa muda na Dr Mohamed Gahribu Bilali makamu wa rais, ambapo baadaye akizumgumza na wanaccm hao waliokubali Dr Shein aliwahidi wanachama wa CCM kuwa  uamuzi wake uko palepale wa kutekeleza ilani ya CCM ya kuitumikia Zanzibar.
Katika hatua nyengine naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar akizungumza baada ya kikao hicho alisema CCM haiwezi kupinga au kukubali suala la majimbo,wao wanasubiri maamuzi ya tume na wako tayari kwa umauzi wowote utakaotolewa na tume ya uchaguzi ambayo inatarajiwa kutangaza majimbo mapya leo asubuhi.
Kupitishwa kwa Dr Shein kugombea urais wa Zanzibar na kamati maalum ni hatua ya kwanza na sasa shuguhli yote inahamia Dodoma ambapo jina la Dr Shein litajadiliwa na kamati kuu na baadaye kutakiwa kuidhinishwa na kupitishwa na halmashuri kuu ya CCM, nafasi ya urais wa Zanzibar inaamuliwa na NEC na siyo na mkutano mkuu waccm.

EDSONI KAMUKARA PUMZIKA KWA AMANI













 Edson Slavatory Kamukara, amezikwa kijijini kwao Ihangiro wilayaniMuleba, huku akiacha majonzi kwa familia yake, baada ya kuacha mtoto mmoja ilhali mama yake akisumbuliwa na kupooza, ambapo siku chache zilizopita, Edson alitokea Muleba kumuangalia mama yake, kama alivyozungumza dada wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Joyce.


 Akizungumza katika maziko hayo, mkurugenzi wa kampuni ya mwana halisi publishers LTD Bwana Said Kubenea, amesema kifo cha marehemu Kamukara, kimezua utata kutokana na hakuna anayejua undani,
huku akisema kuwa madakatari wanasema inaonekana alikufa baada ya kukosa hewa huku, chumbani kwake kukikutwa na damu, akiongeza kuwa alikuwa anakamilisha kazi ya uandishi uliokuwa ukiwahusu vigogo na kama habari zake zingetoka, saizi nchi ingekuwa inaongea mambo mengine.




Waadishi kutoka chama cha waandishi  habari mkoani Kagera KPC, walishiriki maziko hayo na ndiyo walihusika kubeba mwili wa marehemu na picha chini ni Charles Mwebeya akitroa rambirambi yao kwao dada Joyce ambaye anaishi Dar na alikuwa karibu na marehemu














 Marehemu Edson Kamukara, ameacha mtoto anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 3 hadi 4 aitwaye  Edigar Ishengoma, na marehemu alianzia kazi ya uandishi katika gazeti la Majira, akafanya jambo leo, tanzania dai, na hatimaye mwanahalisi publishers ambapo amefanyia kwa kipindi cha miezi minne, na alikuwa anakamilisha habari kuhusu matatizo ya wananchi kupitia viongozi mkoani Kagera.
Na Mwanaharakati.







MWENGE WAZINDUA MIRADI YA THAMANI YASHILINGI BILIONI KUMI NA TATU NJOMBE



Miradi ya Shilingi billion Kumi na  tatu (13,201,109,235.55) inatalajiwa kuzinduliwa,kuwekewa jiwe la Msingi na kukaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Njombe,hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe  Dk.Rehema Nchimbi wakati akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Iringa.
Nchimbi alisema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Njombe utakimbizwa katika halmashauri Sita ambazo ni Njombe,Makete,Ludewa,Wanging’ombe,Mji Njombe  na Mji Makambako,Katika halmashuri jumla ya
Miradi 45 itatembelewa na Mwenge wa Uhuru.
Alisema kuwa Miradi hiyo ipo katika sekta ya Afya ,Elimu,Kilimo,Miundombinu,Utalii na Misitu,miradi mingi imekamilika na kuanza kutumika .
Naye mkimbiza Mwenge Kitaifa  Juma Khatibu chum alisema kuwa amefurai kuingia Mkoa wa Njombe  na anarajia kufungua,kukagua miradi mizuri kwani kutokana na mapokezi walioyapata ya wananchi wengi  waliojitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru, Kauli mbiu ya Mwenge Mwaka huu ni “Tumia haki yako kidemokrasia ,Jiandikishe  na kupiiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2015.




Popular Posts