Edson Slavatory Kamukara, amezikwa kijijini kwao Ihangiro
wilayaniMuleba, huku akiacha majonzi kwa familia yake, baada ya kuacha
mtoto mmoja ilhali mama yake akisumbuliwa na kupooza, ambapo siku chache
zilizopita, Edson alitokea Muleba kumuangalia mama yake, kama
alivyozungumza dada wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Joyce.
huku akisema kuwa madakatari wanasema inaonekana alikufa baada ya kukosa hewa huku, chumbani kwake kukikutwa na damu, akiongeza kuwa alikuwa anakamilisha kazi ya uandishi uliokuwa ukiwahusu vigogo na kama habari zake zingetoka, saizi nchi ingekuwa inaongea mambo mengine.
Waadishi kutoka chama cha waandishi habari mkoani Kagera KPC, walishiriki maziko hayo na ndiyo walihusika kubeba mwili wa marehemu na picha chini ni Charles Mwebeya akitroa rambirambi yao kwao dada Joyce ambaye anaishi Dar na alikuwa karibu na marehemu
Marehemu Edson Kamukara, ameacha mtoto anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 3 hadi 4 aitwaye Edigar Ishengoma, na marehemu alianzia kazi ya uandishi katika gazeti la Majira, akafanya jambo leo, tanzania dai, na hatimaye mwanahalisi publishers ambapo amefanyia kwa kipindi cha miezi minne, na alikuwa anakamilisha habari kuhusu matatizo ya wananchi kupitia viongozi mkoani Kagera.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment