Wednesday, May 14, 2014

AJALI YA DALADALA FRELIMO IRINGA MCHANA HUU..

























https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWmPBrGxkhdgJc8VAZa9Vcpt7SQm5AVToQnuy8GJCQ4Dlx8AEeu6Uac8O1mVR1Yrb2Tj6Vh2DeSE-TDNuhB63L9qm4MauPqko8XqCiUbDSK8BbmxqA1nl0h5HUFHszBt_1intX5rOpzzPx/s1600/DSC02650.JPG

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgK4oL21rrT6NRCw1AHTw-cx7LamPzNxBOLK45nsBwtONWH_HY7jL9CVtk93MGePoVeUdA0V_vJsaFMe8dnZKfwh1sPBbYPHXhQ2YdZFGvy7WGlErEiUYHDLAaIwAkxBzSD5HZCMQv1WIsA/s1600/DSC02654.JPG

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTC-i9ivKGnLmosUsrlFeYF3aSDyG-KaRPpWIz3u0a8jJWc9o6BNahcM_SmtMtpMB93SNVG4arkZKdPvHMykvGC-0jqlBtx9dKJCR7pfCf_Vig8xMJzBsAk7hjTEiOqVGTxN12RliHza9E/s1600/DSC02651.JPG

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdquUKb-IeR9TGKOk0mlSYUD169Mo0NCKTCown8kEBEnEa4afSpIXB6K3iQUggDAvsPNs2uDdv4xSMqfnsw3R_QclS9PPxWfXnQn42B1Nw_vClgJeUrFnXba7dOa0ZfjWaQ5FWZ-nMiDHL/s1600/DSC02657.JPG

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPhyphenhyphen5K-rPhVp1MvEr__x-qj8Tl9SFyID8G867aGPgu5iDB-xOus3NE8k6gXBNe097bypUXD2WiICw0hLZJMvRHZHNUm9zWDMW4FjKFm6JAF3PC9Ki3HxJyW8vhlrlVahYx0wg2RW8rs5kG/s1600/DSC02660.JPG

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-hlmNiGEwuR1WZm83iWzKJ3TzHmzAqn-17pi8MHDuX5hCvwENmkugk-m9puae1wRtDSKKTfAOHLsYXJxSq9HlPCopCS715Ng5dLmQWsXQbMF3nOZr8z-SslbMAFPKewamdl3DBsKuCXd_/s1600/DSC02663.JPG

FRANK KIBIKI, IRINGA
ZAIDI ya watu kumi, wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa, baada daladala waliyokuwa wakisafiria kutoka Frelimo kwenda Tumaini, mjini Iringa kuacha njia na kuanguka.
Ajali  hiyo imetokea mchana huu majira ya saa saba mchana, baada ya gari hiyo kushindwa kupanda mlima, na badala yake kurudi nyuma kabla ya kutumbukia kwenye mto.
Mwitikio imewashuhudia wasamaria wema wakiokoa majeruhi waliokuwa wamepanda daladala hiyo yenye namba za usajili, T 106 ABP ambao wote wamekimbizwahospitali kwa ajili ya matibabu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwamba taarifa zaidi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
.

AJIRI WA ZAMANI, NA MMILIKI WA KWANZA WA GARI AINA YA KOSTA MKOANI IRINGA ATANGAZA KUUZA FIGO YAKE












MKAZI wa Iringa Mjini, Ramadhan Mrisho (Makosa), ametangaza kuuza figo yake moja kwa kile anachodai anatafuta fedha za kumsaidia kuendesha maisha yake.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni mjini Iringa, Mrisho, alisema amefikia uamuzi wa kutangaza kuuza figo yake akiwa na akili timamu.
 “Nisidhaniwe nimekuwa na akili tofauti,” alisema Mrisho na kuongeza; “Nina akili timamu, nimeamua kuchukua uamuzi huu kama nilivyosema kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.”
Hata hivyo Mrisho hakuwa tayari kutaja bei ya figo yake iwapo atapatikana mteja. Alisema anajua wapo watu wenye matatizo ya figo na wamekuwa wakisafiri mbali na nchi kutafuta tiba.
“Kama kuna mtu ana matatizo ya figo au ameitafuta ameikosa aje kwangu tukubaliane bei,” alisema Mrisho.
Katika harakati zake za kutafuta fedha za kusaidia familia yake, Julai, 2012 Mrisho alitishia kujinyonga, tukio alilopanga lifanyike Uwanja wa Samora kwa sharti kuwa mashuhuda kutalipa kiingilio ambacho kingekusanywa kwa ajili ya familia yake.
Wakati huo huo, Mrisho alinukuliwa akisema kuliko familia yake kuendelea kutaabika ni bora ajitoe mhanga ili fedha zitakazopatikana kama kiingilio zitumike kusaidia watoto yake.
Hata hivyo, alisema mpango wake haukufanikiwa kwani akiwa kwenye maandalizi walitokea watu mbalimbali wakiwemo Polisi waliompa ushauri nasaha, hivyo alisitisha mpango huo.
“Sasa nimekuja na mpango mpya, mpango huu si mwingine zaidi ya huu wa kuuza figo yangu moja, naamini nikifanikiwa nitapata fedha,” alisema.
Mrisho ambaye ni maarufu mkoani Iringa kutokana biashara zake zake nyingi alizokuwa akifanya mwanzoni mwa miaka ya tisini baada ya kuacha kazi yake ya ubaharia.
Wakati akifika mjini Iringa, Mrisho alikuwa hanywi pombe, bali alikuwa mnyenyekevu ambapo alijikita kuisaidia jamii ya watu wa Iringa kutunza mazingira kwa kupanda miti kila mtaa.
Aliongoza kupanda miti ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda inayoonekana mjini Iringa.
Mrisho ndiye alikuwa mtu wa kwanza mjini Iringa kuingiza mabasi madogo ya kusafirisha abiria aina ya Coaster yaliyokuwa yakifanya kazi katika maeneo mbalimbali ya mjini Iringa.
Pamoja na biashara ya usafirishaji, Mrisho alijikita katika biashara ya hoteli. Na kwa muda mrefu aliendesha hoteli ya CATS iliyopo jirani na Maktaba ya Mkoa wa Iringa.
Kwa kadri biashara ilivyozidi kumchanganyia katika hoteli hiyo, alimua kuibadili jina na kuiita MAKOSA CATS Hotel.
Katika hoteli hiyo bendi nyingi zimepiga muziki na kwa mara ya mwisho, mwanamuziki Macay Fanta alikuwa akifanya shoo zake mpaka pale Mrisho aliposhindwa kuiendesha mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Mtandao wa biashara za Mrisho haukuishia hapo, alikuwa pia akimiliki hospitali maarufu sana iliyopo jirani kabisa na Soko Kuu la Mjini Iringa, ambayo ilikuwa ikiitwa MAKOSA.
Alisema biashara zote hizo haziko tena mikononi mwake na ugumu wa maisha unazidi kumwandama. Alisema anatafuta njia za kujikwamua na njia halali anayoiona mbele yake hivi sasa ni kuuza figo yake moja.
Chanzo:Majira

Tuesday, May 13, 2014

MIKATABA YA UKARABATI WA BARABARA ZA ITONI- LUDEWA-NKOMANG’OMBE,MCHUCHUMA ACCESS NA MKIU-LIGANGA KWENDA MAENEO YA MIGODI YA MCHUCHUMA.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wawekezaji toka china inakusudia kuanza uchimbaji wa Madini ya Chuma na Makaa ya mawe yaliyopo Mkoa wa Njombe katika vijiji vya Liganga na Mchuchuma mapema mwaka 2014.
 
Ili kufaninikisha  uchimbaji imeonekana kuna umuhimu wa kukarabati barabara na madaraja ili kufanikisha usafirishaji wa mitambo mizito inayofikia tan 150,urefu wa mita 15 na upana wa mita 6.3 kwa baadhi ya mitambo hadi maeneo ya migodi.
 PICHA KUTIA SAINI UTENGENEZAJI WA ITONI -LUDEWA.




























Popular Posts