FRANK KIBIKI, IRINGA
ZAIDI ya watu
kumi, wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Iringa, baada daladala waliyokuwa wakisafiria kutoka Frelimo kwenda Tumaini,
mjini Iringa kuacha njia na kuanguka.
Ajali hiyo imetokea mchana huu majira ya saa saba
mchana, baada ya gari hiyo kushindwa kupanda mlima, na badala yake kurudi nyuma
kabla ya kutumbukia kwenye mto.
Mwitikio
imewashuhudia wasamaria wema wakiokoa majeruhi waliokuwa wamepanda daladala
hiyo yenye namba za usajili, T 106 ABP ambao wote wamekimbizwahospitali kwa
ajili ya matibabu.
Kamanda wa
jeshi la polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo kwamba taarifa zaidi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
.
No comments:
Post a Comment