Akizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com
ofisini kwake Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji mkoani Iringa Ispekta
Shomari Salla alisema kuwa jengo lolote linalojengwa kwa ajili ya biashara ni
lazima likaguliwe ramani ya jengo hilo na kikosi cha zimamoto pamoja na mipango
miji kabla halijaanza kujengwa.
“kanuni
ya ukaguzi ya mwaka 2007 na hati ya mwaka 2008 ya zima zoto imeainishwa kuwa
jengo la gorofa la aina yeyote ile ni lazima likaguliwe kabla ya kujengwa
haijalishi lipo maeneo gani yawe ya mkusanyiko au sio ya mkusanyiko ni lazima
ramani ya mchoro wa hilo jengo upelekwe kwa mipango miji waukague halafu uje
kwetu pia tuukague kwanza ndipo tumruhusu huyo mtu aendelee na ujenzi wake na
tutamruhusu tu endapo kama atakuwa ametimiza hayo masharti na pia kama sisi
tutakuwa tumeridhishwa na vigezo alivyovileta kwetu tuviangalie, kama hatokuwa
na hivyo vigezo basi hatuwezi kumruhusu kujenga jengo lolote lile” alisema
Salla.
Hata
hivyo aliwataka makandarasi kuwaruhusu na pia kuwapa ushirikiano watu wanaoenda
kukagua gorofa ambalo litakuwa bado linajengwa, na kwa upande wa wamiliki wa
majengo hayo watafute wakandarasi wenye ujuzi na uzoefu mzuri wa ujenzi ili
majengo yao yajengwe kwa uimara zaidi na pia alitoa onyo kwa yeyote
atakayekiuka masharti hayo na kujenga bila kibali basi hatua kali za kisheria
zitachukuliwa.
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
No comments:
Post a Comment