Monday, August 11, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MALAWI PROFESA PETER MUTHARIKA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI






Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika akisalimiana na Rais Jakaya  Kikwete alipomtembelea kumjulia hali Rais Kikwetev  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  na wake zao, Mama Salma Kikwete na Mama Getrude Mutharika,  wakiongea kwa furaha walipokutana  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao   walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya  nchi hizo mbili.
PICHA NA IKULU












RPC NGONYANI WA NJOMBE APATA AJALI NA BODYGAD WAKE AFARIKI PAPO HAPO



 Hilo ndio gari la RPC Ngonyani baada ya ajali

 


 

 Muonekana wa Gari la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe BAADA YA AJALI USIKU HUKO TANWATT, KIBENA  Njombe.Picha na Gabriel Kilamlya


Taarifa ambazo zimetufikia katika chumba chetu cha habari muda huu zinasema kwamba kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani amepata ajali mbaya ya gari usiku wa kuamkia leo akitoka Makambako kuelekea Njombe

Kwa mujibu wa taarifa ajali hiyo imesababisha kifo cha "body guard" wa kamanda Ngonyani ajulikanaye kama H580 PC Geroge kufariki dunia papo hapo, huku kamanda Ngonyani na dereva wake Nwaka Seme wakinusurika na kwa sasa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Njombe

Akizungumza na mwandishi wetu Katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe Muuguzi wa Zamu Bi.Neda Chelesi Amesema Kuwa Ajali Hiyo Imetokea Maeneo ya TANWATT Karibu na Jengo la TANSEED Kibena Usiku wa Kuamkia leo Agosti 9 Mwaka Huu na Kwamba Katika Ajali Hiyo Amepokea Majeruhi Wawili na Maiti Moja

Chanzo cha ajali hiyo inayodaiwa kutokea majira ya saa tano usiku hakijafahamika na  taarifa zaidi utazidi  kupata endelea kutufuatilia.

KAMANDA wa polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  pamoja na dereva wake Nuaka Seme  wamelazwa katika hispitari ya Mkoa wa Njombe ya kibena ambako wanaendelea  kupatiwa matibabu kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia  jana katika eneo la kiwanda cha Miwati (TANWAT) ambapo katika ajali hiyo askari mwenye cheo cha "constable" alifariki dunia papo hapo.

Akiongea na vyombo vya habari  huku akipatiwa matibabu katika hospitari ya Mkoa kutokana na Mnadhimu wa Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe ASP Yahaya  rajab kushindwa kuongea kwa madai kuwa hanaruhusa Kamanda Ngonyani alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu hadi saa nne za usiku katika barabara ya  Makambako hadi Njombe.

Aidha Jeshi la Polisi  limesema kuwa  katika ajali hiyo aliyefariki dunia ni George  Stephano  Matiko (24)



 H580 Pc George  Enzi za uhai wake.
Nuaka Sema aliyekuwa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili PT 2058  alisema kuwa kutokana  gari hilo la mizigo kukaa katikati ya barabara walishindwa kupishana kwa wakati na kuligonga kwa nyuma na baadae kukutana uso kwa uso na nguzo ya umeme iliyowasababishia ajali.

"ghafla niliona gari mbele likiwa limewasha taa zote za mbele (full light) likiwa upande wetu na nilivyoona hivyo niliwasha taa kuashiria hatari  na ndipo mwenye gari la mizigo alianza kukwepa kuelekea upande wake na wakati tukipishana mwishoni kwa kuwa lilikuwa refu tulienda tukakwanguana ndipo tulipoteza mwelekeo" alisema dereva huyo.

Aliongeza kuwa " mara baada ya kukwanguliwa tukilikwepa lori tukaigonga nguzo ya umeme na hapo hapo mwenzetu akafariki na tunashukuru sana wafanyakazi wa kampuni ya tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na lile lori hatukuweza kuchukua namba zake na liliendelea na safari".





Saturday, July 26, 2014

BREAKING NEWS : BASI LA HOOD LAPATA AJALI MBAYA ASUBUHI HII LIKITOKEA MBEYA


 Muda mchache baada ajali kutokea 












  Askari wa usalama wa barabarani wakiwa wamefika eneo la tukio  na baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo







 


 Basi la Hood limepata ajali asubuhi hii likitoka Mbeya haijafahamika mara moja lilikuwa linaelekea wapi na haijafahamika kama kuna watu waliojeruhiwa, endelea kufutilia hapa kupata taarifa kamili hii ni taarifa ya awali.

Picha na Mbeya yetu Blog














Friday, July 25, 2014

Maandamano makubwa yamefanyika katika ukingo wa Magharibi mwa Palestina karibu na mpaka wake na Israel kupinga mashambulio yanayofanywa na Israel.

Waandamanaji hao wakiwa na hasira wakiwa Gaza walipambana na vikosi vya usalama vya Israel.
Hata hivyo mapambano makubwa dhidi ya vikosi vya usalama ilikuwa katika eneo la Qalandia katika mpaka wa Ramallah and Jerusalem.
Raia mmoja wa Palestinian ameuawa katika maandamano hayo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa .
Takriban wapaelestina 800 wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza mapema mwezi huu.

Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali.

Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.
Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa.
Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
„Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa.Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua"
Ameongeza kuwa waziri wa ulinzi wa ufaransa alikuwa akisaidia katika utafutaji wa ndege hiyo.
"Waziri wa ulinzi wameviruhusu vyombo vyao kwenda kwenye eneo kuitafuta ndege. Majeshi ya Algeria na Umoja wa mataifa wanafanya hivyo pia. Ndege mbili za jeshi la ufaransa zilizopiga kambi Niyame hivi sasa na tangu asubuhi zimekua zikiitafuta ndege hiyo. Majeshi yetu katika eneo hilo ikiwamo vifaa vya matibabu vyote viko tayari"
Hapo awali, waziri mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal alitoa ufafanuzi wa tukio la kuanguka kwa ndege hiyo.
"Usiku wa jana kama saa 9 ndege ya Hispania iliyokodiwa na Shirika la Ndege la Algeria ilikuwa katika safari yake kati ya Ouagadougou na Algiers. Ilipoteza mawasiliano na Rada muda huo wa saa tisa usiku dakika 10 tu baada ya kupaa. Mawasiliano ya mwisho ilikuwa na mnara wa kuongozea ndege ulioko Niger na ndege ilikuwa juu ya Gao, kama kilomita 500 kutoka kwenye mpaka wa Algeria. Kulikuwa na abiria 119 wakiwamo wafanyakazi wake. Utafutaji bado unaendelea na tunawasiliana na mamlaka zinazohusika. Waliokuwa kwenye ndege ni raia wa Algeria pamoja na mataifa mengine"
Mamlaka zinazohusika nchini Burkina Faso ambako ndiko ndege ilitokea wameamua kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafamilia wa wale waliokuwa katika ndege. Baadhi ya ndugu wamefika katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou kufuatilia taarifa kuhusu ndugu zao. Baadhi walikuwa na malalamiko
"Tuwanataka watuambie kama ndege hiyo imeanguka, kuna walionusurika, au wote wamekufa. Hayo ndio tunayotaka kujua. Tupo kwenye wakati mgumu. Watatu miongoni mwetu, tulitaka kusafiri na dada yetu lakini tuliamua kuahirisha safari katika dakika za mwisho. Hata hivyo dada yetu yeye aliondoka usiku jana."
Mwaume mwingine aliyekuwepo kwenye uwanjahuo wa ndege alisem
a

MBUNGE MGIMWA ATUMILIA MILIONI 42 KWA MIEZI MIWILI KUTEKELEZA AHADI



 Katibu  wa  mbunge wa  jimbo la Kalenga Bw Martine Simangwa  kushoto akikabidhi sehemu  bati kwa  viongozi wa kijiji  cha Makota kata ya Mseke

 

 katibu  wa  mbunge Mgimwa Bw  Simangwa akizungumza na  wananchi wa kijiji cha Malagosi 

 

 Sehemu ya saruji  iliyotolewa na  mbunge Mgimwa


 
 Mbunge Mgimwa wa pili  kulia   kulia akikabidhi msaada wa  Saruji kwa  viongozi wa kata ya Nzihi  

 
 Mbunge Mgimwa akiwa katika  usafiri wa Baiskeli 

MBUGE wa  jimbo la kalenga  Gopdfrey Mgimwa ametumia  zaidi ya  Tsh milioni 42   kutekeleza ahadi mbali mbali zilizoachwa na  marehemu babake Dr Wiliam Mgimwa.

Mbunge  Mgimwa amefananikiwa  kutekeleza ahadi hizo ndani ya kipindi  kifupi  cha miezi miwili  toka alipoapishwa  kuwa  mbunge wa  jimbo hilo









 

Popular Posts