Thursday, December 4, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI -KITAIFA YAMEFANYIKA VIWANJA VYA SABASABA MJINI NJOMBE

 Makamu wa Rais akisalimiana na viongozi mbalimbali walioudhuria Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI yaliofanyika Mkoa wa Njombe







Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr.Rehema Nchimbi ( aliyevaa T-shirtNyekundu) akicheza  na wanakwaya wa KKKT Makambako

Sunday, November 16, 2014

MKUU WA MKOA WA NJOMBE DK.REHEMA NCHIMBI APOKELEWA KWA SHANGWE NJOMBE

 Dk.Rehema Nchimbi akisalimiana na baadhi ya watumishi kwenye ofisi yake
Mkuu wa Mkoa wa Bibi Rehema Nchimbi akipokea ua kutoka kwa Bibi Linda Chatila





























Thursday, September 25, 2014

SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) LATOA ELIMU YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWA WATUMISHI WA UMMA.

Shirika la kazi duniani kushirikiana na Ofisi ya Rais Sekretalieti ya Utumishi wa Umma imezindua elimu ya kujinginga na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwa watumishi wa umma katika mkoa wa Njombe,uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashuri ya Njombe na ulizinduliwa na katibu Mkuu utumishi Bwan. Gorgeg Yambesi.
Katibu Mkuu aliwataka watumishi kujitokeza na kupima afya zao ili kujitambua mapema na serikali iweze kuwasidia,kwa kuwawezesha kwa kuwapa huduma bora ili waweze kufanya kazi kwa amani na ufanisi.
Yambes alisema kuwa uzinduzi  huwo wa kupima maambukizi ya UKIMWI kwa hiari kwa watumishi  umefanyika katika Mkoa wa Njombe kutoka na Mkoa huo kuwa na kuongoza kwa Maambukizi.

Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Njombe Bibi Salara Dumba alisema kuwa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya Ukimwi kwa asilimi 14.8 na kufutiwa na Iringa asilimia 9.1.
Dumba alisema Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi kutoka na Mila potofu kama vile kurithishana wajane,kutakasa wagane na wanaume kutofanya tohara.
Naye mwakislishi wa Shirika la kazi Duniani Bibi Getrudi Sime alisema shirika hilo limelidhia Mkataba wa mwaka 2010 kwa kutambua kuwa VVU na UKIMWI una athari kubwa kwa jamii na uchumi kwa ulimwengu wa kazi katika sekta  rasmi na zisizo rasmi.










Tuesday, September 9, 2014

TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA MAGEREZA KUHUSU TAARIFA ZA UZUSHI ZINAZOZAGAA KUWA BABU SEYA NA MAWAE WAMEACHIWA HURU

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).



Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.

Monday, September 8, 2014

MBIO ZA MWENGE NYUMBANI KWA MWALIMU NYERERE WILAYA YA BUTIAMA






Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mara wakiwa nje ya lango la Nyumba ya Baba wa taifa hayati Mwl Julius Nyerere wakingojea Mwenge wa uhuru ukiwa umechukuliwa kwenda kuwasha Mwenge wa Mwingo hivi karibuni.  

 

 Kiongozi w mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2012 kapt Honest Ernest Mwanossa akitamka manane Sisi tumekwisha uwasha Mwenge na kuuweka mlima Kilimanjaro,baada ya kuwasha Mwenge uliopo Mwitongo Nyumbani kwa Baba wa taifa hayati Mwl Julius K Nyerere.






































 

Popular Posts