Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na
mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili
wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni
Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa
jina la Papii Kocha).
Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote
zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga
kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea
kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.
Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na
uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo
waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea
kuusambaza ni kosa kisheria.
Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini
wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa
lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi
yake.
Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Umati wa watu wakisubiri kutambua maiti za watu waliofariki katika ajali ya basi la Majinja Express katika chumba cha kuhifadhia maiti ...
-
UZEMBE wa dereva wa basi Mitsubishi Fuso, mali ya kampuni ya Another G Trans lenye usajili Namba T.927 CEF, Nicolaus Magula (30) umes...
-
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain (mst) Aseri Msangi amemwagiza Mkurugenzi wa halmashuri ya wilaya ya Njombe kuakikisha barabara kutoka Ikond...
-
Askari wawili wa Jeshi la Polisi katika Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani, wameuawa baada ya kushambuliwa kwa silaha na m...
No comments:
Post a Comment