WAZIRI
wa Ujenzi Dk. John Magufuli, ametumia nafasi ya uwekaji wa jiwe la
msingi katika barabara ya Mbande Kwangwa kuwatisha wananchi kuwa iwapo
watachagua viongozi nje ya CCM watashidwa kufungua barabara hiyo.
Magufuli, alitoa kauli hiyo wakati akitoa utangulizi wa kumkaribisha
Rais Jakaya Kikwete katika uzinduzi wa barabara ya Mbade Kongwa yenye
urefu wa kilometa 5 zilizogharimu sh bilioni 2.9.
Alisema kuwa juhudi ambazo zinafanywa na serikali ya CCM za
kuwajengea barabara wananchi wa maeneo mbalimbali ili kuhakikisha
wanarahisisha uchumi wao.
“Leo wananchi wa Kongwa nataka niwaambie kuwa, tunaweka jiwe la
msingi na nataka kuwahakikishia kuwa barabara hii itafunguliwa na wewe
Rais Kikwete kabla hujamaliza muda wako, pia ni lazima tumalize ujenzi
wa barabara yote yenye urefu wa kilometa 101.1.
“Nataka niwaambie watani zangu Wagogo, mkiweka madarakani mtu kutoka
nje ya CCM, kuna uwezekano mkubwa akaja kufungua kipande hiki cha
kilometa tano tu na kwingine akapaacha bila kupajenga, sasa nataka
niwaambie mkifanya mchezo mwafaaa… lakini sipigi kampeni,” alisema Dk
Magufuli.
Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kuwa ni aibu kwa nchi kama
Tanzania, kuendelea kuomba omba kwa wafadhili kwa ajili ya ujenzi wa
barabara.
Chanzo;Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment