Watumishi
wa afya katika halmashauri za wilaya za Masasi, Newala na Mtwara
Vijijini watanufaika na nyumba 30 zilizojengwa kwenye vituo vyao vya
kazi. Kila Halmashauri ya Wilaya hizi itakabidhiwa nyumba 10 kwenye
hafla itakayofanyika Jumatano, tarehe19 Desemba 2012 kwenye Zahanati ya
Imekuwa iliyopo Mtwara Vijijini.
Nyumba
hizi ni miongoni mwa nyumba 90 zinazomalizika kujengwa, katika mikoa ya
Mtwara, Rukwa na Katavi. Nyumba hizi zinajengwa na Taasisi ya Benjamin
William Mkapa HIV/AIDS Foundation kwa ushirikiano na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kupitia mradi wa uimarishaji wa mfumo wa sekta ya afya
(Health Systems Strengthening), unaofadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa
Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria- Mzunguko wa 9.
Mgeni
rasmi katika hafla hiyo atakuwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, ambaye pia ni Msarifu wa
Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation.
Vifuatavyo ni vituo vya tiba ambavyo nyumba hizi 30 zimejengwa :
Zahanati za Mahoha, Malatu, Tawala, Kiridu 1 na Chihanga kwenye Halmashauri ya Newala.
-Zahanati za Imekuwa, Kawawa, Kilombero, Narunga na Kiwengulo zilizopo katika Halmashauri ya Mtwara Vijijinii.
-Zahanati za Mnavira, Makong’onda, Mitesa, Majembe, Shaurimoyo na Nanyindwa zilizopo Halmashauri ya Masasi.
Zahanati hizi zimejengewa nyumba 1 hadi 2 kila moja, kulingana na mahitaji halisi ya vituo hivyo.
Aidha
nyumba 60 zilizobaki, zipo katika hatua ya mwisho ya ujenzi na
zitakabidhiwa rasmi kwa Halmashauri husika, kati ya mwezi Januari na Mei
2013.
Taasisi
ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii na wadau wengine wa sekta ya afya ndani na nje ya nchi, imekuwa
ikikabiliana na changamoto ya upungufu wa Watumishi wa afya ambao kwa
mujibu wa takwimu ni zaidi ya 60 nchi nzima.
Aidha
miradi na programu mbalimbali imeendelea kubuniwa, kwa nia ya kuwavutia
na kuwabakiza watumishi wa afya kuweza kufanya kazi maeneo ya vijijini,
ambayo yana changamoto nyingi za kimazingira.
No comments:
Post a Comment