Msemaji
wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Meja Josephat Musira
akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani)kuhusu Mradi wa ujenzi
wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi ambapo kwa awamu ya
kwanza idadi ya nyumba 6064 zinatarajiwa kujengwa na mpaka sasa
nyumba 1160 zimeshakamilika kwa ajili ya matumizi, wakati wa ziara ya
waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara
hiyo Mhandisi Stephen Mpapasingo.
Mkuu
wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaeleza Waandishi wa
habari (Hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji
wa Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi,
wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Wizara hiyo Meja Josephat
Musira
Mkuu
wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaonesha waandishi wa
habari (hawapo pichani) sehemu ya jiko katika moja ya nyumba hizo.
Baadhi
ya nyumba zilizojengwa eneo la Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi Nyumba 10,000 kwa ajili ya
makazi ya Wanajeshi.
Picha
na Hassan Silayo.
No comments:
Post a Comment