Tuesday, July 22, 2014

HIVI NDIVYO VIUNGO VYA BINADAMU VILIVYOKUTWA KWENYE MFUKO USIKU HUU JIJINI DAR ES SALAAM

Jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, limefanikiwa kukamata viungo vya binadamu vikiwa kwenye mifuko ya plastiki katika maeneo ya Bunju eneo ambalo ni marufu kwa uchimbaji wa kokoto.


Viungo hivyo vilivyotambulika ni  kama vile miguu iliyokauka na mafuvu ya vichwa vya binadamu huku navyo vikiwa vimekaushwa.....
 
 
 
 
 
 
 Mmoja ya Kiungo cha Mguu
 
 
 
 
 
 
 
 
 Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika  mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
 
 
 
Watu zaidi wakiwa wanaongezeka katika eneo la Tukio

Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limekamata viungo mbalimbali vya binadamu vilivyohifadhiwa ktk mifuko ya plastiki ktk machimbo ya kokoto ya Bunju nje kidogo ya jiji la Dsm

Taarifa za tukio hilo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura. 

Mpaka tunaondoka eneo la Tukio Miili ilikuwa imechukuliwa na Jeshi la Polisi kwa Uchunguzi zaidi, Taarifa kamili itatolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam.





Endelea kufuatilia hapa tukio hili hapa blog.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment

Popular Posts