Thursday, March 12, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea tarehe 11 Machi, 2015 Mafinga katika Mkoa wa Iringa katika eneo lijulikanalo kwa jina la Changarawe, ambayo imepoteza uhai wa watu zaidi ya 40 waliokuwa wakisafiri kwa basi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi la Kampuni ya Majinja Express walilokuwa wakisafiria watu hao kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam kugongana na lori lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya, hivyo kusababisha kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo kuliangukia basi.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kufuatia taarifa za vifo vya watu zaidi ya 40 huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika ajali hii mbaya ambayo imesababisha simanzi na majonzi makubwa kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu”, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huu.
“Huu ni msiba mkubwa, na Taifa kwa ujumla limepata pigo kubwa, hivyo naomba upokee salamu zangu za rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na ajali hii iliyotokea Mkoani kwako. Naomba, kupitia kwako, rambirambi zangu na pole nyingi ziwafikie watu wote waliopotelewa ghafla na wapendwa wao. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Roho za Marehemu wote mahala pema peponi, Amina”, ameongeza kusema Rais Kikwete.
Katika Salamu zake hizo, Rais Kikwete amewahakikishia wafiwa wote kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba wa ndugu na jamaa zao, lakini amesema, pamoja na machungu yote ya kupotelewa na ndugu na jamaa zao, anawaomba wafiwa wawe na moyo wa uvumilivu na subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya wapendwa wao.
Aidha, Rais Kikwete amehitimisha rambirambi zake kwa kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema watu wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo wapone haraka, ili waweze kuungana tena na ndugu na jamaa zao.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Machi, 2015

BASI LA MAJINJA EXPRESS LAPATA AJALI MUFINDI



001
Umati wa watu wakisubiri kutambua maiti za watu waliofariki katika ajali ya basi la Majinja Express katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya Mufindi.




002

 Baadhi ya ndugu waliopoteza ndugu zao katika ajali ya basi la Majinja Express wakilia kwa uchungu mara baada ya kujua kuwa moja wa ndugu zao wamefariki dunia.

 003
 Mmoja wa majeruhi ambaye jina lake halijatambulika akiwa katika hospitali ya wilaya Mufindi kwa matibabu zaidi.



004

 Mmoja wa majeruhi ambaye hali yake mbaya akipakizwa katika gari la wagonjwa kupelekwa kwa matibabu zaidi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.


 005

Umati wa watu wakiwa katika eneo la tukio mara baada ya ajali kutokea eneo tukio ambapo ajali ya basi la Majinja limepoteza watu 42 katika ajali hiyo.
(Picha na Denis Mlowe)



 
 
 
 










Mpaka saa hizi naambiwa na watu wa Iringa idadi ya waliokufa katika ajali hiyo ni 42 na maiti 32 ambazo hazijitambuliwa zimefikishwa hospitali ya mkoa wa Iringa kutoka Mafinga.
Moja wa mashuhuda wa ajali hiyo Jackson Manga alisema kama dereva wa basi hilo angezingatia ishara za taa kali alizokuwa akiwashiwa na dereva wa roli hilo kwa vyovyote vile ajali hiyo isingetokea.
Manga alisema katika eneo hilo lenye mteremko wa wastani, roli lilikuwa likipandisha na basi lilikuwa likishuka.
 
 
Alisema ukaidi wa dereva wa basi ulisababisha dereva wa roli aingie katika shimo kubwa katika eneo hilo hali iliyosababisha ashindwe kulimudu gari hilo kabla ya kuvaana uso kwa uso na basi hilo.
“Baada ya kuvaana, kontena la futi 40 lililokuwa limepakiwa katika roli hilo liliruka juu na kwa kishindo kikubwa, kubamiza na kufunika basi hilo,” alisema.
Mmoja wa majeruhi wa basi hilo, Kevin Humphrey ambaye kalazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi alisema; “tulisikia mshindo mkubwa baada ya basi letukugongana na roli hilo na mshindo huo ulisababisha na kontena iliyotoka kwenye roli hilo na kupiga juu ya basi letu.”















 

Wednesday, March 11, 2015

AJALI BASI LA MAJINJA KUTOKA MBEYA KWENDA DARE ES SALAAM LAPATA AJALI CHANGALAWE MAFINGA




Ajali mbaya sana imetokea changalawe Mafinga express, basi la Majinja lilikuwa linatoka Mbeya kulelekea Dar es salaam limeangukiwa na kontena
Idadi kubwa ya abiria wa basi hilo wanakadiriwa kufariki dunia papo hapo baada ya basi hilo la Majinja Express kugongana na lori na kuangukiwa na kontena








Thursday, March 5, 2015

Kahama: Mvua yasababisha vifo 39, zaidi ya 60 wajeruhiwa!

Maji yakiwa yametuama katika Kijiji hicho
Moja ya familia zilizoathiriwa na mvua hizo (Sio familia moja)  ambazo hazina mahali pa kuishi



 













RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA KAPTENI JOHN KOMBA KIJIJINI KWAKE LITUHI


 Vijana Ndugu Sixtus Mapunda  pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania kwenda kumzika marehemu Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.

 

 



 Mke wa Marehemu Kapteni John Komba ,Salome (kushoto) akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu.



 Watoto wa marehemu Kapteni John Komba wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba yao.


 





 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyezikwa kwenye makaburi ya kijiji cha Lituhi.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba.













Marehemu Kapt. John Komba kuzikwa leo kijijini kwao Lituhi,Nyasa,Ruvuma


Mwili wa aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi na mjumbe wa NEC,Marehemu Kapt.John Komba unatarajiwa kuzikwa leo kijijini kwao Lituhi,Nyasa mkoani Ruvuma





 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza maelfu ya Watanzania kuuaga mwili wa Kapteni John Komba, katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.










 


 

 







Komba azikwa kwa tingatinga

Ndugu na jamaa wakisaidiwa na kijiko cha tingatinga kushusha mfuniko wa zege kwenye kaburi la Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba aliyezikwa  katika Kijiji cha LItuhi, wilayani Nyasa, Ruvuma jana. Picha na Emmanuel Herman 




Nyasa. Safari ya mwisho ya mbunge wa Mbinga Magharibi jana ilihitimishwa saa 9.25 alasiri wakati mwili wake ulipofunikwa na mfuniko mkubwa wa zege uliobebwa na gari maarufu kwa jina la “kijiko”.
Haikuwa kitu cha kawaida wakati gari hilo kubwa likishusha mfuniko huo wa zege kwenye kaburi la mwimbaji huyo maarufu wa nyimbo za uhamasishaji za CCM na kiongozi wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT), lakini majonzi yaliwafanya waombolezaji kulichukulia tukio hilo kuwa la kawaida.
Safari ya Komba, iliyoanza miaka 61 iliyopita kwenye kijiji cha Lituhi ambako aliazikwa jana, ilikamilishwa kwa salamu mbalimbali ambazo zilielezea ushupavu wa kapteni huyo mstaafu wa jeshi.
Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi, wakiwamo viongozi mbalimbaliwakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete na mkewe Salma, yalifanyika katika makaburi ya Misheni,katika Kijiji cha Lituhi (Bundi) wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Nyuso za majonzi zilitawala kwa waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa marehemu, takriban mita 500 kutoka katika makaburi hayo na baadaye katika misa iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Lituhi, ikiongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki la Mbinga.
Kaimu katibu wa Bunge, John Joel, akisoma wasifu wa marehemu, alisema Kapteni Komba aliyefariki dunia Februari 28, mwaka huu akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na mara kadhaa Ofisi ya Bunge ilimpeleka India kwa matibabu. Pia alikuwa na tatizo la kisukari ambalo ndilo lililochukua maisha yake.
Mazishi hayo yalishuhudiwa na viongozi mbalimbali, akiwamo Edward Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Utaratibu na Bunge), Jenister Mhagama na mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi.
Wengine ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ali Abdallah Ali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Uwanja wa ndege
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, viongozi mbalimbali waliwasili kwa ndege za kukodi na Lowassa ndiye aliyefungua mlango kwa ndege iliyotua saa 2:33 asubuhi akiambatana na mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani.
Haikupita muda mrefu, ndege nyingine ilitua saa 2:50 ikiwa na Spika Makinda na msafara wake uliomjumuisha mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe.
Saa 3:22 ilitua ndege iliyobeba ujumbe wa CCM ukiongozwa na Kinana. Wengine waliokuwamo ni naibu katibu mkuu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, katibu wa itikadi na uenezi, Nape Nnauye na mwimbaji wa kikundi cha TOT, Khadija Kopa. Pia baadaye Rais Kikwete alitua na ndege ya Serikali.



Mwili wa marehemu uliwasili ukiwa katika moja ya ndege mbili zilizobeba familia yake, ndugu na watu mbalimbali wa karibu.
Fulana za Lowassa
Wakati ibada ya misa ikiendelea, walionekana vijana wakiwa wamevaa fulana nyeupe na nyeusi zenye ujumbe wa “Marafiki wa Lowassa”,  zilizokuwa zimeandikwa mbele “4 U Movement  Lowassa”  huku mgongoni zikiandikwa “Kapteni John Damiano Komba 1954-2015 Friends of Lowasa”.
Baada ya vijana hao kuonekana,  mmoja wa viongozi wa Bunge alimwamuru mmoja wao aliyekuwa anapiga picha kwenda kuivua, lakini aligoma na hakuna kati yao aliyekubali kuivua hadi mazishi yalipomalizika. Mmoja wa vijana hao ambaye aligoma kutaja jina lake aliiambia Mwnanchi akisema: “Kwa sasa fulana zimeisha kwa kuwa zilizokuwa zinagawiwa. Lakini kama unazitaka unaweza kuacha namba yako na utaletewa sehemu yoyote utakapokuwa.
“Tumeamua kutoa fulani hizi kama zawadi ya kumbukumbu kwa mchango alioutoa Komba wakati wa urafiki wao (na Lowassa) na ndiyo maana unaona tumezivaa.”
Salamu za rambirambi
Katika salamu zake, Gasper Tumaini, katibu wa kikundi cha Sanaa cha TOT kilichokuwa kikiongoza Kapteni Komba, alisema Komba alipenda jimbo lake na chama chake na kuwa siku moja kabla kifo walikwenda kurekodi nyimbo za uchaguzi. Kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, mbunge wa Lindi Mjini (CUF), Salum Barwany alisema: “Tunatoa pole kwa wananchi na familia kwa kuondokewa na mbunge mahiri na shupavu, tumefika kuonyesha namna Komba alivyoishi vizuri nasi.
“Kila mmoja amejifunza namna Komba alivyoishi na watu vizuri , alikuwa akinipa faraja wakati matukio ya mauaji ya albino yalipotokea na wakati wote alikuwa akinihakikishia usalama wangu, hivyo tumepata  pigo kubwa kwa kuondoka kwake.”
Katibu Mkuu CCM, Abdulahman Kinana, alisema: “Tuna huzuni kubwa kutokana na msiba mkubwa uliotokea. Komba alifanya kazi nzuri ya kuwahudumia na kuwajali na kuangalia maslahi ya wananchi aliowaongoza. Alhamisi iliyopita alikuja ofisini kwangu na kuniambia anakwenda kiwandani kutafuta mabati 900 kupeleka jimboni kwake.”
Waziri Mhagama kwa niaba ya Serikali alisema: “Komba alikuwa kiungo muhimu kwa serikali. Wengi wamemzoea katika masuala ya siasa na chama, wote wanamkumbuka kwa tukio la kuimba nyimbo za maombolezi wakati wa msiba wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.”
Spika Makinda alitumia fursa hiyo kuzungumzia muswada wa mabadiliko katika sheria za Kiislamu ya mwaka 1963 kuhusu Mahakama ya Kadhi akisema inatakiwa kubadilishwa kushughulikia mirathi, talaka hivyo Wakristo wawe wavumilivu, wasikubali kuzungumzia vitu ambavyo hawana uhakika navyo.
source Mwananchi






Tuesday, March 3, 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MAELFU KUMUAGA MAREHEMU CAPT JOHN KOMBA HII LEO

 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma  wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Lituhi wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.




 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa marehemu Salome Komba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo






























Popular Posts