Wednesday, June 3, 2015

WATUMISHI WATAKIWA KUHAMIA WANGING'OMBE



Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi amewataka  watumishi walioamishiwa  na walioajiliwa katika halmashuri ya Wiaya ya Wanging’ombe   kuakikisha wamehamia kimakazi  katika wilaya hiyo.
Dk.Rehema Nchimbi,amesema kuwa wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe  watakiwa kupata huduma kutoka kwa watumishi hao na anashangaa kuona watumishi wanaishi Njombe mjini na kufanyakazi katika halmashuri ya wilaya ya Wanging’ombe ambayo ipo zaidi ya umbali wa kilometa 40 kutoka Njombe Mjini.
Nchimbi ametoa wiki mmoja toka leo kuakikisha watumishi hao wawe wameamia na kuishi katika Wilaya hiyo ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuwa karibu na wananchi ,aliyasema hayo kwenye ukumbi wa halmashuri ya wilaya ya Wang’ingombe wakati akifanya mkutano wa watumishi wa halmshauri hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Fedrick Mwakalebela  alisema kuwa wilaya hiyo inamahitaji yote  muhimu kama vile ofisi,miundombinu ya maji na barabara  na kuwasihii watumishi hao wakikishe wanahami katika wilaya hiyo haraka iwezekanazo kwani maendeleo ya wanging’ombe yataletwa na wananchi wa wanging’ombe kwa kushilikiana na watumishi.
Mkurungenzi wa Wilaya hiyo Melizedeki Humbe  alisema kuwa watumishi wengi katika wilaya hiyo bado wanaishi Njombe mjini lakini wamewaka mikakati ambayo ndani ya wiki mmoja waliopewa kuakikisha watumishi hao wote wanaamia katika wilaya hiyo mpya iliyo anzishwa mwaka 2012.



















Tuesday, June 2, 2015

NJOMBE KUTATUA SHIDA YA MAJI



Mamlaka ya Maji Mkoa wa Njombe(NJUWASA)  imepokea kiasi cha fedha 2.6 ( 2,577,138,890.00)  bilioni  kutoka Wizara ya Maji  toka mwaka 2013 kwa ajili ya kuboresha hudumaya maji katika Mji wa Njombe.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Njombe Mhandisi, Daudi Majani amesema kuwa mpaka sasa fedha hizo zimetumika kujenga chanzo cha maji  cha Nyenga,matanti matatu ya maji na utandazaji wa mabomba ya maji ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi wa saba mwaka huu.
Alisema kuwa mpaka sasa Ujenzi wa kidakio cha maji umekamilika  na ujenzi wa matanki matatu yaliyopo katika maeneo ya Airport,Kambalage ,Igeleke na Nzengelendete  na kila tank linauwezo wa ujazo wa lita 135,000 kila mojaHatua inayoendelea sasa ni utandazaji wa mabomba ya maji katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Njombe .
Mradi huo ukikamilika utawezesha kufanya mji wa Njombe kuongeza upatikanaji wa maji kutoka  asilimia 55 hadi 80  na kufanya mji huo kuondoka na huwaba wa maji .
Majani amesema hayo jana kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi alipotembelea vyanzo vya maji na kuangalia mtandao wa maji katika mji wa Njombe.
Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka Halmashuri za mji wa Njombe kushirikiana na mamlaka ya maji Mkoa wa Njombe kuakikisha wanatoa elimu kwa wananchi waliopo kwenye vyanzo vya maji ili kutunza vyanzo vya hivyo.























Monday, May 18, 2015

NDC YAFANYA UTHAMINISHAJI WA MALI ZA WANANCHI WA MCHUCHUMA NA LIGANGA ILI KULIPA FIDIA






Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi  wa pili kutoka kushoto akiwa amebeba Mkaa wa Mawe unaopatika katika machimbo ya Mchuchuma katika Wilaya ya Ludewa,wa kwanza kushoto ni Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo filikunjombe,wa tatu kutoka kushoto Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe  Fedrick Mwakalebela na Mkuu wa wilaya ya Njombe Bibi Salah Dumba




Mbunge wa  Ludewa Deo Filikunjombe  akiongea na Mkuu wa  Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi wakiwa wanatoka kukagua Makaa ya Mawe kwenya Mgodi wa Mchuchuma.






Shirika la Taifa La Maendeleo ( NDC) limezindua zoezi la Uthaminishaji wa Mali za Wananchi walio ndani ya Maeneo ya Mradi wa chuma cha Liganga katika      Wilaya ya Ludewa.
Kaimu Mkurugenzi wa ( NDC) Mlingi Mkocha amesema kuwa zoezi hilo la Uthamini wa Mali za wananchi litachukuwa miezi miwili mpaka kukamilika kwake ili kuendelea kuendelea kwa hatua za malipo kwa watu ambao wataamishwa maeneo yao kupisha uchimbwaji wa madini hayo.
Mkocha alisema kuwa  inakisiwa kuna tani milioni 126 za madini ya chuma zilizohakikiwa zinaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 40 kwa kiwango cha tani milioni 2.9 kwa mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo aliwataka  watalaam watakaofanya uthamini wa mali za wananchi kuwa waaminifu na makini ili kutenda haki kwa kila mwananchi anayefanyiwa uthamini wa mali zake bila kuomba wala kupokea rushwa
Nchimbi alisema kuwa kazi hiyo ni muhimu na itaepusha migogoro  kama itatendwa kwa haki,vilevile aliwataka NDC na wawekezaji kutoa ajira kwa wananchi wa Ludewa na Njombe kwani wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi.

Mbunge  wa Jimbo hilo Deo Filikunjombe akiwahutubia wanachi wa kijiji cha Mkomang’ombe aliwataka washirikiane na wawekezaji katika kazi mbalimbali katika wilaya hiyo kwani itasaidia kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.

Mradi huo wa Chuma wa Liganga unatekelezwa  na Serikali ya Tanzania na China ,gharama za uwekezaji katika mradi huu zinakadiriwa kuwa na Dola za Marekani bilioni 1.8





















Popular Posts