Monday, June 8, 2015
CCM waanza kupitia mafaili ya wagombea urais
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
KAMATI Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Philip Mangula, imeanza vikao vyake mjini Dodoma kupitia taarifa za utekelezaji wa adhabu kwa makada sita wa chama hicho wanaodaiwa kuanza kampeni kuwania urais mwaka 2015 kabla ya wakati.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya CCM kiliiambia MTANZANIA kuwa kikao hicho kilianza jana saa 6 mchana, kuanza kupata taarifa za kamati za maadili za mikoa.
Hatua hiyo inatokana na agizo la Mangula ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, alilolitoa Februari 8, mwaka huu kwa kuzitaka ofisi zote za ngazi ya mikoa na wilaya kufungua mafaili hayo ili kupitia mienendo ya wagombea walioanza kampeni za uchaguzi wa kuteuliwa kugombea urais kabla ya wakati.
Makada hao waliozuiwa kujihusisha na kampeni kwa miezi 12, huku mienendo yao ya kisiasa ikifuatiliwa ni January Makamba, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
“Leo (jana) tangu saa 6 mchana Kamati Ndogo ya Maadili ilikuwa na vikao mfululizo, na kazi kubwa walikuwa wanapitia mafaili ya wagombea waliotangaza nia ya kuwania urais mwaka 2015.
“Walichokuwa wanakifanya ni taarifa ya utekelezaji wa adhabu hiyo kwa kila mgombea pamoja na kufuatilia mienendo yao… ila kinachoonekana kuna baadhi ya makada huenda adhabu zao zikaongezwa na hata kupoteza sifa za kuwania nafasi hiyo.
“Unajua tangu walipopewa adhabu, baadhi yao wamekuwa wakikiuka na hata kuendelea na mikakati ya kampeni kwa kukusanya watu wao kupanga nini cha kufanya kuelekea mwaka 2015, pia wengine walitumia Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani kuandaa futari ambazo zilikuwa na harufu ya kampeni,” kilisema chanzo hicho kilichopo Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, zinaeleza kuwa katika kipindi cha miezi kadhaa, timu za maofisa usalama wa chama zilisambazwa mikoa yote na kukusanya taarifa za makada hao.
Kikao hicho kimefanyika kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC), kilichoitishwa kwa dharura mjini hapa leo chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.
Hatua hiyo ya kuitishwa kikao hicho imekuja baada ya kuwapo kile kinachodaiwa ni shinikizo kutoka kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kumtaka Rais Kikwete aliahirishe Bunge la Katiba linaloendelea na vikao vyake mjini hapa.
Hatua ya Rais Kikwete kuitisha CC inatokana na uamuzi wa kamati hiyo, iliyoketi Julai 16, mwaka huu ambapo ilipokea taarifa za harakati za baadhi ya wanachama wa CCM walioonyesha nia ya kuomba ridhaa ya chama kugombea urais.
Kutokana na hali hiyo, CC iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada hao sita kama wanatekeleza ama la.
Hatua hiyo ya CCM kupitia mienendo ya makada hao waliopewa onyo Februari mwaka huu inawafanya kukalia kuti kavu, kwani ikiwa watabainika kuvunja utaratibu wa chama wanaweza kupoteza sifa za kuwania urais mwakani.
Julai 17, mwaka huu Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema endapo Kamati ya Usalama na Maadili itabaini kama makada hao walikiuka mwenendo wa utekelezaji wa adhabu waliyopewa, watapoteza sifa.
Kabla ya adhabu hiyo, makada hao waliitwa na kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ambayo iliwatia hatiani kwa kutumia Kitabu cha Kanuni ya Uongozi na Maadili ya CCM, toleo la Februari 2010, Ibara ya 6 (7)(i).
Nape alisema Kamati Kuu ilipokea taarifa za harakati za baadhi ya wanachama wa CCM walioonyesha nia ya kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais.
“Baada ya kutafakari kwa kina, Kamati Kuu inapenda kuwakumbusha kuwa ili wasipoteze nia ya kugombea, ni muhimu wakazingatia Katiba, kanuni na taratibu za chama zinazosimamia masuala hayo,” alisema Nape.
Alisema kama itabainika makada hao hawakutekeleza masharti ya adhabu zao kama zilivyotolewa na CC, kuna hatari ya kuongezewa adhabu kulingana na ukubwa wa uvunjaji wa masharti ya adhabu husika.
“Kila mmoja anafuatiliwa mwenendo wake, kuhusu wale waliopewa adhabu na Kamati Kuu kutokana na kukiuka baadhi ya taratibu za chama kwa suala hili, Kamati ya Usalama na Maadili ya chama itafanya mapitio ya mwenendo wao wa utekelezaji wa adhabu hiyo.
“Kama watakuwa hawajatekeleza adhabu zao, kamati itapeleka mapendekezo CC ili waweze kuongezewa adhabu kulingana na ukubwa wa makosa yao na taratibu za chama,” alisema Nape.
Alisema ni muhimu kwa wanachama wote kukumbuka chama ni pamoja na Katiba, kanuni na taratibu zake, hivyo kutoziheshimu na kuzifuata ni kukivuruga jambo ambalo halivumiliki.
Kwamba nia ya CCM ni kusimamia na kuhakikisha chama kinakuwa na umoja na mshikamano ambao ni muhimu sana, hasa katika kuelekea kukamilisha kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010/2015 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Habari ambazo gazeti hili limezipata kutoka ndani ya Kamati Kuu, zinasema aliyetoa hoja kuendelea kufuatiliwa kwa makada hao ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Mangula aliyesema amefungua faili kwa ajili ya makada hao.
Alisema suala jingine alilowasilisha Mangula ni ripoti ya ziara yake aliyoifanya katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Tanga.
Februari 18, mwaka huu CCM kupitia Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu katika kikao chake ilipendekeza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa makada wake ambao wameanza kampeni ya kuwania urais wa mwaka 2015.
Uamuzi huo ulibarikiwa na Kamati Kuu iliyokutana Februari 17, mwaka huu mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Rais Kikwete. source www.tanzaniatoday.co.tz/
Msafara wa Makongoro Nyerere wapata Ajali Mbaya Mkoani Kigoma
Msafara wa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Charles Makongoro Nyerere umepata ajali wilayani Kasulu mkoani
kigoma mapema leo hii.
Msafara huo uliokuwa ukielekea wilayani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini, ambapo gari walilokuwa wamepanda wasaidizi wa Makongoro ndilo lililopata ajali kwa kupinduka wakati likiwa kwenye mwendo.
Watu waliokuwepo katika gari hilo lililopata ajali wameumia vibaya sana akiwemo Mwandishi wa habari, Cyprian Musiba na kukimbizwa katika hospital ya wilaya ya kasulu (mlimani) kwaajili ya matibabu.
tutaendelea kuwajuza zaidi juu tukio hilo
Gari lililopata ajali katika msafara wa
Msafara huo uliokuwa ukielekea wilayani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini, ambapo gari walilokuwa wamepanda wasaidizi wa Makongoro ndilo lililopata ajali kwa kupinduka wakati likiwa kwenye mwendo.
Watu waliokuwepo katika gari hilo lililopata ajali wameumia vibaya sana akiwemo Mwandishi wa habari, Cyprian Musiba na kukimbizwa katika hospital ya wilaya ya kasulu (mlimani) kwaajili ya matibabu.
tutaendelea kuwajuza zaidi juu tukio hilo
Gari lililopata ajali katika msafara wa Mwenyekiti CCM atamba kumng’oa Mchungaji Msigwa

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca
Msambatavangu (39) amesema anayo nia na uwezo wa kumuangusha katika
Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu, Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini
anayemaliza muda wake Mchungaji Peter Msigwa (Chadema).
Msambatavangu aliyasema hayo jana ikiwa ni wiki moja tangu Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Phillip Mangula afike mjini Iringa
kumaliza mgogoro wa kisiasa uliosababisha baadhi ya wanachama wa chama
hicho jimbo la Iringa Mjini wafukuzwe uanachama huku Mwenyekiti huyo wa
Mkoa akipewa onyo kali.
Machi mwaka huu, vikao vya chama hicho ngazi ya wilaya na mkoa
viliwafukuza uanachama Shukuru Luhambati, Clara Shirima na Hosea
Kaberege huku Msambatavangu akipewa onyo kali lililodaiwa kumuondolea
sifa ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi kupitia chama hicho na kuzusha
hofu kubwa ya mpasuko ndani yake.
Akizungumzia rufaa walizokata na maamuzi aliyokuja nayo Mangula na
kuyawasilisha katika kikao cha Halmashauri ya Wilaya ya CCM Manispaa ya
Iringa, Msambatavangu alisema; “CCM kwa kutumia kanuni na Katiba yake
imepitia rufaa zetu, ikajifunza kitu na kutumia busara yake kutupilia
mbali adhabu hizo ili kulinda maslahi mapana ya chama hiki.
“Tunajiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao tukiwa wamoja na
niwahakikishieni mimi ni mmoja kati ya wana CCM wenye nia ya kugombea
ubunge katika jimbo la Iringa Mjini.
“Sijajua makada gani wengine
watajitokeza; wenye uwezo wa kusema ni nani ni CCM wenyewe na wananchi
wa jimbo hili.
"Kwa mimi kutangaza nia na kujitoa nina hakika na ninafahamu nina
uwezo wa kupeperusha bendera na kurudi na ushindi, sitakiletea aibu
Chama Cha Mapinduzi pamoja na kwamba nipo tayari kumuunga mkono mgombea
atakayeteuliwa,” alisema.
Alitaja kipaumbele chake cha kwanza endapo CCM itampa ridhaa ya
kuwania nafasi hiyo kuwa ni elimu na katika sekta hiyo atahakikisha
miundombinu yake inaboreshwa ili iwe ya kisasa.
“Nitahakikisha kunakuwepo na ustawi wa elimu, shule bora zenye nidhamu ili Iringa iingie kwenye ushindani wa juu kitaifa.
"Tutajiimarisha kujenga mabweni katika shule zetu ili watoto hasa wa
kike wawe jirani na shule,” alisema.
Thursday, June 4, 2015
WACHINA ELFU 6,000 KUINGIA NJOMBE
Zaidi ya
wachina elfu sita (6,000) wanatarajiwa kuingia katika Mkoa wa Njombe kwenye
sekta ya madini hasa makaa ya mawe na
Chuma kwenye eneo la Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa.
Hayo yamesemwa jana
kwenye Ukumbi wa Lutheran Makambako na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi
alipokuanaongea na watumishi wa Halmashuri ya Mji Makambako,alisema kuwa Mradi
wa Linganga na Mchuchuma unatarajiwa
kuanza kuchimbwa makaa ya m awe na chuma hivi karibuni utatoa ajira zaidi ya
Elfu thelathini (30,000) zikiwepo za
wazawa na wageni.
Kutokana na hilo
amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji Makambako hasa sekta ya Ardhi
kuakikisha wanaweka mipango mizuri ya matumizi ya ardhi na kupima viwanja ili
kuwavutia wawekezaji mbalimbali katika ujenzi wa Hoteli za kisasa na halmashuri
kuakikisha wanaboresha miundombinu ya Maji na barabara .
Dk .Nchimbi alisema kuwa mpaka sasa shirika la maendeleo ya
Taifa (NDC) limeanza mchakato wa uthamini
wa mali za wananchi ili waweze kulipwa fidia kupisha mradi huo.
Aliwataka wananchi wa
Makambako na Njombe kwa Ujumla kujiandaa na ujio wa wageni mbalimbali
kwa kufuga kuku ,Ng’ombe pamoja na mifugo mingine ili kuweza kuwauzia wageni hao na kuongeza kipato
cha familiya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako Hanana Chesco Mfikwa alisema kuwa wanajiandaa kwa kuwapokea wageni hao kwa
kuakikisha wanaweka mipango mizuri ambayo itasaidia wageni kuwekeza zaidi
katika eneo la Makambako.
Wednesday, June 3, 2015
WATUMISHI WATAKIWA KUHAMIA WANGING'OMBE
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema
Nchimbi amewataka watumishi
walioamishiwa na walioajiliwa katika
halmashuri ya Wiaya ya Wanging’ombe kuakikisha wamehamia kimakazi katika wilaya hiyo.
Dk.Rehema Nchimbi,amesema
kuwa wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe
watakiwa kupata huduma kutoka kwa watumishi hao na anashangaa kuona
watumishi wanaishi Njombe mjini na kufanyakazi katika halmashuri ya wilaya ya
Wanging’ombe ambayo ipo zaidi ya umbali wa kilometa 40 kutoka Njombe Mjini.
Nchimbi ametoa wiki
mmoja toka leo kuakikisha watumishi hao wawe wameamia na kuishi katika Wilaya
hiyo ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuwa karibu na wananchi ,aliyasema hayo
kwenye ukumbi wa halmashuri ya wilaya ya Wang’ingombe wakati akifanya mkutano
wa watumishi wa halmshauri hiyo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya
Wanging’ombe Fedrick Mwakalebela alisema
kuwa wilaya hiyo inamahitaji yote muhimu
kama vile ofisi,miundombinu ya maji na barabara na kuwasihii watumishi hao wakikishe wanahami
katika wilaya hiyo haraka iwezekanazo kwani maendeleo ya wanging’ombe yataletwa
na wananchi wa wanging’ombe kwa kushilikiana na watumishi.
Mkurungenzi wa Wilaya
hiyo Melizedeki Humbe alisema kuwa
watumishi wengi katika wilaya hiyo bado wanaishi Njombe mjini lakini wamewaka
mikakati ambayo ndani ya wiki mmoja waliopewa kuakikisha watumishi hao wote
wanaamia katika wilaya hiyo mpya iliyo anzishwa mwaka 2012.
Tuesday, June 2, 2015
NJOMBE KUTATUA SHIDA YA MAJI
Mamlaka ya Maji Mkoa
wa Njombe(NJUWASA) imepokea kiasi cha
fedha 2.6 ( 2,577,138,890.00) bilioni kutoka Wizara ya Maji toka mwaka 2013 kwa ajili ya kuboresha
hudumaya maji katika Mji wa Njombe.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Njombe Mhandisi, Daudi
Majani amesema kuwa mpaka sasa fedha hizo zimetumika kujenga chanzo cha
maji cha Nyenga,matanti matatu ya maji
na utandazaji wa mabomba ya maji ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika
mwisho wa mwezi wa saba mwaka huu.
Alisema kuwa mpaka sasa Ujenzi wa kidakio cha maji
umekamilika na ujenzi wa matanki matatu
yaliyopo katika maeneo ya Airport,Kambalage ,Igeleke na Nzengelendete na kila tank linauwezo wa ujazo wa lita
135,000 kila mojaHatua inayoendelea sasa ni utandazaji wa mabomba ya maji
katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Njombe .
Mradi huo ukikamilika utawezesha kufanya mji wa Njombe
kuongeza upatikanaji wa maji kutoka
asilimia 55 hadi 80 na kufanya
mji huo kuondoka na huwaba wa maji .
Majani amesema hayo jana kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa
Njombe Dk.Rehema Nchimbi alipotembelea vyanzo vya maji na kuangalia mtandao wa
maji katika mji wa Njombe.
Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka Halmashuri za mji wa Njombe
kushirikiana na mamlaka ya maji Mkoa wa Njombe kuakikisha wanatoa elimu kwa
wananchi waliopo kwenye vyanzo vya maji ili kutunza vyanzo vya hivyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Popular Posts
-
Umati wa watu wakisubiri kutambua maiti za watu waliofariki katika ajali ya basi la Majinja Express katika chumba cha kuhifadhia maiti ...
-
UZEMBE wa dereva wa basi Mitsubishi Fuso, mali ya kampuni ya Another G Trans lenye usajili Namba T.927 CEF, Nicolaus Magula (30) umes...
-
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain (mst) Aseri Msangi amemwagiza Mkurugenzi wa halmashuri ya wilaya ya Njombe kuakikisha barabara kutoka Ikond...
-
Askari wawili wa Jeshi la Polisi katika Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani, wameuawa baada ya kushambuliwa kwa silaha na m...