Tuesday, June 23, 2015

Serikali yakana kumtorosha Rais wa Sudani






 Serikali ya Afrika Kusini imekana ripoti kwamba mawaziri wake walipanga njama ya kumtorosha rais wa Sudan Omar El Bashir wiki iliopita.
 
Katika tukio hilo nusura rais huyo akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
 
Mahakama ya Afrika Kusini ilimuagiza Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo litekelezwe. Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake bwana Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurudi nyumbani.
 
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika kumkamata kwa kuwa mwanachama wa ICC.
 
Kwa mujibu wa  gazeti la Sunday Times nchini Afrika Kusini limenukuu duru za serikali kwamba katika mkutano wa mawaziri ilikubalika kwamba Afrika Kusini itamlinda hata iwapo italazimika kukiuka uamuzi wa mahakama na kukiuka katiba.
 
Katika taarifa yake,serikali imekana kwamba kulikuwa na mkutano wa siri na kwamba itaipatia mahakama hiyo maelezo kuhusu vile Bashir alivyoondoka nchini humo.
 
Mahakama kuu imeipatia serikali ya taifa hilo hadi alhamisi kubaini ni vipi aliruhusiwa kuondoka.

Ngassa arejea Yanga kiaina








Mshambuliaji wa Free Stars ya Afrika Kusini,Mrisho Ngassa (kulia) akifanya mazoezi na timu yake ya zamani Yanga baada ya kurejea nyumbani kwa mapumziko kwenye uwanja wa karume Dar es Salaam Jana.Picha na Said Khamis. 



Dar er Salaam. Mshambuliaji Mrisho Ngassa aliyesajiliwa na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini hivi karibuni, jana aliibuka katika mazoezi ya timu yake ya zamani Yanga.
Ngassa alisajiliwa na Free State Stars kwa mkataba wa miaka minne mwishoni mwa mwezi uliopita na alirudi nchini kwa ajili ya kuitumikia Taifa Starsiliyokuwa ikicheza dhidi ya Uganda katika mechi ya kuwania kufuzu kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN), ingawa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilimzuia kwani ameishasajiliwa nje ya ligi ya Tanzania.
Gazeti hili lilimshuhudia mshambuliaji huyo akifanya mazoezi na Yanga mwanzo mwisho na alipomaliza mashabiki wa klabu hiyo walilisukuma gari lake mpaka nje geti wakionyesha mapenzi kwa mchezaji huyo.
Ngassa ameitumikia Yanga kwa mafanikio kabla ya kuamua kuachana nayo na kwenda kusaka ulaji katika klabu ya Free State.
Ngassa alisema ameamua kufanya mazoezi na Yanga kwani bado iko moyoni mwake na hakuondoka kwa ubaya.
“Hapa kama niko nyumbani, kwani hii ni timu iliyo moyoni mwangu hivyo kama niko Dar es Salaam sioni ubaya kufanya mazoezi na Yanga kwani naamini kuna siku nitarudi hapa,”alisema Ngassa.
“Najiweka fiti wakati nikisubiri klabu yangu initumie tiketi ya kurudi Afrika Kusini maana walinipa ruhusa ya kuja Dar es Salaam kwa ajili ya timu ya Taifa, lakini nikazuiwa kucheza mechi na Uganda,” alisema Ngassa.
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Ngassa kwani aliifungia Yanga mabao manne tu licha ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Aprili

















Urais 2015: Mwanamke wa 5 ajitosa kuchukua fomu CCM



















 Mwananmke mwingine  ambaye ni kada wa CCM, Ritta Ngowi amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
 
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu jana makao makuu ya CCM mkoani Dodoma Ngowi alisema akifanikiwa kuwa rais  ataanzisha kituo kikubwa cha kuwahudumia wastaafu, walemavu, wasiojiweza na vijana.
 
Kingine atakachofanya ni kuendeleza mazuri yaliyofanywa na marais waliopita, lakini zaidi akiweka mkazo kwenye masuala ya elimu na kukuza uchumi.
 
Aidha Ritha anafanya ,  idadi ya wanawake waliojitosa mbio za urais kufikia watano kati ya 39 waliochukua fomu hadi sasa.
 
Wanawake wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa (NIMR), Dk Mwele Malecela, Balozi Amina Salum Alli na Monica Mbega.

Kocha wa Taifa Stars Maart Nooij na Benchi Lake Lote La Ufundi Watimuliwa Kazi




 Kocha Mkuu wa Taifa Stars Maart Nooij akisindikizwa na ulinzi mkali usiku wa kuamkia leo baada ya kumalizika kwa mchezo wa Tanzania na Uganda wa kuwania kufuzu fainali za CHAN katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa 3-0. *******
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.
 
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
 
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
 
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Juni 20, 2015















Monday, June 22, 2015

Lowassa Azidi Kupata Mapokezi Makubwa

WAZIRI Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina lake katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.

Lowassa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.

"Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu". alisema Lowassa.

Lowassa aliwasili Mkoani Ruvuma mapema  jana mchana akitokea Mkoani Iringa kwaajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea kufunga barabara kuu ya mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya paa la  jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza nao.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Wednesday, June 17, 2015

PINDA APATA WADHAMINI NJOMBE




Mgombea wa Urais kupitia chama cha mapinduzi na waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda amewataka wananchama wa chama  cha mapinduzi Mkoa wa Njombe kuendelea kujitokeza kwa wingi na kuendelea kuwadhamini wagombea mbalimbali  waliochukua fomu na watakaochukua fomu  za kugombea nafasi ya  Urais bila kubagua Mgombea yoyote.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe ambapo mamia ya wananchama wa chama hicho  walijitokeza kumdhamini ili aweze kugombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi
Alisema kuwa waliojitokeza kuchukua fomu kupitia chama cha mapinduzi ni wengi lakini atakayepitishwa kupitia chama hicho ni mgombea mmoja ambaye atawakilisha chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi unatakofanyika mwezi wa kumi na mgombea huyo ndie atanadiwa na chama hicho akishindanishwa na vyama vingine  kwenye uchaguzi Mkuu.
Wanachama waliojitokeza kumdhamini Mgombea huyo wamesema kuwa wanaimani kubwa na mgombea huyo na kuamini kuwa chama kitampitisha kuwakilisha chama hicho kwenye kugombea Urais.
Kwa Mkoa wa Njombe tayari wagombea January Makamba,Bernard Membe,Stive Wassira,Samweli Sitta,Makongoro Nyerere ,Monica Mbega ,Amosi Siyatemi na Prof.Mark Mwandosya.










Tuesday, June 16, 2015

AJALI YA ANOTHER G MAFINGA ,WATU 25 WAFARIKI


 Image result for ajali ya another G mafinga

UZEMBE wa dereva wa basi Mitsubishi Fuso, mali ya kampuni ya Another G Trans lenye usajili Namba T.927 CEF, Nicolaus Magula (30) umesababisha abiria 23 wapoteze maisha na wengine 34 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea juzi Jumapili mjini Mafinga.
Ajali hiyo ilitokea Majira ya saa 1.45 usiku katika eneo la Kinyanambo A, barabara Kuu ya Iringa Mbeya baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na  na roli aina ya Scania lenye namba za usajili T.916 AQM likiwa na tela namba T 965 BEH, mali ya kampuni ya Bravo Logistics (T) Ltd ya Dar es Salaam.
Wakati ajali hiyo ikitokea, wakazi wa Mafinga na Tanzania kwa ujumla bado wanakumbuka ajali nyingine iliyotokea katika eneo la Changarawe, mjini Mafinga miezi mitatu iliyopita (Machi 11, mwaka huu) ikuhusisha roli Scania namba T 689 APJ mali ya Cipex Company na basi Scania namba T 438 CED  na kusababisha vifo vya watu 50.
Akizungumza na wanahabari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Pudenciana Protas alisema; “wakati basi hilo lenye uwezo wa kupakia abiraia 65 lilikuwa likitokea Iriinga kuelekea Njombe, roli hilo lililokuwa likiendeshwa na Rogers Wales mwenye miaka 39, Msambaa mkazi wa Mwanza lilikuwa likitokea barabara kuu ya Mafinga kuelekea Iringa.”
Protas alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo aliyekosa umakini na kutaka kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari.
Alisema miili ya marehemu na majeruhi hao ilikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi ya mjini Mafinga, mapema baada ya ajali hiyo kutokea.
Alisema miili 12 ya watu waliokufa imekwishatambuliwa na kuwataja kuwa ni pamoja na Lucas Pancras, Blasto Samila, Dickson Luvanda, Albert Silla (askari wa Ruvu JKT), Eva Mbalinga, Khadija Mkoi (4), Clemence Mtati, Mohamed Lalika, Castory Mwakiamba, Damiana Myala na Silo Nziku ambao wote walikuwa katika basi hilo na dereva wa roli hilo Rogers Wales.
Alitaja majeruhi wa ajali hiyo waliokuwa katika basi hilo kuwa ni pamoja na Emma Lupembe (35), Veronica Simba (20), Shafia Ally (24), Mariamu Mbise (23), Anita Makwela (24), Benita Sagara (18), Bertha Mkoi (27), Rahel Mavika (18),, Selina Fulgensi (23), Maria Mwenda (17), Ndipako Mbilinyi (28), Alexander Mkakazi (28), Meshack Kibiki (44), Simoni Jumbe (22), Jerry Lutego (36), Enock Kanyika (18) na Yusuph Lulandala (22).
Wengine ni Deogratias Kayombo (21), Petro Mwalongo (21), Paul Chahe (21), Kennedy Msemwa (28), Emanuel Anthony (21), Mode Shilazi (21), Godfrey Kanyika (39), Boniface Bosha (20), Ambiana Meshack (35), Martha Kanyika (30), Melika Tonga (2.5), Yusuph Luhumba (34) na Damiana Kuyala (42).
Protas alisema majeruhi wengine wanne, wanaume wawili na wanawake hawajatambuliwa majina yao kwasababu walikuwa hawaongei
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Popular Posts