Thursday, September 25, 2014

SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) LATOA ELIMU YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWA WATUMISHI WA UMMA.

Shirika la kazi duniani kushirikiana na Ofisi ya Rais Sekretalieti ya Utumishi wa Umma imezindua elimu ya kujinginga na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwa watumishi wa umma katika mkoa wa Njombe,uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashuri ya Njombe na ulizinduliwa na katibu Mkuu utumishi Bwan. Gorgeg Yambesi.
Katibu Mkuu aliwataka watumishi kujitokeza na kupima afya zao ili kujitambua mapema na serikali iweze kuwasidia,kwa kuwawezesha kwa kuwapa huduma bora ili waweze kufanya kazi kwa amani na ufanisi.
Yambes alisema kuwa uzinduzi  huwo wa kupima maambukizi ya UKIMWI kwa hiari kwa watumishi  umefanyika katika Mkoa wa Njombe kutoka na Mkoa huo kuwa na kuongoza kwa Maambukizi.

Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Njombe Bibi Salara Dumba alisema kuwa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya Ukimwi kwa asilimi 14.8 na kufutiwa na Iringa asilimia 9.1.
Dumba alisema Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi kutoka na Mila potofu kama vile kurithishana wajane,kutakasa wagane na wanaume kutofanya tohara.
Naye mwakislishi wa Shirika la kazi Duniani Bibi Getrudi Sime alisema shirika hilo limelidhia Mkataba wa mwaka 2010 kwa kutambua kuwa VVU na UKIMWI una athari kubwa kwa jamii na uchumi kwa ulimwengu wa kazi katika sekta  rasmi na zisizo rasmi.










Tuesday, September 9, 2014

TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA MAGEREZA KUHUSU TAARIFA ZA UZUSHI ZINAZOZAGAA KUWA BABU SEYA NA MAWAE WAMEACHIWA HURU

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).



Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014.

Monday, September 8, 2014

MBIO ZA MWENGE NYUMBANI KWA MWALIMU NYERERE WILAYA YA BUTIAMA






Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mara wakiwa nje ya lango la Nyumba ya Baba wa taifa hayati Mwl Julius Nyerere wakingojea Mwenge wa uhuru ukiwa umechukuliwa kwenda kuwasha Mwenge wa Mwingo hivi karibuni.  

 

 Kiongozi w mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2012 kapt Honest Ernest Mwanossa akitamka manane Sisi tumekwisha uwasha Mwenge na kuuweka mlima Kilimanjaro,baada ya kuwasha Mwenge uliopo Mwitongo Nyumbani kwa Baba wa taifa hayati Mwl Julius K Nyerere.






































 

HABARI YA KUSIKITISHA: AJALI YAUA ZAIDI YA 50 LEO MUSOMA NI MABASI YA MWANZA COACH NA JUMANNE, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA


 
Home » » NEWS ALERT HABARI YA KUSIKITISHA: AJALI YAUA ZAIDI YA 50 LEO MUSOMA NI MABASI YA MWANZA COACH NA JUMANNE, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA

NEWS ALERT HABARI YA KUSIKITISHA: AJALI YAUA ZAIDI YA 50 LEO MUSOMA NI MABASI YA MWANZA COACH NA JUMANNE, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA



 Mabasi hayo yakiwa yamegongana








 









Basi la Jumanne lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza coach lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Musoma. Ajali imetokea katika eneo la daraja la sabasaba, Musoma.  Endelea kufuatilia 
Maelezo kwa Mujibu wa Father Kidevu blog







Friday, September 5, 2014

MTU MMOJA AUAWA PAPO HAPO KWA KUCHOMWA NA KISU KISA WALIKUWA WANADAIANA TSH 5,000, KITUO CHA MABASI IRINGA

 Tunaomba Radhi kwa picha.
 Tukio tulilopokea muda mchache uliopita mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika amemuua mwenzake kisa walikuwa wanaiana Shilingi Elfu tano... Tunaendelea kufuatilia tukio zaidi .. endekea kufuatilia hapa hapa.
 
Kijana huyo ambaye jina halijafahamika akiwa amefariki baada ya Kuchomwa kisu na mwenzake kisa madai ya Tsh 5000 tuu
 
 
 
 
Mamia ya watu wakiwa wanashuhudia tukio hilo.
Picha na Iringa yetu Blog
 
 

BODA BODA NA ABIRIA WAKE WAGONGWA NA GARI BARABARA YA CHALINZE SEGERA












 Mwendesha pikipiki na abiria (majina hayakutambulika) wakiwa wamelala chini katika barabara ya Chalinze Segera karibu na Kabuku baada ya kugongwa na gari ndogo yenye usajili namba T818 BNS leo mchana. Mpiga picha wa tukio hili alienda kutoa taarifa ya ajali kiTuo cha polisi cha Kabuku ambapo Polisi walienda kutoa msaada wa kukimbiza majeruhi hospitali pamoja na kupima ajali. (Picha kwa hisani ya Rodney Thadeus)


PICHA ZA JK, MAMA SALMA NA MJUKUU WAO SHAMBANI KWAO MSOGA.





























 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mjukuu wao Aziza Ridhiwani (3) katika ghala ya mahindi yaliyovunwa kwenye shamba lao kijijini Msoga, nje kidogo ya mji mdogo wa Chalinze, Mkoa wa Pwani. Rais Kikwete ni mkulima na mfugaji kijijini hapo na ameonesha kufurahishwa sana na mavuno makubwa ya mahindi shambani kwake. Hii  katika kutekeleza kwa vitendo sera ya Serikali  ya kuendeleza kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya sekta ya kilimo katika Tanzania.


Picha na Ikulu                               





Cheki jinsi Polisi Walivyowatawanya wananchi walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake na Kuchoma Moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani. huku mwandishi wa habari mmoja akiripotiwa kujeruhiwa Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani



                                                         Askari
                                          wa kutuliza ghasia










                          Diwani Chehako akiwa nyumbani kwake








 mahakama ya Mwanzo






Mwandishi wa Channel Ten, John Kasembe


 


 
 

 wa kutuliza ghasia wakijiandaa kuzuia vurugu zilizotokea Mtwara, jana kwa kile kilinachodaiwa ni mwendelezo wa vurugu za madai ya gesi.
---
POLISI jana wamelazimika
kupiga mabomu ya machozi kutwa nzima katika kata ya Chikongola, Manispaa
ya Mtwara Mikindani kutawanya wananchi walioizingira nyumba ya diwani
wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya
nyumba yake, huku mwandishi wa habari mmoja akiripotiwa kujeruhiwa.



Habari
ambazo hazijathibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa, Maria Nzuki
zinadai kuwa majira ya saa 10 kasoro za jioni watu wanaodaiwa kuwa ni
wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliingilia kati na
kuanza kutembeza mkong’oto kwa wananchi ili kuzima vuguvugu hilo.



Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuwasiliana na kamanda Nzuki kwa njia ya simu za mkononi hakuweza kupatikana.



Wananchi
walitoa tuhuma hizo baada ya kukuta ungo ikiwa na tunguri ndani yake
ambayo inadaiwa kuwa ni ndege ya wachawi uwanjani kwake maeneo ya
makaburi Msafa.



Wananchi walijikusanya nyumbani kwa Diwani huyo
na kumshinikiza awatoe wachawi nje ili waweze kuwadhibu, amri
iliyopingwa na Diwani huyo. Kadiri mda ulivyokwenda ndivyo wananchi
walivyozidi kuongezeka na hatimaye kulijitokeza kundi la watu walioanza
kutia vurugu, hali iliyomlazimu Chehako kuomba msaada wa polisi.



Mashuhuda
wa tukio walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa polisi walipofika
waliwasihi wananchi kutawanyika kwa kuwa ungo na tunguri zake zilikuwa
zimeteketezwa kwa moto na diwani huyo mbele ya wananchi hao.



Chenako akihojiwa nyumbani kwake alisema:
Wananchi
waliendelea kupinga na kudai ndani ya nyumba kuna rubani na abiria wa
ndege nimewahifadhi…polisi wakawachagua wananchi watano na kuingia ndani
ya nyumba kuwasaka watu hao…hawakuona kitu, walitoka nje na kuwamabia
wenzao hata hivyo wenzao walibisha.



Walianza kurusha mawe
nyumba… polisi walianza kupambana nao kwa kuwarushia mabomu…hata hivyo
wananchi walikuwa wanakimbia na kwenda upande wapili kufanya vurugu.
Chehako
alibainisha kuwa ni kawada yake kuamka alfajiri kwa ajili ya sala ya
asubuhi, lakini asubuhi ya jana alishindwa kuamka mapema, hata hivyo
hakuweza kuhisi jambo lolote.
Ilipofika
saa 12 asubuhi nikaanza kusikia watu wakishangaa kitu nje, nilipotoka
nikakuta nyungo na tunguri ndani yake…mara wakaja vijana wawili na
pikipiki wakachukua ule ungo na kukimbia nao…nikawatuma vijana wawafuate
waurudishe…walifanikiwa na nyungo ile ilirejeshwa nyumbani hapa na
ndipo nilipouteketeza kwa moto.



Nilidhani yatakuwa yameisha,
lakini wananchi waliendelea kudai nimewafungia wahuska ndani, si kweli
hakuna mtu humu ndani wala mimi sijui kilichotokea hadi hivyo vitu
vikawa humu ndani.
Katika
mapambano hayo ya wananchi na polisi, wananchi kwa kutumia mawe
wamemjeruhi Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoani hapa, John Kasembe
kwa jiwe kichwani, sehemu za kisogoni ambapo ametibiwa zahanati ya
Fajima na anaendelea vizuri.



Kwa mujibu wa Kasembe, alipigwa mawe kichwani akiwa kazini kukusanya habari na wananchi waliokuwa wakiwarushia mawe polisi.



Ofisa
wa polisi ambaye jina lake hakutaka litajwe kwa sababu si msemaji wa
jeshi hilo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa gari
moja ya polisi PT 1421 limevunjwa kioo cha mbele kwa mawe.



Hadi
saa 10.00 jioni bado polisi walikuwa wanaendelea kupiga mabomu ya
machozi hewani huku wananchi wakionekana kujipanga katika makundi hali
iliyotishia usalama wa maeneo hayo.






Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za
waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani
(Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.

Wakiwa katika
mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba
mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha
Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi.

Baadhi ya barabara za mji huo zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi











MKAPA FOUNDATION KUKABIDHI NYUMBA 30 ZA WATUMISHI WA AFYA MKOANI MTWARA





Watumishi wa afya katika halmashauri za wilaya za Masasi, Newala na Mtwara Vijijini watanufaika na nyumba 30 zilizojengwa kwenye vituo vyao vya kazi. Kila Halmashauri ya Wilaya hizi itakabidhiwa nyumba 10 kwenye hafla itakayofanyika Jumatano, tarehe19 Desemba 2012 kwenye Zahanati ya Imekuwa iliyopo Mtwara Vijijini.

Nyumba hizi ni miongoni mwa nyumba 90 zinazomalizika kujengwa, katika mikoa ya Mtwara, Rukwa na Katavi. Nyumba hizi zinajengwa na Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation kwa ushirikiano na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia mradi wa uimarishaji wa mfumo wa sekta ya afya (Health Systems Strengthening), unaofadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria- Mzunguko wa 9.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, ambaye pia ni Msarifu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation.

Vifuatavyo ni vituo vya tiba ambavyo nyumba hizi 30 zimejengwa :
 
 
 
 
 
 Zahanati za Mahoha, Malatu, Tawala, Kiridu 1 na Chihanga kwenye Halmashauri ya Newala.

-Zahanati za Imekuwa, Kawawa, Kilombero, Narunga na Kiwengulo zilizopo katika Halmashauri ya Mtwara Vijijinii.
 
 
 
 
 
 
-Zahanati za Mnavira, Makong’onda, Mitesa, Majembe, Shaurimoyo na Nanyindwa zilizopo Halmashauri ya Masasi.

Zahanati hizi zimejengewa nyumba 1 hadi 2 kila moja, kulingana na mahitaji halisi ya vituo hivyo.

Aidha nyumba 60 zilizobaki, zipo katika hatua ya mwisho ya ujenzi na zitakabidhiwa rasmi kwa Halmashauri husika, kati ya mwezi Januari na Mei 2013.

Taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wadau wengine wa sekta ya afya ndani na nje ya nchi, imekuwa ikikabiliana na changamoto ya upungufu wa Watumishi wa afya ambao kwa mujibu wa takwimu ni zaidi ya 60 nchi nzima.

Aidha miradi na programu mbalimbali imeendelea kubuniwa, kwa nia ya kuwavutia na kuwabakiza watumishi wa afya kuweza kufanya kazi maeneo ya vijijini, ambayo yana changamoto nyingi za kimazingira. 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

DK. MAGUFULI AWATISHA WANANCHI KONGWA

WAZIRI wa Ujenzi Dk. John Magufuli na Rais Kikwete

WAZIRI wa Ujenzi Dk. John Magufuli, ametumia nafasi ya uwekaji wa jiwe la msingi katika barabara ya Mbande Kwangwa kuwatisha wananchi kuwa iwapo watachagua viongozi nje ya CCM watashidwa kufungua barabara hiyo.
Magufuli, alitoa kauli hiyo wakati akitoa utangulizi wa kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete katika uzinduzi wa barabara ya Mbade Kongwa yenye urefu wa kilometa 5 zilizogharimu sh bilioni 2.9.
Alisema kuwa juhudi ambazo zinafanywa na serikali ya CCM za kuwajengea barabara wananchi wa maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wanarahisisha uchumi wao.
“Leo wananchi wa Kongwa nataka niwaambie kuwa, tunaweka jiwe la msingi na nataka kuwahakikishia kuwa barabara hii itafunguliwa na wewe Rais Kikwete kabla hujamaliza muda wako, pia ni lazima tumalize ujenzi wa barabara yote yenye urefu wa kilometa 101.1.
“Nataka niwaambie watani zangu Wagogo, mkiweka madarakani mtu kutoka nje ya CCM, kuna uwezekano mkubwa akaja kufungua kipande hiki cha kilometa tano tu na kwingine akapaacha bila kupajenga, sasa nataka niwaambie mkifanya mchezo mwafaaa… lakini sipigi kampeni,” alisema Dk Magufuli.
Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kuwa ni aibu kwa nchi kama Tanzania, kuendelea kuomba omba kwa wafadhili kwa ajili ya ujenzi wa barabara.
Chanzo;Tanzania Daima 

Serikali yaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi

 



Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Meja Josephat Musira akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani)kuhusu Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi ambapo kwa awamu ya kwanza idadi ya nyumba 6064 zinatarajiwa kujengwa na mpaka sasa nyumba 1160 zimeshakamilika kwa ajili ya matumizi, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara hiyo Mhandisi Stephen Mpapasingo.

 

 Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Wizara hiyo Meja Josephat Musira



Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sehemu ya jiko katika moja ya nyumba hizo.
Baadhi ya nyumba zilizojengwa eneo la Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi.
Picha na Hassan Silayo.
















Popular Posts