Monday, June 3, 2019
Monday, July 6, 2015
Dr Shein Apitishwa Kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar
Kamati kuu maalum ya chama cha mapinduzi Zanzibar kwa kauli moja
imempitisha Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia
chama cha mapinduzi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wajumbe wa NEC wa Zanzibar wanounda
kamati maalum ya Zanzibar kukutana hapa Zanzibar katika ofisi kuu ya CCM
na kuamua kumuidhinisha Dr Shein kugombea tena kiti hicho cha urais
baada ya wajumbe karibu 102 ambao ni aslimia 83 kuridhia Dr Shein
agombee.
Awali Dr Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar
alilazimika kuondoka ndani ya kikao ili ijadaliwe na wanachama hao
ambapo kiti hicho kilishikwa kwa muda na Dr Mohamed Gahribu Bilali makamu
wa rais, ambapo baadaye akizumgumza na wanaccm hao waliokubali Dr Shein
aliwahidi wanachama wa CCM kuwa uamuzi wake uko palepale wa kutekeleza
ilani ya CCM ya kuitumikia Zanzibar.
Katika hatua nyengine naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar akizungumza
baada ya kikao hicho alisema CCM haiwezi kupinga au kukubali suala la
majimbo,wao wanasubiri maamuzi ya tume na wako tayari kwa umauzi wowote
utakaotolewa na tume ya uchaguzi ambayo inatarajiwa kutangaza majimbo
mapya leo asubuhi.
Kupitishwa kwa Dr Shein kugombea urais wa Zanzibar na kamati maalum
ni hatua ya kwanza na sasa shuguhli yote inahamia Dodoma ambapo jina la
Dr Shein litajadiliwa na kamati kuu na baadaye kutakiwa kuidhinishwa na
kupitishwa na halmashuri kuu ya CCM, nafasi ya urais wa Zanzibar
inaamuliwa na NEC na siyo na mkutano mkuu waccm.
EDSONI KAMUKARA PUMZIKA KWA AMANI

Edson Slavatory Kamukara, amezikwa kijijini kwao Ihangiro
wilayaniMuleba, huku akiacha majonzi kwa familia yake, baada ya kuacha
mtoto mmoja ilhali mama yake akisumbuliwa na kupooza, ambapo siku chache
zilizopita, Edson alitokea Muleba kumuangalia mama yake, kama
alivyozungumza dada wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Joyce.
huku
akisema kuwa madakatari wanasema inaonekana alikufa baada ya kukosa
hewa huku, chumbani kwake kukikutwa na damu, akiongeza kuwa alikuwa
anakamilisha kazi ya uandishi uliokuwa ukiwahusu vigogo na kama habari
zake zingetoka, saizi nchi ingekuwa inaongea mambo mengine.Waadishi kutoka chama cha waandishi habari mkoani Kagera KPC, walishiriki maziko hayo na ndiyo walihusika kubeba mwili wa marehemu na picha chini ni Charles Mwebeya akitroa rambirambi yao kwao dada Joyce ambaye anaishi Dar na alikuwa karibu na marehemu


Marehemu Edson Kamukara, ameacha mtoto anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 3 hadi 4 aitwaye Edigar Ishengoma, na marehemu alianzia kazi ya uandishi katika gazeti la Majira, akafanya jambo leo, tanzania dai, na hatimaye mwanahalisi publishers ambapo amefanyia kwa kipindi cha miezi minne, na alikuwa anakamilisha habari kuhusu matatizo ya wananchi kupitia viongozi mkoani Kagera.
Na Mwanaharakati.
MWENGE WAZINDUA MIRADI YA THAMANI YASHILINGI BILIONI KUMI NA TATU NJOMBE
Miradi ya Shilingi billion Kumi na tatu (13,201,109,235.55) inatalajiwa
kuzinduliwa,kuwekewa jiwe la Msingi na kukaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru
katika Mkoa wa Njombe,hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi wakati akipokea Mwenge wa
Uhuru kutoka Mkoa wa Iringa.
Nchimbi alisema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Njombe
utakimbizwa katika halmashauri Sita ambazo ni Njombe,Makete,Ludewa,Wanging’ombe,Mji
Njombe na Mji Makambako,Katika
halmashuri jumla ya
Miradi 45 itatembelewa na Mwenge wa Uhuru.
Alisema kuwa Miradi hiyo ipo katika sekta ya Afya
,Elimu,Kilimo,Miundombinu,Utalii na Misitu,miradi mingi imekamilika na kuanza
kutumika .
Naye mkimbiza Mwenge Kitaifa Juma Khatibu chum alisema kuwa amefurai kuingia
Mkoa wa Njombe na anarajia
kufungua,kukagua miradi mizuri kwani kutokana na mapokezi walioyapata ya
wananchi wengi waliojitokeza kuupokea
Mwenge wa Uhuru, Kauli mbiu ya Mwenge Mwaka huu ni “Tumia haki yako
kidemokrasia ,Jiandikishe na kupiiga kura
katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Wednesday, June 24, 2015
Dkt. Nchimbi atangaza rasmi kutogombea Songea
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi wakiwemo wanachama wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma,
wamejikuta katika hali ya sintofahamu huku wengine wakimwaga machozi
baada ya mbunge wa jimbo hilo, mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza rasmi
kutogombea tena ubunge katika jimbo hilo.
Katika uwanja huu wa majimaji mjini songea, mbunge wa jimbo la Songea mjini, mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyelitumikia jimbo hilo kwa miaka 10 akakutana na wanachama wa chama cha mapinduzi pamoja na kuelezea mafanikio mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati na shule za sekondari lakini pia akatumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo la songea mjini.
Tamko hilo la dkt. Nchimbi likazua simanzi kwa baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM hapa Songea huku wengine wakishindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga machozi.
Katika maelezo yao wanachama hawa wanasema kuachia ngazi kwa Dkt, Nchimbi kutogombea katika jimbo hilo kunatoa fursa kubwa kwa vyama vya upinzani kuchukua jimbo hilo hali ambayo hawakubaliani nayo.
Hata hivyo wanachama hao wakamuomba mbunge huyo kutengua msimamo wake na kumtaka arejee tena kugombea jimbo la Songea mjini, jibu la dkt. Nchimbi ikawa anaenda kufikiria.
Katika uwanja huu wa majimaji mjini songea, mbunge wa jimbo la Songea mjini, mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyelitumikia jimbo hilo kwa miaka 10 akakutana na wanachama wa chama cha mapinduzi pamoja na kuelezea mafanikio mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati na shule za sekondari lakini pia akatumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo la songea mjini.
Tamko hilo la dkt. Nchimbi likazua simanzi kwa baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM hapa Songea huku wengine wakishindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga machozi.
Katika maelezo yao wanachama hawa wanasema kuachia ngazi kwa Dkt, Nchimbi kutogombea katika jimbo hilo kunatoa fursa kubwa kwa vyama vya upinzani kuchukua jimbo hilo hali ambayo hawakubaliani nayo.
Hata hivyo wanachama hao wakamuomba mbunge huyo kutengua msimamo wake na kumtaka arejee tena kugombea jimbo la Songea mjini, jibu la dkt. Nchimbi ikawa anaenda kufikiria.
Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limemteua Charles Boniface Mkwassa, kuwa kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania(Taifa Stars)

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, mholanzi Mart Nooij.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema
wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia
wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.
“Mpira
wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika
mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu
ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema Malinzi.
Duniani
kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na
vijana wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri
wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora.
Nchi
za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na
wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi
wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana.
TFF
ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua
zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo
la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana
mwaka 2016.
Kikosi
cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi
za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani
mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza
michezo ya kirafiki.
Naye
Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa
habari alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa
miguu nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa
timu ya Taifa.
Nooij
alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote
alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho
wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka
Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.
Wakati
huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa
kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa
ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa
kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya
kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.
Malinzi
amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa
timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana
kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo
makocha hao wazawa wamekizi.
Kocha
Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho)
alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua
benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa
mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao
wazawa” aliongeza Malinzi”
Aidha
Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa
timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya
kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.
U15 Yaingia Kambini
Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania, imeingia
kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume kujiandaa na
mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya siku ya
jumapili.
Kikosi
hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza
mchezo huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na
kuwaongeza wengine watakaoneka katika kikosi hicho.
U15
ni mpango wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania
kufuzu ka fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini
Madagascar, ambapo vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia
mwakani wakati michezo ya kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.
NB:
Kesho siku ya jumatano kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Mkwasa na
msaidizi wake Hemed Moroco wataongea na waandishi wa habari saa 5:30
asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.
Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
Mjamzito Afanyiwa Ukatili wa Kutisha

MJAMZITO aliyefahamika kwa jina la Rotha Bujiku, amejifungulia bafuni karibu na zahanati ya kijiji baada ya kudaiwa kufukuzwa na wauguzi waliokuwa zamu siku hiyo, kwa maelezo kuwa anajifungua kila mwaka.
Tukio hilo lilitokea wilaya ya Maswa katika mkoa wa Simiyu majira ya
saa 2 asubuhi baada ya mjamzito huyo kufika katika zahanati hiyo kwa
lengo la kupata huduma ya kujifungulia kwa wataalamu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililovuta umati wa watu,
mjamzito huyo alikataliwa kupokewa na muuguzi wa zamu aliyetajwa kwa
jina la Constansia John.
Ilielezwa kuwa muuguzi huyo alikataa kumpokea kwa madai kuwa mjamzito
huyo alishapewa maelekezo tangu awali kuwa anatakiwa akajifungue katika
hospitali ya wilaya ya Maswa kwani amekuwa akizaa watoto kwa mfululizo.
Inaelezwa kwamba, wakati Rotha akiugulia maumivu ya uchungu, muuguzi
huyo alimpigia simu ya mkononi Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo, Leticia
Kachumi kumjulisha hali hiyo na alipofika alitaka mjamzito huyo aondoke
katika eneo hilo na atafute usafiri ili aweze kufika katika hospitali ya
wilaya kama alivyoelekezwa katika siku za nyuma.
“Leticia alipofika hapo zahanati baada ya kupigiwa simu na
Constansia, licha ya kumuona anaendelea kulalamika kutokana na uchungu
alimwamuru aondoke eneo hilo mara moja na atafute usafiri wa kumfikisha
hospitali ya wilaya iliyoko umbali wa kilomita 36, kwani walishamweleza
kuwa amekuwa akizaa mfululizo na hiyo ni mimba ya kumi na moja,” alisema
shuhuda, Kundi Mageni.
Kutokana na hali hiyo, mjamzito huyo alilazimika kuondoka zahanati
hapo bila msaada wowote na baada kufika karibu na nyumba iliyoko na
zahanati hiyo, alikwenda katika bafu la nyumba ya jirani ambalo halina
sakafu na kujifungulia humo na baadaye kusaidiwa na wasamaria wema
waliosikia sauti ya mtoto.
“Kwa kweli huyu mama amejifungulia katika mazingira machafu na
hatarishi kwa afya yake na mtoto aliyemzaa. Kwa kweli hili ni tukio la
kusikitisha. Huwezi kuamini wauuguzi hao ambao ni wanawake kumtendea
mwenzao ukatili wa kiasi hiki,” alisema Pili Kidesela, Diwani wa kata ya
Shishiyu (CCM).
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk Jonathan Budenu aliyefika katika
eneo la tukio muda mfupi baada ya kupata taarifa hizo, alisema kitendo
kilichofanywa na wauguzi hao ni kinyume cha maadili ya kazi yao na hivyo
ni lazima hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa wote waliohusika.
Mwingine ajifungulia kichakani
Wakati hayo yakitokea Maswa, mkoani
Arusha binti mwenye umri wa miaka 17 alijikuta akijifungulia kichakani
baada ya kuzidiwa uchungu wakati akisubiri kuombewa kwenye mkutano wa
dini uliofanyika Viwanja vya Magereza, Kisongo nje kidogo na Jiji la
Arusha.
Anna Ngitoria, mkazi wa Endurimeti, wilayani Arumeru, alikuwa
miongoni mwa mamia ya wakazi wa Arusha, Kilimanjaro na vitongoji vyake
waliokuwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja huo wa magereza kwa
ajili ya kile kilichodaiwa kuwa ni maombi yaliyoandaliwa na kituo kimoja
cha redio cha jijini Arusha, Radio Safina.
Kwa kawaida uongozi wa kituo hicho huandaa makongamano ya kila mwezi
kwenye uwanja huo wa Kisongo na kujumuisha mamia ya watu, wengi wao
wakiwa ni wanawake na wasichana ambao hupendelea kuhudhuria maombezi
hayo kwa matarajio tofauti.
Mikusanyiko ya maombi ya ‘Radio Safina’ imekuwa ikikusanya watu wengi
mithili ya ‘Kikombe cha Babu,’ ambacho nacho kilivuma sana miaka mitatu
iliyopita na tukio la msichana huyo kujifungua katika moja ya matukio
hayo kimezua hisia tofauti mjini hapa.
Akizungumza katika hospitali ya Mount Meru ambapo amelazwa kwa sasa,
binti huyo, Anna amekiri kuwa alijifungua kabla ya wakati kwa sababu
alikuwa na ujauzito wa miezi saba tu.
Mtoto wake njiti sasa anahudumiwa katika wodi maalumu iliyopo hospitalini hapo na wauguzi wanasema anaendelea vizuri.
Mpekuzi blog
TANZIA: Mbunge wa Geita, Donald Max afariki Dunia.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geita (CCM) Mheshimiwa Donald Kevin Max (58)(picha) amefariki dunia.
Kufuatia
taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) kwa Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na
umma kwa ujumla, Mhe. Max amefariki dunia tarehe 23 Juni, 2015 katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa
mujibu wa taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea
kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia kadri
zitakavyopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba ya Mazishi.
“BWANA ametoa, BWANA ametwaa,
Jina la BWANA lihimidiwe.” Amina.
Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
DODOMA
Urais CCM: Waliorudisha Fomu ya Urais
WIKI moja kabla ya kwisha kwa muda wa warudisha fomu kwa makada wa CCM
waliojitokeza kuwania kupitishwa na chama hicho kuwania urais wa
Tanzania, ni wanachama sita tu kati ya 39 ndio waliorudisha fomu mpaka
sasa.
Kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa urais ndani ya
CCM, mwisho wa kurudisha fomu ni Julai 2, mwaka huu ambapo kila
aliyechukua fomu anatakiwa kuwa na wadhamini 450 kutoka mikoa 15 ambapo
mitatu iwe ya Zanzibar.
Idadi ya wanachama waliojitokeza mwaka huu inaonekana kuwa ni kubwa,
mara tatu zaidi ya waliojitokeza mwaka 2005 ambapo wagombea walikuwa 11,
ingawa Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyeibuka kidedea na kutetea tena
ushindi wake mwaka 2010.
Waliorudisha fomu ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Makamu
wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Makongoro Nyerere (Mbunge wa Afrika
Mashariki), Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli, Waziri wa Kilimo, Chakula
na Ushirika, Steven Wassira na Balozi Ally Karume.
Wengine waliojitokeza kuchukua fomu ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
Mawaziri wakuu wa zamani, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Pia wamo Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri
wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Mbunge
waSengerema, William Ngeleja, Mkazi wa Musoma mkoani Mara, Boniface
Ndengo na mkulima kutoka Kijiji cha Mjimtala Wilaya ya Kasulu, Kigoma,
Idelphonce Bilohe na Balozi Augustino Mahiga.
Wengine ni Dk Hans Kitime, Dk Mwele Malecela, Mbunge wa Nzega Dk
Hamis Kingwangala, Balozi Amina Salum Ally, Naibu Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, Mtumishi wa CCM, Amos
Siyantemi, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, Wakili Mwandamizi Godwin
Mwapongo, Peter Nyalile, Leonce Mulenda, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino
Ramadhani na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro.
WanaCCM wengine wanaoutaka Urais ni Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani, Monica Mbega, Patrick
Chokala, Joseph Chagama, Malick Malupu, Ritha Ngowi na mwanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Mzumbe, Amos Robert.
Mpekuzi blog
Tuesday, June 23, 2015
Nape: CCM itashinda tu hata kwa goli la mkono

CCM imesema kuwa itahakikisha inarudi Ikulu hata “kwa bao la mkono” wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.
Katibu
wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema hayo katika
mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Nyehunge wilayani
hapa.
Neno
“bao la mkono” hutumiwa kama goli lililofungwa kwa kuupiga mpira kwa
mkono kinyume cha taratibu za mpira, lakini hukubaliwa kwa kuwa mwamuzi
anakuwa hajaona kitendo hicho.
“Rangi
inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa
na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile,
CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao ni bao tu ili
mradi refa hajaona,” alisema Nape.
Nape,
aliye kwenye ziara ya katibu mkuu wa CCM, aliwataka wananchi wa
Sengerema kusubiri ushindi wa chama hicho na kuwakumbusha kuwa wanapaswa
kuiweka CCM kuanzia udiwani mpaka ubunge kwa nafasi ya urais tayari
kuna uhakika.
Katika
mkutano huo, Nape alisema ana uhakika CCM itashinda baada ya kushuhudia
mwitikio wa Watanzania tangu alipoanza kuongozana na Kinana katika
ziara zake za kuizunguka nchi na kuzungumza na wananchi pamoja na
kusikiliza kero zao.
Amebainisha
kuwa amejifunza na kujiridhisha kuwa chama chake bado kinapendwa
miongoni mwa wapigakura waliofikiwa tofauti na vyama vya upinzani.
“Tumefika
maeneo mengi ambayo upinzani haujafika. Huko tuna hazina kubwa ya
wanachama. Hakuna namna Ukawa wanaweza kuingia Ikulu mwaka huu,”
alisisitiza.
Wapinzani waja juu
Kauli
hiyo ya Nape ilipingwa na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani
waliosema kuwa mtendaji huyo anamaanisha kuwa CCM itaiba kura.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa hakutaka kabisa kuzungumzia kauli ya Nape zaidi ya kusema watakutana Oktoba.
“Kwa
bahati mbaya kauli za Nape siwezi kuzijibu. Kauli za Nape zichukue kama
zilivyo, ingekuwa ni (katibu mkuu wa CCM, Abdulraham) Kinana,
ningemjibu lakini ajue kuwa tutakutana Oktoba,” alisema Dk Slaa alipoulizwa na Mwananchi kuhusu suala hilo.
Naibu
mkurugenzi wa habari wa CUF, Abdul Kambaya alisema kauli ya Nape
inamaanisha kuwa CCM itaiba kura kwani kwa kawaida bao la mkono ni bao
haramu.
“Kauli
hiyo inaonyesha dhahiri kuwa wataiba kura na kwa sababu katiba yetu ni
mbovu matokeo yake yatatangazwa kama yalivyo… hiyo ndiyo maana ya bao la
mkono,” alisema.
Kambaya
alisema hata hivyo CCM isijiaminishe kwa lolote kwani hivi sasa
wananchi wamebadilika kimtazamo kutokana na matatizo mengi yanayoiandama
nchi kama vile afya, elimu duni na migogoro ya ardhi.
“Lakini
CCM wajue kuwa kutatokea machafuko makubwa iwapo wamejipanga kuingia
Ikulu kwa njia hiyo ya bao la mkono. Kauli ya Nape ni ya kidikteta na
inaonyesha dhahiri kuwa wamejikita kwenye utawala wa mabavu,” alisema.
Kadhalika
Kambaya alisema CUF imeshajipanga na kuhakikisha inaziba mianya yoyote
ya wizi wa kura kuanzia kwenye Daftari la Wapigakura hadi katika ujanja
wa kuwapigisha kura marehemu, askari na wanajeshi kama inavyodaiwa
kufanyika Zanzibar.
Katibu
mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema Nape anatoa maneno ya
kuvutia kwake kama njia ya kuwakatisha tamaa wapinzani na wanachama,
hata hivyo alimuonya kuwa siasa za sasa hazitabiriki kwa njia hiyo.
“Lakini
ajue kuwa mambo yanabadilika. Anaweza kushangaa mambo yakawa mengine,
sasa hivi wananchi wana mwamko mkubwa na wanabadilika,” alisema.
Alisema
CCM haina haja ya kujitapa kwa sasa wakati bado haijapata mgombea kwani
huenda wakapata ambaye wananchi hawatamuunga mkono hata kidogo.
“Bado
CCM wana makundi jambo ambalo kwao ni udhaifu. Lakini pia lazima wajue
kuwa wakati wa mchujo utakapofika, wale watakaokatwa hawatafurahia
kuachwa na hapo kuna sababu za wapinzani kushinda,”alisema.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema wakati Nape anabishana kwenye majukwaa, NCCR inaendelea kupiga kazi.
“Badala ya kujadili hoja za msingi zenye manufaa kwa wananchi yeye anajadili CCM kupiga bao?” alihoji Mbatia.
Akijibu
hoja ya Nape, Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mrikaria alisema kauli ya
kada huyo imekaa kisiasa na si kiuhalisia kwani ni kawaida kwa chama
cha siasa kujiaminisha kuwa kitashika dola.
“Unajua
chama chochote hata kiwe kidogo lazima kikiri kuwa kitashika dola ili
mradi ilani yao inakubalika na unakubaliwa na wananchi kwa sababu chama
chochote nia yake ni kuingia ikulu,” alisema.
Alisema
hata vyama vidogo kama TLP hukiri ushindi kwa kusema kuwa vinataka
kuingia ikulu kwa sababu chama hakiwezi kukiri mbele ya wananchi kuwa
hakitashinda.
source Mpekuzi
Serikali yakana kumtorosha Rais wa Sudani

Serikali ya Afrika Kusini imekana ripoti kwamba mawaziri wake walipanga njama ya kumtorosha rais wa Sudan Omar El Bashir wiki iliopita.
Katika tukio hilo nusura rais huyo akamatwe kufuatia agizo la
mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na
mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Mahakama ya Afrika Kusini ilimuagiza Bashir kusalia nchini humo huku
ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo litekelezwe. Lakini kabla ya
mahakama hiyo kutoa uamuzi wake bwana Bashir aliondoka nchini Afrika
Kusini na kurudi nyumbani.
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa
viongozi wa bara Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba
ilihitajika kumkamata kwa kuwa mwanachama wa ICC.
Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times nchini Afrika Kusini limenukuu
duru za serikali kwamba katika mkutano wa mawaziri ilikubalika kwamba
Afrika Kusini itamlinda hata iwapo italazimika kukiuka uamuzi wa
mahakama na kukiuka katiba.
Katika taarifa yake,serikali imekana kwamba kulikuwa na mkutano wa
siri na kwamba itaipatia mahakama hiyo maelezo kuhusu vile Bashir
alivyoondoka nchini humo.
Mahakama kuu imeipatia serikali ya taifa hilo hadi alhamisi kubaini ni vipi aliruhusiwa kuondoka.
Ngassa arejea Yanga kiaina
Mshambuliaji wa Free Stars ya Afrika Kusini,Mrisho Ngassa (kulia)
akifanya mazoezi na timu yake ya zamani Yanga baada ya kurejea nyumbani
kwa mapumziko kwenye uwanja wa karume Dar es Salaam Jana.Picha na Said
Khamis.
Dar er Salaam. Mshambuliaji Mrisho Ngassa
aliyesajiliwa na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini hivi
karibuni, jana aliibuka katika mazoezi ya timu yake ya zamani Yanga.
Ngassa alisajiliwa na Free State Stars kwa mkataba
wa miaka minne mwishoni mwa mwezi uliopita na alirudi nchini kwa ajili
ya kuitumikia Taifa Starsiliyokuwa ikicheza dhidi ya Uganda katika mechi
ya kuwania kufuzu kushiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza
ligi za ndani (CHAN), ingawa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilimzuia
kwani ameishasajiliwa nje ya ligi ya Tanzania.
Gazeti hili lilimshuhudia mshambuliaji huyo
akifanya mazoezi na Yanga mwanzo mwisho na alipomaliza mashabiki wa
klabu hiyo walilisukuma gari lake mpaka nje geti wakionyesha mapenzi kwa
mchezaji huyo.
Ngassa ameitumikia Yanga kwa mafanikio kabla ya kuamua kuachana nayo na kwenda kusaka ulaji katika klabu ya Free State.
Ngassa alisema ameamua kufanya mazoezi na Yanga kwani bado iko moyoni mwake na hakuondoka kwa ubaya.
“Hapa kama niko nyumbani, kwani hii ni timu iliyo
moyoni mwangu hivyo kama niko Dar es Salaam sioni ubaya kufanya mazoezi
na Yanga kwani naamini kuna siku nitarudi hapa,”alisema Ngassa.
“Najiweka fiti wakati nikisubiri klabu yangu
initumie tiketi ya kurudi Afrika Kusini maana walinipa ruhusa ya kuja
Dar es Salaam kwa ajili ya timu ya Taifa, lakini nikazuiwa kucheza mechi
na Uganda,” alisema Ngassa.
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Ngassa kwani aliifungia Yanga mabao manne tu licha ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Aprili
Urais 2015: Mwanamke wa 5 ajitosa kuchukua fomu CCM

Mwananmke mwingine ambaye ni kada wa CCM, Ritta Ngowi amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu jana makao makuu ya CCM
mkoani Dodoma Ngowi alisema akifanikiwa kuwa rais ataanzisha kituo
kikubwa cha kuwahudumia wastaafu, walemavu, wasiojiweza na vijana.
Kingine atakachofanya ni kuendeleza mazuri yaliyofanywa na marais
waliopita, lakini zaidi akiweka mkazo kwenye masuala ya elimu na kukuza
uchumi.
Aidha Ritha anafanya , idadi ya wanawake waliojitosa mbio za urais kufikia watano kati ya 39 waliochukua fomu hadi sasa.
Wanawake wengine ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro,
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa (NIMR), Dk Mwele Malecela,
Balozi Amina Salum Alli na Monica Mbega.
Kocha wa Taifa Stars Maart Nooij na Benchi Lake Lote La Ufundi Watimuliwa Kazi

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Maart Nooij akisindikizwa na ulinzi mkali usiku wa kuamkia leo baada ya kumalizika kwa mchezo wa Tanzania na Uganda wa kuwania kufuzu fainali za CHAN katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar ambapo Taifa Stars ilichapwa 3-0. *******
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Juni 20, 2015
Monday, June 22, 2015
Lowassa Azidi Kupata Mapokezi Makubwa
WAZIRI
Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina
lake katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama
chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa
Tanzania.
Lowassa
aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi
wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa
shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.
"Nimekuwa
mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya
kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza
kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata
jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa
jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi
tu". alisema Lowassa.
Lowassa
aliwasili Mkoani Ruvuma mapema jana mchana akitokea Mkoani Iringa
kwaajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi
ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea
kufunga barabara kuu ya mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya
paa la jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza nao.

Wednesday, June 17, 2015
PINDA APATA WADHAMINI NJOMBE
Mgombea wa Urais kupitia chama cha mapinduzi na waziri
Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda amewataka wananchama wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe kuendelea
kujitokeza kwa wingi na kuendelea kuwadhamini wagombea mbalimbali waliochukua fomu na watakaochukua fomu za kugombea nafasi ya Urais bila kubagua Mgombea yoyote.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa chama
cha mapinduzi Mkoa wa Njombe ambapo mamia ya wananchama wa chama hicho walijitokeza kumdhamini ili aweze kugombea
Urais kupitia chama cha Mapinduzi
Alisema kuwa waliojitokeza kuchukua fomu kupitia chama
cha mapinduzi ni wengi lakini atakayepitishwa kupitia chama hicho ni mgombea
mmoja ambaye atawakilisha chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi unatakofanyika
mwezi wa kumi na mgombea huyo ndie atanadiwa na chama hicho akishindanishwa na
vyama vingine kwenye uchaguzi Mkuu.
Wanachama waliojitokeza kumdhamini Mgombea huyo
wamesema kuwa wanaimani kubwa na mgombea huyo na kuamini kuwa chama kitampitisha
kuwakilisha chama hicho kwenye kugombea Urais.
Kwa Mkoa wa Njombe tayari wagombea January
Makamba,Bernard Membe,Stive Wassira,Samweli Sitta,Makongoro Nyerere ,Monica
Mbega ,Amosi Siyatemi na Prof.Mark Mwandosya.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Popular Posts
-
Umati wa watu wakisubiri kutambua maiti za watu waliofariki katika ajali ya basi la Majinja Express katika chumba cha kuhifadhia maiti ...
-
UZEMBE wa dereva wa basi Mitsubishi Fuso, mali ya kampuni ya Another G Trans lenye usajili Namba T.927 CEF, Nicolaus Magula (30) umes...
-
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain (mst) Aseri Msangi amemwagiza Mkurugenzi wa halmashuri ya wilaya ya Njombe kuakikisha barabara kutoka Ikond...
-
Askari wawili wa Jeshi la Polisi katika Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani, wameuawa baada ya kushambuliwa kwa silaha na m...

