Kichanga kilichotupwa Iringa Sokoni.
ito umetolewa kwa kina mama na wadada waishio mkoani Iringa wenye tabia ya kupenda kutupa watoto pindi wanapojifungua kuacha kabisa kufanya kitendo hicho kwani wanapoteza Taifa la kesho.
Hayo
yalisemwa na Kamanda wa polisi mkoani hapa ACP Ramadhani Mungi alipokuwa
akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com
ofisini kwake kuhusiana na taarifa za kutupwa kwa mtoto kachanga maeneo ya
karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
“leo
saa mbili asubuhi tulipokea taarifa ya kuwa kuna katoto kametupwa kwenye jalala
lililopo karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya, mtoto huyo ni wa jinsia ya kiume na
hata kitovu chake bado hakijakatwa uchunguzi unaonyesha inawezekana kuna mtu
alitoa mimba na akaenda kuitupa pale hivyo bado tunaendelea na uchunguzi na
endapo tukimpata mtu huyu aliyefanya kitendo hicho cha kikatili basi hatua kali
za kisheria zitachukuliwa, watu wanafanya kitendo hichi hawajui kuwa hawa
wanaowatupa ndo Taifa la kesho huwezi jua huyo uliyemtupa angekuja kuwa nani
mbeleni,” alisema Kamanda.
Tukio
lingine, Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wanne kwa kosa la
kumchoma moto mwanafunzi wa Chuo cha Ruco aliyetambulika kwa jina la Daniel
Lema (25) mkazi wa Kihesa mkoani hapa.
Kamanda
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 20 June majira ya
saa 9 usiku huko maeneo ya Kihesa.
“majira
ya saa 9 usiku polisi walipigiwa simu na wasamalia wema kutoka kihesa kuwa kuna
mtu amefungwa kamba mikononi na anatembea huku anawaka moto mwilini polisi
wakaenda eneo la tukio na kumkuta mtu huyo ameanguka chini huku bado anawaka
moto basi polisi wakamfungua na kumpeleka hospitali kwani alikuwa bado anathema”
alisema kamanda Mungi.
Kamanda
alisema taarifa zinaonyesha kuwa mwanafunzi huyo ambaye yuko mwaka wan ne katika
kitivo cha sheria alikuwa katika bar ya Inbox iliyopo kihesa akiangalia mpira,
wakati akirudi kwake maeneo ya Transfoma alipitia kwenye grory grocery iliyopo
pembezoni mwa grory lodge na kukuta imefungwa ambapo mlinzi alipomuona alimuita
lakini mwanafunzi huyo alikimbia baada ya kumuona mlinzi akiwa na kirungu.
“mwanafunzi
Yule alikimbia na mlinzi alimkimbiza na kumkamata ambapo alimpeleka kwa meneja
wa hiyo lodge hata hivyo meneja huyo aliwapigia walinzi wengine kutoka katika
kampuni ya Juka Security ili waje kumchukua kijana huyo wampeleke kituo cha
polisi walinzi walifika wakiwa watatu na kumchukua mtu huyo ambapo walipofika
mbele wakamfunga mikono yake na kamba na kisha kummwagia mafuta na kumchoma
moto kisha wakakimbia.” Alisema.
Hata
hivyo watuhumiwa hao walitaka kutoroka mkoani hapa mara baada ya kutenda
kitendo hicho ambapo walikamatwa kabla hawajafanikiwa kutoroka, watuhumiwa hao
ni Musa Nganga (28), Costa Mganyuko (38), Steven Kalolo (24) pamoja na Samson
Peter (24) wote wakazi wa Kihesa, pia kwa upande wa mgonjwa hali yake sio nzuri
bado.
NA
DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA NA CHRISSMPUZU.BLONGSPORT.COM -NJOMBE