Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi kushoto akisalimiana na mwakilishi wa kampuni ya Dandu ambao lori lao limeteketezwa kwa moto .
Hii ndio mitumba iliyohifadhiwa mali ya wizi
Mitumba hiyo ikionekana kwa nje baada ya kujaa ndani ya nyumba hiyo kupita kiasi
Safari ya kwenda kubaini mali ya wizi iliyofanywa na kamanda wa polisi Iringa
RPC Iringa Ramadhan Mungi akiangalia mitumba iliyohifadhiwa porini baada ya kuporwa
kamanda wa polisi Iringa Ramadhan Mungi akimwonyesha mmiliki wa nyumba iliyohifadhi mali hizo za wizi kulia na dereva wa gari hilo mbele lenye namba T 185 CJM ambalo ndilo lilikuwa likisomba mali hizo za wizi kutoka katika lori lililochomwa moto
Watuhumiwa wa wizi wa mali zilizokuwa zikisafirishwa na lori la kampuni ya Dandu
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akionyesha lori hilo mali ya kampuni ya Dandu ambalo limechomwa moto na dereva na utingo wake baada ya kufaulisha mali zote kwa lengo la kuiba
JESHI la polisi mkoa
wa Iringa kupitia dhana ya polisi
jamii na ulinzi shirikishi
limefanikiwa kukamata mali za wizi ambazo zilizokuwa zikisafirishwa kwenda nchi ya DRC Kongo
zikiwa na thamani ya Tsh milioni 100
pamoja na lori lenye thamani ya Tsh milioni 100 ambalo liliteketezwa
kwa moto kabla ya dereva na utingo wa lori hilo
kulichoma moto kama njia ya kupoteza ushahidi.
Imedaiwa kuwa watu
zaidi ya 6 wanashikiliwa na jeshi
hilo la polisi akiwemo
dereva na utingo wake ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la wizi
huo.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Iringa Ramadhan Mungi alisema
kuwa tukio hilo lilitokea juzi May 31 ambapo askari
wa doria wilaya ya Mufindi wakiwa katika shughuli hiyo ya doria walifanikiwa
kuliona lori hilo likiwa
limeegeshwa kando ya barabara ya
Iringa –Mbeya eneo la Kinegembasi wilaya
ya Mufindi huku likiwa limeteketea kwa moto katika kibini yake.
Alisema kuwa watu hao
waliteketeza lori lenye namba za usajili T527 DPQ likiwa na tela lenye namba T 974
EFE aina ya scania mali ya kampuni ya Dandu ambalo walilikuta
likiungua huku silizi zake zikiwa
zimefunguliwa na baada ya uchungu wa awali walibaini
kuwa lori hilo lilikuwa limebeba
mitumba na viatu na baada ya msako ndipo
walipofanikiwa kukuta
mitumba hiyo ikiwa imefichwa katika nyumba moja kuukuu mali ya mama Gray Mpinga mwenyeji wa Maguhani Mufindi .
Alisema kuwa
mali hizo ambazo ni mabelu ya mitumba na
viatu yalitoka Bandarini kwenda DRC na kuwa dereva wa lori hilo ni Enedia Christian (26) mkazi wa
Mbeya na utingo wake Deus
Gendo (20) mkazi wa Mbeya .
Kamanda Mungi alisema kuwa utingo na
dereva wa lori hilo baada ya kufika kijiji hicho cha Maguhani
walivunja kontena na kushusha mali zote na kuzihifadhi katika nyumba
hiyo kabla ya kutafuta mteja na
kisha lori kulichoma moto .
Alisema kuwa baada
ya kufanya wizi huo
walitoweka na simu zao kuzimwa na kutokana na jitihada za jeshi la
polisi kupitia mtandao wa
kimawasiliano wa kuthibiti na wizi wa
mitandaoni walifanikiwa kuwanasa
watuhumiwa hao wakiwa kijiji cha Nyololo
Mbali ya kuwakamata
dereva na tingo pia
polisi wamekamata watu
mbali mbali wahusika wa mtandao huo na kuendelea kumsaka Masko Buhewa mkazi wa Nyololo
kwa kuhusika na umilikiwa wa mtandao huo
USIKOSE HABARI HII INAENDELEA ZAIDI
No comments:
Post a Comment