Msichana Yusta Lucas wa miaka ishirini aliyefungiwa ndani kwa miaka
mitatu huku akipewa adhabu ya kung'atwa na kuchomwa na pasi ameruhusiwa
kutoka hopitalini baada ya hali yake kuendelea vizuri huku jeshi la
polisi likikamilisha uchunguzi na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani tarehe
11 Juni mwaka huu.
ITV imefika katika hospitali ya Mwananyamala
alikokuwa amelizwa Yusta Lucus na kukutana na ndugu zake akiwemo mama
ake mzazi ambaye amefafanua kwa uchungu hali aliyomkuta nayo binti yake
na hatua alizochukua mara baada ya kupokea taarifa za tukio hilo.
Kaka wa Yusta licha ya kutoa shukrani kwa msamaria
aliyetoo habari za mdogo wake kwa jeshi la polisi ameelezea kuendelea
kusikitishwa na kitendo hicho cha kinyama na kutoa wito kwa Watanzania
kuwa na moyo wa kusaidia wale wote wanaopatwa na matatizo kama

kuwa na moyo wa kusaidia wale wote wanaopatwa na matatizo kama hayo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni
Camillius Wambura amesema tayari uchunguzi umeshakamilika ikiwemo
kumpima akili mtuhumiwa na tayari shauri hilo liko kwa mwanasheria mkuu
wa serikjali na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani tare 11 Juni mwaka huu.
CREDITS:ITV
No comments:
Post a Comment