Monday, June 16, 2014

NAPE ATINGISHA JIMBONI MNYIKA, LEO

Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,  leo ametoboa siri kwamba, viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema wamelazimika kukumbatia kinachoitwa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA), ili kujaribu kupoza migogoro iliyopo ndani ya chama hicho ambayo inakiua.

Amesema, siyo kweli kwamba Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Woilbrod Silaa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe wanahangaika na muungano huo unaoitwa wa kutafuta Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa lengo la kusaidia wananchi bali ni kujaribu kupoza makali, baada ya kuona kwamba chama chao kimo katika mgogoro mkubwa wa ndani ambao si mda mrefu utaua.

"Chadema wapo katika mgogoro mkubwa kutokana na baadhi ya viongozi wake hasa wa ngazi za juu kukiendesha chama katika misingi ya ubaguzi.. na ndiyo sababu leo au hata kesho, Mbowe hawezi kuitisha kikao cha Baraza Kuu la chama hicho, na akijaribu kufanya hivyo anatimuliwa", alisema Nape.

Nape pia hakumuweka kiporo Mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mwinyika, badala yake alimpasha kwenye mkutano huo kwamba, baada ya wananchi wa jimbo hilo kudanganyika na kumpa ubunge, sasa akae mkao wa kuondoka baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika 2014.

"Mnyika na Chadema yake tunawambia pango lao hapa jimbo la Ubungo  linamalizika rasmi mwaka 2014 na hatuma mpango wa kumuongezea, kilichobaki sasa ajiandae tu kuondoka taratibu", alisema Nape.

Alisema, Mnyika kama walivyo wabunge katika maeneo ambako wananchi walijaribu kuwachagua wapinzani, anachofanya yeye na Chama chake cha Chadema ni kupambana na kujenga misingi ya chama chao kuendelea kuwa kuishi na kamwe hawashughulikii matatizo ya wananchi.

"Na hili niliwaambia miaka mingi iliyopita, nilisema hapa ubungo kwamba mkimchagua mpinzani kazi yake itakuwa kutafuta njia za kuimarisha chama chake, na kamwe hataweza kujihusisha na masuala ya maendeleo yenu", alidai Nape na kuongeza;-

"Mnyika kama kweli una lengo la kuwatumikia wananchi wa Ubungo, umefika wakati wa kuacha sasa na mambo ya kudai kila mara hoja binafsi bungeni, sasa udai na hoja za wananchi, maana ukiendelea kudai hoja binafsi zaa wananchi utadai lini?"

Alisema, ni kutokana na wapinzani akiwemo Mnyika na chama chake cha Chadema, kutokwa mapovu midomoni kila kona ya nchi wakihangaika na Katiba mpya, tena wanachozungumzia zaidi serikalikali tatu na kusingizia kwamba ndiyo mahitaji ya wananchi huku wakijua wazi kwamba wanachohitaji wananchi kama wa Ubungo ni maji, elimu na afya na siyo idadi ya serikali.
 
Nape alisema hivi sasa wananchi wameshastukia vyama vya upinzani kwamba vipo kwa maslahi ya wachache ni si ya wananchi kama vinavyovyojinadi.

Alisema, miongoni mwa dalili za wananchi kuvistukia vyama cya upinzani, ni hali ilivyojitokeza wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alkizofanya akiambatana na Nape mwenyewe mikoani.

Nape alisema, katika ziara hizo hadi sasa wanachama  12, 430 walijiunga CCM huku karibu nusu yao wakiwa wametoka katika vyama vya upinzani vikiwemo Chadema na CUF.

Katika mkutano huo ulioandaliliwa na Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Nape alipokea wanachama wapya 480, wengi wao wakiwa wamehamia CCM kutoka katika vyama vya Chadema na CUF kwa nyakati tofauti.












  Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Ramadham Madabiba akimlaki Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape  Nnauye alipowasili katika Kata ya Kimara kwa ajili ya ziara ya siku moja kukagua uhai wa Chama katika kata hiyo, leo Juni 15, 2014.


 Vijana wa Chipukizi wa CCM, wakimvisha skafu Nape alipowasili katika kata hiyo kuanza ziara ya siku moja leo,Juni 15, 2014. Kushoto ni Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge


No comments:

Post a Comment

Popular Posts