Tuesday, June 24, 2014

WATOTO WALIA NA WANAWAKE KWA KUWATUPA.


Kichanga kilichotupwa Iringa Sokoni.
ito umetolewa kwa kina mama na wadada waishio mkoani Iringa wenye tabia ya kupenda kutupa watoto pindi wanapojifungua kuacha kabisa kufanya kitendo hicho kwani wanapoteza Taifa la kesho.
Hayo yalisemwa na Kamanda wa polisi mkoani hapa ACP Ramadhani Mungi alipokuwa akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake kuhusiana na taarifa za kutupwa kwa mtoto kachanga maeneo ya karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
“leo saa mbili asubuhi tulipokea taarifa ya kuwa kuna katoto kametupwa kwenye jalala lililopo karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya, mtoto huyo ni wa jinsia ya kiume na hata kitovu chake bado hakijakatwa uchunguzi unaonyesha inawezekana kuna mtu alitoa mimba na akaenda kuitupa pale hivyo bado tunaendelea na uchunguzi na endapo tukimpata mtu huyu aliyefanya kitendo hicho cha kikatili basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa, watu wanafanya kitendo hichi hawajui kuwa hawa wanaowatupa ndo Taifa la kesho huwezi jua huyo uliyemtupa angekuja kuwa nani mbeleni,” alisema Kamanda.
Tukio lingine, Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wanne kwa kosa la kumchoma moto mwanafunzi wa Chuo cha Ruco aliyetambulika kwa jina la Daniel Lema (25) mkazi wa Kihesa mkoani hapa.
Kamanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 20 June majira ya saa 9 usiku huko maeneo ya Kihesa.
“majira ya saa 9 usiku polisi walipigiwa simu na wasamalia wema kutoka kihesa kuwa kuna mtu amefungwa kamba mikononi na anatembea huku anawaka moto mwilini polisi wakaenda eneo la tukio na kumkuta mtu huyo ameanguka chini huku bado anawaka moto basi polisi wakamfungua na kumpeleka hospitali kwani alikuwa bado anathema” alisema kamanda Mungi.
Kamanda alisema taarifa zinaonyesha kuwa mwanafunzi huyo ambaye yuko mwaka wan ne katika kitivo cha sheria alikuwa katika bar ya Inbox iliyopo kihesa akiangalia mpira, wakati akirudi kwake maeneo ya Transfoma alipitia kwenye grory grocery iliyopo pembezoni mwa grory lodge na kukuta imefungwa ambapo mlinzi alipomuona alimuita lakini mwanafunzi huyo alikimbia baada ya kumuona mlinzi akiwa na kirungu.
“mwanafunzi Yule alikimbia na mlinzi alimkimbiza na kumkamata ambapo alimpeleka kwa meneja wa hiyo lodge hata hivyo meneja huyo aliwapigia walinzi wengine kutoka katika kampuni ya Juka Security ili waje kumchukua kijana huyo wampeleke kituo cha polisi walinzi walifika wakiwa watatu na kumchukua mtu huyo ambapo walipofika mbele wakamfunga mikono yake na kamba na kisha kummwagia mafuta na kumchoma moto kisha wakakimbia.” Alisema.
Hata hivyo watuhumiwa hao walitaka kutoroka mkoani hapa mara baada ya kutenda kitendo hicho ambapo walikamatwa kabla hawajafanikiwa kutoroka, watuhumiwa hao ni Musa Nganga (28), Costa Mganyuko (38), Steven Kalolo (24) pamoja na Samson Peter (24) wote wakazi wa Kihesa, pia kwa upande wa mgonjwa hali yake sio nzuri bado.
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA  NA CHRISSMPUZU.BLONGSPORT.COM -NJOMBE

No comments:

Post a Comment

Popular Posts