Friday, January 30, 2015

Sakata la Machinga kupigwa: Waziri Mkuu aahidi kumshughulikia Katibu Tarafa wa Kariakoo -Dar

 

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameagiza watendaji katika Manispaa na Jiji waliohusika kunyang’anya mali za wafanyabiashara mbalimbali kwa kisingizio cha kusafisha jiji na kugawana badala ya kupeleka kunakoruhusiwa kuchukuliwa hatua huku akiahidi kumshughulikia Katibu Tarafa wa Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
 
Aidha, amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kukaa na wafanyabiashara na kuangalia njia nzuri ya kufanya biashara ili kuondoa vurugu baina yao na vijana.
 
Pinda aliyasema hayo jana wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu alipojibu swali la Mbunge wa Ilala, Iddi Zungu (CCM) aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu wanamgambo wanaotumia nafasi ya kusafisha jiji kuwanyanyasa wafanyabiashara na kugawana mali zao huku tatizo kubwa likiwa kwa Katibu Tarafa wa Kariakoo.
 
Amesema yeye binafsi alitumiwa picha ya watendaji hao wakigawana mali walizowanyang’anya wafanyabiashara wakiwamo mama lishe, jambo ambalo ni kuwanyanyasa na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
 
Waziri Mkuu alikemea kitendo cha watendaji wa jiji na mikoa kutumia kusafisha jiji kunyanyasa wananchi.
 
Hivyo aliagiza wakuu wa wilaya na mikoa kukaa na wafanyabiashara ndogo na kupanga jinsi ya kuendesha biashara kistaarabu ikiwa ni pamoja na kupanga masoko ya jioni na Jumapili ili wafanye biashara muda mfupi na kuondoka.



Masheikh: Maaskofu msiingilie mchakato wa mahakama ya kadhi

 

TAASISI ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, imepinga tamko la maaskofu kuhusu kuzuia kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na kusema hatua hiyo ni sawa na kuingilia uhuru wa Bunge.
 
Kutokana na hali hiyo, wametaka maaskofu hao kupitia Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF), kuwaacha wabunge ili waweze kujadili muswada huo kwa uhuru bila kuwapo shinikizo katika suala hilo.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Sheikh Khamis Mataka, alisema tamko lililotolewa na maaskofu ni sawa na kuingilia madaraka ya Bunge na kutaka kuifanya Serikali ichukiwe kwa kuonekana imeshindwa kutimiza ahadi iliyoitoa kupitia Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
 
“Tamko lililotolewa na maaskofu halina hoja, hawana sababu za msingi za kuikataa Mahakama ya Kadhi, tunawasihi na kuwaomba maaskofu waachie uhuru wa wabunge hasa waumini wa dini ya Kikristo walioko bungeni, ili waweze kuujadili muswada huo bila shinikizo la kiimani.
 
“Mbinu zozote za kuwashawishi wabunge kiimani kutekeleza maazimio ya maaskofu chini ya Jukwaa la Wakristo Tanzania zitaleta udini na jaribio la kuligawa Bunge kiimani, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu,” alisema Sheikh Mataka.
 
Alisema wabunge wanapaswa kuzingatia viapo vyao vya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu bila kuathiriwa na shinikizo la kiimani lililotolewa na maaskofu.
 
Sheikh Mataka alisema taasisi inawakumbusha maaskofu kwamba Serikali ina vyombo vya uchunguzi na utafiti vyenye uwezo wa kubaini maeneo yanayovunja umoja wa kitaifa pamoja na mambo yanayokwenda kinyume na Katiba ya nchi ambapo wao si sehemu ya vyombo hivyo.
 
Alisema hofu ya kuwapo kwa Mahakama ya Kadhi bara ni bandia kwa kuwa kesi za Kiislamu zinazohusu masuala ya talaka, mirathi, wosia, wakfu na malezi ya watoto zinaamuliwa kwa sheria na taratibu za dini hiyo.
 
“Wanachoomba Waislamu ni kubadilishwa hakimu na kuondoa malalamiko na uonevu, hasa kwa wanawake ambapo lengo ni kuwapo mtu anayejua sheria na kuamua kuamua kesi hizo,” alisema.
 
Sheikh Mataka, ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata Taifa, alisema migogoro ya kiimani ya ndani, hasa kwa Waislamu isitumike kama kigezo cha kupinga mahakama hiyo kwa upande wa Tanzania Bara.
 
Alisema Mahakama ya Kadhi haihusiani na migogoro ya Wakristo, bali ni kuamua masuala ya Waislamu, huku akishangazwa na hatua ya maaskofu hao kupinga mchakato huo hali ya kuwa hauwahusu na wala haugusi imani yao.
 
“Tutashangaa iwapo Serikali itaamua kuuondoa bungeni muswada unaolenga kuitambua Mahakama ya Kadhi kwa kuitungia sheria maalumu. Je, iweje leo kuwa na maneno ya kila aina ya kushinikiza kuondolewa kwa muswada huo, hili hapana, wabunge waachwe waamue kwa utashi wao na sio kuingiliwa na makundi ya nje,” alisema.
 
Sheikh Mataka alisema kama Mahakama ya Kadhi ingekuwa na matatizo, ni wazi isingeanzishwa kwa upande wa Zanzibar ambako hadi sasa imekuwa ikitumika pasi na kuwapo na migogoro ya aina yoyote.
 
Juzi, viongozi wengine wa dini ya Kiislamu walipinga tamko lililotolewa na Jukwaa la Wakristo kuhusu sheria hiyo ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi na kudai kuwa matamko ya aina hiyo yanaweza kusababisha machafuko nchini.
 
Kauli hiyo zimekuja baada ya Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) kutoa waraka juzi, likipinga muswada unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni wakati wowote.
 
Kutokana na hali hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, aliwatoa hofu Wakristo wanaohofia mpango wa Serikali wa kuitambua kisheria Mahakama ya Kadhi nchini.
 
Alisema pamoja na kwamba mpango huo umeanza kulalamikiwa na baadhi ya makundi ya kidini, nia hiyo haina madhara kwa wananchi kwa kuwa Serikali haiwezi kupitisha sheria itakayowagawa watu.
  SOURCE MPEKUZI














‘Mume kanikimbia kisa nazaa sana’




 


 Sitasahau siku niliyokimbiwa na mume wangu baada ya kumzalia pacha kwa mara ya tatu mfululizo.” Hii ni kauli ya Salome Paul Mhando, mama wa watoto sita ambao ni pacha, aliowazaa kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miaka sita iliyopita, wakipishana miaka miwili miwili.
Salome, alitelekezwa nyumbani na mumewe huyo baada ya kujifungua pacha kwa mara ya tatu, huku wakiwa hawana sehemu maalumu ya kuishi, achilia mbali njaa iliyotokana na umaskini wa kipato.
Baada ya kutelekezwa, msamaria mwema alijitolea kumhifadhi katika shamba lake lililopo eneo la Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kabla ya kupata msaada wa nyumba ya kuishi.
Mama huyo anayekumbuka tukio hilo kwa uchungu, anasimulia kuwa mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Ali, alimtoroka saa saba mchana na kumwacha akiwa na pacha hao.
Anabainisha kuwa tukio hilo lilitokea baada ya familia hiyo kukaa na njaa kwa siku kadhaa kutokana na umaskini wa kipato.
“Siku hiyo, ambayo tarehe yake siikumbuki, mume wangu alirudi nyumbani akiwa tena hana chakula na kunieleza kuwa anaumwa. Nilipomwuuliza sasa tunafanyaje kuhusu chakula, alitoka nje,” anaeleza mama huyo na kuendelea:
“Nikaamua kumfuata na kuanza kumsema nikimdai chakula. Baadaye (mumewe) akaniuliza mbona unanisema? Mimi nikamjibu; naulizia masuala ya chakula, tunafanyaje leo? Akasema; basi niache naenda kukitafuta.”
Salome anaeleza kuwa kinyume na ahadi hiyo, tangu wakati huo alipoondoka hajaonekana nyumbani hadi sasa. “Niliamua kwenda kulala, lakini nikiwa na wasiwasi kuhusu usalama wake. Nikapatwa na hofu nikijiuliza; nini kimempata mwenzangu na kuanza kuwapigia simu ndugu zake ambao pia hawakupatikana.”
Salome anasema jitihada za kuwatafuta ndugu wa mumewe ziligonga mwamba na hadi sasa hana mawasiliano yoyote na familia hiyo ya mumewe.
Anaeleza kuwa kutokana na mumewe huyo kutorudi tena nyumbani, alilazimika kwenda kwenye vyombo vya habari kuomba msaada wa malezi ya watoto hao.
“Nilikwenda kwanza ITV ambako mbali na kunisaidia katika mahitaji ya msingi ya chakula, walinitangaza pia kwenye luninga kuwa ninahitaji msaada na tukio hilo ndilo limenisaidia kupata msaada wa kudumu.

Hali ikoje?
Salome anahusisha kutoroka nyumbani kwa mumewe na ugumu wa maisha unaoikabili familia hiyo.
“Nina watoto pacha sita; wawili wana umri wa miaka sita, wawili wengine wana umri wa miaka minne na wawili wa mwisho wana umri wa miezi 12. Nasikitika kukimbiwa na mume kwa sababu ya ugumu wa maisha, lakini zaidi akidai kuwa ninazaa sana. Maisha ni magumu na ninashukuru kwa misaada ninayoendelea kuipata kutoka kwa jamii, hasa kupatiwa msaada wa nyumba ya kuishi na wanangu,” anasema.
Akifafanua kuhusu ugumu wa maisha, Salome anasema ameshindwa hata kuwapeleka shule watoto wake wakubwa... “Hakuna anayesoma, wote bado wako nyumbani.”
Msaada wa nyumba
Hata hivyo, ugumu wa maisha wa Salome umeigusa Benki ya Covenant ya jijini Dar es Salaam, ambayo imejitokeza kumnunulia nyumba ya kuishi na watoto hao eneo la Mabwepande.
Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, Sabetha Mwambenja anasema mbali na msaada huo, anatamani kuona mume huyo aliyemtelekeza anapatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Anasema benki yake ilitambua mahitaji ya mama huyo kupitia vyombo vya habari na kuamua kumpa msaada wa kumnunulia nyumba ya kuishi yenye thamani ya Sh25 milioni, ambayo alikabidhiwa juzi.
“Tumemkabidhi, nyumba, tukamnunulia magodoro, vitanda vinne, mashuka na taa za sola na familia nzima tumeikatia bima ya afya itakayowawezesha kutibiwa katika hospitali yoyote inayotoa huduma kupitia bima hiyo,” anaeleza mkurugenzi huyo.
“Sisi hatuna kitengo wala idara inayojishughulisha na matatizo ya jamii, tumeguswa tu na tatizo la mama huyo aliyekimbiwa na mumewe sababu ya kumzalia pacha. Natoa wito kwa benki nyingine na wadau mbalimbali wa maendeleo kuguswa na matatizo ya jamii inayowazunguka na kusaidia pale inapowezekana,” anasema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Balozi Salome Sijanona anasema baada ya kuona mateso aliyokuwa akiyapata mwanamke huyo kwa kukosa makazi, chakula na mahitaji mengine ya kibinaadamu, waliona ni vyema kujitolea kumsaidia ikiwa ni moja ya kutimiza majukumu yake kwa jamii.

“Tumeguswa na mateso aliyokuwa akipata Salome Mhando, yeye pamoja na watoto wake, baada ya kutelekezwa na mumewe kwa kigezo ha kuzaa watoto pacha mfululizo. Tuliguswa na kuamua kujitolea kumnunulia nyumba ambayo ataimiliki mwenyewe,” anasema Balozi Sijaona na kuongeza:
“Nyumba hii tumemkabidhi pamoja na samani za ndani ambazo sasa zitamwezesha kuishi maisha ya amani na furaha akiwa kama wanawake wengine na kufurahi pamoja na watoto wake.”
Shukrani
“Ninaishukuru Benki ya Covenant kuniwezesha kumiliki nyumba yangu, ninawashukuru na ninaomba waendelee na moyo huo wa kuwasaidia kina mama wenye matatizo kama haya kwa sababu siko peke yangu,” alisema Salome na kuongeza:
“Kina mama tumekuwa na wakati mgumu katika ndoa zetu hususan katika masuala ya uzazi. Ninawashukuru watu wote ambao walijitolea kunisaidia chakula na nguo katika wakati wote nilipokuwa sina sehemu maalumu ya kukaa, hadi sasa ninamiliki nyumba yangu.”

SOURCE MWANANCHI






















Wednesday, January 28, 2015

PROFESA LIPUMBA AKAMATWA NA POLISI KWA NGUVU! TAARIFA KAMILI.



Ndugu zangu, hivi punde nimeongea na Maharagande Mbarala na Bonifasia Mapunda na wamenijulisha kuwa, Profesa Lipumba na Manaibu Wakurugenzi wawili wa Chama Cha Wananchi CUF (Shaweji Mketo na Abdul Kambaya), pamoja na walinzi wa Profesa Lipumba, wamekamatwa na polisi. Pia, nimeongea na mhe. Joram Bashange, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF, tayari yuko Central Police lakini hajaruhusiwa kuwaona viongozi. Mawakili wa CUF wanaelekea polisi pia.


KUMBUKIZI YA MWAKA 2001

Ukamataji huo uliotumia nguvu kubwa umetokea leo majira ya Mchana wilayani Temeke. Leo ni Januari 27 na ni siku yenye kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Wananchi CUF baada ya matukio ya mauaji yaliyofanyika tarehe na mwezi kama huu huko Zanzibar ambako wafuasi wa CUF zaidi ya 100 waliuawa kwa risasi na vyombo vya dola. Mauaji hayo yalifuatiwa na maandamano mbalimbali yakiwemo ya Dar Es Salaam yaliyoongozwa na Prof. Lipumba ambaye alivunjwa mkono, kuporwa saa yake ya thamani na polisi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

MAANDAMANO YA CUF KILA MWAKA:

Baada ya tukio hilo CUF imekuwa na utaratibu wa kuandamana kila mwaka (maandamano ya amani) ili kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya Januari 2001 na kuwaenzi waliopata ulemavu wa kudumu kutokana na kipigo cha vyombo vya dola. Mwaka jana 2014 mwezi kama huu Bendera za Chama cha Wananchi CUF zilipepea nusu mlingoti na pia maandamano yalifanywa maeneo kadhaa ya nchi na vyombo vya dola viliyalinda.

Mwaka huu nimeambiwa kuwa CUF ililijulisha jeshi la polisi juu ya maandamano ya leo kupitia barua ya Alhamisi, Tarehe 22 Januari 2014. Baada ya CUF kuandika barua hiyo, maandalizi ya maandamano na mkutano wa hadhara yaliendelea, ikiwemo kufanya matangazo kwenye wilaya za DSM, kukodi vifaa mbalimbali na hata kulipia matangazo LIVE kwenye redio kadhaa ili hotuba za viongozi ziweze kurushwa. Jeshi la polisi lilipokea barua hiyo tokea tarehe 22 Januari na likakaa kimya muda wote huo.

ZUIO LA POLISI:

Leo tarehe 27 Januari, maandamano yalipangwa kuanza saa 8 mchana kuanzia Temeke Mwisho kwenda hadi viwanja vya MBAGALA ZAKIEM ambako mkutano wa hadhara ungefanyika kuanzia saa 10.00 - 12.00 jioni. Cha ajabu ni kuwa, asubuhi ya leo ndipo Jeshi la Polisi limepeleka barua kwenye Ofisi Kuu za CUF Buguruni KUZUIA MAANDAMANO na MKUTANO WA HADHARA.

Barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar Es Salaam na Pwani inaeleza sababu kadhaa za zuio hilo:
1. Kwamba, maandamano ya CUF ya Mwezi Januari 2001 yaliyofanya vyombo vya dola vitumie nguvu na kuua raia hayakuwa halali na hivyo kuadhimisha siku hiyo mwaka huu ni haramu na kunaweza kuhatarisha amani ya nchi.
2. Kwamba, Taarifa za kiintelijensia zinaonesha ati kuna watu wamepanga kufanya vurugu katika maandamano na mkutano huo.
3. Kwamba, kuna vitisho vya UGAIDI katika nchi yetu na hivyo maandamano hayo na mkutano huo vinaweza kuleta madhara ya magaidi kupenya na kutekeleza azma zao mbaya.
4. Sababu nyingine za kipuuzi, dhaifu na zisizo na maana.
Baada ya kupokea barua hiyo na kwa sababu wananchi na wapenzi wa CUF walikwishajikusanya kwa maelfu kwa ajili ya maandamano, ilimpasa Profesa Lipumba na viongozi waandamizi wa chama waweze kwenda hadi Temeke Mwisho ili kuahirisha maandamano hayo.

TEMEKE MWISHO:

Majira ya mchana leo, Profesa Lipumba aliongea na wanachama na wapenzi wa CUF waliojazana Temeke Mwisho karibu na Ofisi za CUF Wilaya na akaahirisha maandamano na mkutano (Usalama wa Taifa walikuwepo, Polisi walikuwepo kwa mamia na vyombo vya habari vilikuwepo). Baada ya kufanikiwa kuwatawanya wafuasi waliokuwa Temeke Mwisho, Profesa akajulishwa kuwa kule uwanjani Zakiem tayari kuna maelfu ya wafuasi, ikampasa yeye na viongozi waandamizi waingie katika magari na kuanza safari kwenda Zakiem kwa lengo la kuwatawanya wafuasi kwa amani kama alivyofanya kwa wale waliokusanyika Temeke Mwisho. Hapakuwa na wafuasi wa chama waliomfuata.

KUELEKEA MBAGALA ZAKIEM:

Wakiwa katika Magari yao na katika safari ya kwenda Mbagala Zakiem, wakazuiwa na magari zaidi ya 10 ya polisi walio tayari kwa mapambano. Profesa na viongozi wakawajulisha Polisi azma yao ya kwenda kutawanya wafuasi walioko Zakiem, baada ya mvutano mfupi Polisi hao waliwaruhusu waende Zakiem. Safari ya magari machache ikaendelea, bila wafuasi wanaotembea kwa miguu.

Walipofika mbele (Mtoni Mtongani - Round about) wakakuta BLOCK ya pili ya mamia ya Polisi wenye magari na silaha. Hawa nao wakawazuia wasiende ZAKIEM, wakati bado Profesa anawaelewesha, mabomu yakaanza kupigwa na viongozi kusambaratishwa kwa nguvu mno kama vile kulikuwa na jambo kubwa. Profesa amebebwa mzobemzobe akipigwa virungu na kutupwa kwenye DIFENDA ya polisi yeye, wakurugenzi wake na walinzi wake. Hivi sasa tuongeavyo wako CENTRAL POLICE na mie nilitoka tu kidogo Darasani ili kupiga simu na kusimuliwa tukio zima.

 
 
CHA KUSHANGAZA:

Wakati polisi wanazuia maandamano ya CUF kwa nguvu kubwa kiasi hiki, wanawapiga na kuwajeruhi viongozi wasio na hatia na ambao wamejishusha na kuahirisha maandamano na mkutano wao, Polisi haohao kila siku tunaona wanasimamia maandamano na mikutano ya Mwigulu Nchemba, Abdulrahman Kinana, Nape Nauye na viongozi chungu mbovu wa CCM.

Hata katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yanayotarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma, nimejulishwa kuwa kuna maandamano yamepangwa yakihusisha wana CCM mbalimbali katika wilaya za jirani ili kusheherekea sikukuu yao na kwamba Polisi watayalinda maandamano hayo ya CCM.


MASWALI YA KUJIULIZA:

Je, hizi taarifa za Kiintelijensia zinafanya kazi kwa mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu? Je, hao Magaidi wao wanavamia na kulipua mikutano ya vyama vya upinzani tu? Magaidi gani hawa ambao hawaendi kuvamia wezi wa fedha za umma ati wanakwenda kuvamia viongozi waadilifu wanaopigania haki sawa kwa wote na mabadiliko makubwa katika nchi yetu? Tunadhani matendo haya ya serikali na vyombo vyake dhidi ya vyama vya upinzani yanajenga mustakabali wa taifa? Yanajenga amani na upendo miongoni mwetu? Au yanazidisha chuki na uhasama na mgawanyiko/mpasuko katika taifa?

Kwa nini mamia ya askari wanaokwenda kupiga na kujeruhi viongozi wenye nia njema yasitumike kwenda kusaka majambazi walioua askari wetu pale Ikwiriri Rufiji? Kwa nini mamia ya askari hao yasiwasake majambazi walioteka mabasi ya abiria mkoani Arusha majuzi? Kwa nini mamia ya Askari hao yasijielekeze kuwasaka wauaji wa Albino na wazee wenye macho mekundu Shinyanga?

Kwa nini mamia ya askari hao wasipelekwe kuwasaka magaidi ambao tumegundua watakuja kutuvamia? Na mbona maguvu hayo ya polisi yasielekezwe kuwasaka wala rushwa wakubwa, wafadhili na wamiliki wa mitandao ya kuuza madawa ya kulevya, wezi wa fedha za umma na waharibifu wakuu wa Taifa hili?
Mbona taifa hili linaendeshwa kipuuzi namna hii? Mbona nchi yetu inapelekwa mbele kama vile kuwa Chama Cha Upinzani ni dhambi dhidi ya watawala wezi na mafisadi? Kwa nini basi CCM hao hao wakapigia debe kuanzishwe vyama vingi mwaka 1992? Sasa wanaogopa na kuweweseka kwa lipi?

(UKIONA SERIKALI INAOGOPA MAANDAMANO YA AMANI NA MKUTANO WA CHAMA KIMOJA TU HADI KUPIGA NA KUKAMATA VIONGOZI, JUA KWAMBA SERIKALI HIYO HAINA SIKU NYINGI MADARAKANI).

"Time will determine and judge each of us".


Julius Mtatiro,
27 Januari 2015,
Masomoni.

TAARIFA YA POLISI



Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,CP Suleiman Kova--Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG yenye namba BA172288  na risasi kumi na tatu wakati wa  mapambano makali ya ana kwa ana kati ya majambazi na Jeshi la Polisi.  Aidha katika tukio hilo majambazi wawili waliuawa  kwa risasi wak ati wakijaribu kuwadhuru askari.
Tukio hilo lilitokea eneo la Kariakoo mtaa wa Mkunguni na Livingstone saa 3.00hrs usiku. Wakati wa tukio hilo umeme ulikuwa hakuna na mlalamikaji alikuwa anatumia taa za kawaida.  Mara baada ya kuanza tukio hilo la uporaji wasamaria wema walijulisha Jeshi la Polisi ndipo kikosi maalum cha kupambana na majambazi (ant robbery squared) kilipofika kwa haraka katika eneo la tukio tayari kwa mapambano.
Majambazi hao walistuka na kuanza kuwarushia risasi askari waliokuwa katika gari la Polisi na ndipo sasa kukawa na mapambano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili kwa kutumia silaha na kurushiana risasi. Hatimaye majambazi wawili waliuawa mmoja anayejulikana kwa jina la ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO, Miaka 24, raia wa Kenya aliyepatikana na Pass ya kusafiria yenye nambari A1688495 iliyotolewa katika mji wa KISUMU nchini Kenya. Jambazi mwingine aliyeuawa ametambuliwa kwa jina la YUSSUPH S/O HAMIS @ TWALIB, Miaka 46, Mshiraz, Mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Majambazi wengine waliotoroka baada ya tukio hilo wanaendelea kutafutwa na tunaomba raia wema waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi ili wapatikane.
Pamoja na kuuawa kwa majambazi hawa na kukamatwa kwa silaha, pia zimekamatwa pikipiki mbili moja ni SUNLG yenye namba za usajili T249 CMC, rangi nyekundu. Nyingine ni aina ya BOXER yenye namba za usajili MC350 AM rangi nyeusi ambazo zote zilitumiwa na majambazi hao katika tukio. Aidha, Jambazi ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO  aliyeuawa amekutwa na simu ya mkononi aina ya TECNO.
MAJAMBAZI WENGINE TISA SUGU WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM
Katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam dhidi ya ujambazi wa kutumia silaha Jeshi la Polisi limekamata majambazi tisa wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.
Oparesheni kali bado inaendelea jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha kwamba majambazi wote wanaotumia silaha pamoja na makosa mengine ambayo ni kero katika jamii yanashughulikiwa kikamilifu. Pamoja na mafanikio hayo tunawashukuru raia wema kutokana na juhudi zao za kutoa taarifa mapema zenye kuwa na mafanikio ya kulifanya jiji la Dar es Salaam liendelee kuwa shwari.
S. H. KOVAKAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUMDAR ES SALAAM


Saturday, January 24, 2015

Jeshi lawataka watu watambue ujenzi maeneo ya jeshi nikinyume na sheria.




Jeshi la wananchi limewataka watu wachache wanaovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi ya kijeshi ikiwemo mafunzo zana hatari za kijeshi na mabomu katika eneo la Tondoroni na Kiluvya 'B' kutambua kufanya hivyo ni kosa kisheria na litaendelea kuwaondoa katika maeneo hayo kutokana na kukiuka taratibu na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa jeshi la wananchi meja Joseph Masanja amekanusha madai ya wananchi wa Tondoroni la kuibiwa mali zao na kusisitiza serikali ilishawalipa wananchi hao fidia mara mbili kufuatia tathimini iliyofanyika mwaka 1987/88 na ya mwaka 1992/93 ambapo malipo yao yalifanyika juni 11 mwaka 2003 na 2006 na wananchi wengine walilipwa mwaka 2012 kutokana kesi madai na 144/1996.
 
Aidha baadhi ya viongozi wa wanakijiji cha Tondoroni wamefika katika studio za ITV na Redio One wakiwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo barua kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kisarawe na wizara ya ardhi zinazoonyesha kijiji cha Tondoroni kilipata hati ya usajili wa kudumu namba 539 ya mwaka 1993, na kusisitiza serikali iliwalipa wananchi 145 huku wananchi 1404 mpaka sasa hawajalipwa.
 
Mgogoro eneo la Tondoroni lililopo katika wilaya ya Kisarawe, kati ya jeshi la wananchi na wanakijiji umeibuka baada ya serikali kuchukua maeneo mbalimbali ikiwemo kijiji cha Mloganzila, Kiluvya B, na kijiji cha Tondoroni lenye hekta elfu 4197 kwa ajili ya matumizi ya jeshi ambapo yalipimwa kwa mujibu wa sheria.
















Madereva wa daladala wamefunga barabara mkoani Mwanza




Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza leo wamelazimika kutembea kwa miguu, kufuatia madereva wa daladala na taksi kufunga barabara kwa zaidi ya saa tano ili kushinikiza uongozi wa jiji la Mwanza kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga waliovamia eneo la stendi ya Tanganyika na kujigawia maeneo ya kufanyia biashara kinyemela.
Barabara zote za kuingia katikati ya jiji la Mwanza zilifungwa toka alfajiri baada ya madereva wa hiace na taksi kupaki magari yao katikakati ya barabara na kuyazima hali ambayo imesababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wengine wa barabara, huku baadhi ya askari polisi wenye mbwa wakifanya doria kwa miguu na wengine kwa kutumia defender ili kukabiliana na vurugu ambazo zingeweza kujitokeza.
 
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wamekerwa na kitendo hicho cha kufunga barabara na kusababisha kutembea kwa miguu huku wakiwa na mizigo, na kushauri kufanyika kwa mazungumzo ili kufikia muafaka kuhusu eneo hilo la stendi ya mabasi ya Tanganyika ambalo kabla ya machinga kulivamia na kujigawia maeneo ya kufanyia biashara zao lilikuwa likitumika kwa ajili ya maegesho ya magari ya mizgo aina ya canter na bodaboda.
 
Kufuati hali hiyo, mkurugenzi wa jiji la Mwanza Halifa Hassan Hida amewaagiza machinga waliovamia eneo la stendi ya Tanganyika pamoja na stendi ya daladala za Mwaloni- Kirumba, kupisha eneo hilo kwa muda hadi pale watakapotangaziwa rasmi.





Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wauawa Dar es Salaam.

 
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za moto wameuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya watu hao kujaribu kuwakimbia askari polisi katika mtaa wa sikukuu- Ilala jijini Dar es salaam.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleimani Konda amesema majambazi hao walikuwa na silaha moja aina ya Smg na risasi 6 na baada ya kugundua  kufuatiliwa na polisi walifyatua risasi kujihami ambapo mbali na watu hao kuuwawa na wananchi jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja aliyeokolewa na polisi katika mapigano hayo akiwa na hali mbaya na amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili chini ya ulinzi mkali wa polisi kwa mahojiano zaidi.
Aidha kamishna Kova amebaini kufuatia msako mkali unaofanywa na jeshi la polisi katika jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 113 kwa makosa mbalimbali,silaha za moto 6,sare za jeshi, cd mbili zenye mafunzo ya kigaidi pamoja na magari mawili ya wizi ambapo amesema msako huo bado unaendelea ili kumaliza kabisa matukio ya uhalifu hapa nchini.

Natamani kuonana na Rais Kikwete nimweleze ukweli

 

Baada ya kufanikisha lengo la kuonana na familia zaidi ya 30 za Watanzania waliofungwa katika magereza mbalimbali Hong Kong, Padri wa Kanisa Katoliki, John Wootherspoon aliyeleta ujumbe wa watu hao amesema anatamani kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili amweleze hali ya biashara ya dawa za kulevya na manung’uniko ya wafungwa hao.
 
“Nilichoona ni kuwa Tanzania imetawaliwa na rushwa, vijana wengi wanaingia katika dawa za kulevya kwa sababu ya umaskini. Umaskini wenyewe naona kuwa kiini chake ni rushwa. Natamani nizungumze naye iwapo atakubali,” alisema Padri Wootherspoon.
 
Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Wootherspoon, raia wa Australia na padri wa parokia ya Notre Dame, Shing Tak Street, Hong Kong, Kowloon, anasema anatamani azungumze na Rais Kikwete ili amweleze hali halisi ya biashara ya dawa za kulevya kwani kukutana kwake na wafungwa wa Kitanzania mjini Hong Kong kumempa fursa ya kujua mengi.
 
Katika ziara yake ya hapa nchini ya kutembelea familia za wafungwa hao wa dawa za kulevya kwenye magereza ya Hong Kong, Macau na Guang Zhou, Padri Wootherspoon pia alionana na kamishna wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa.
 
Kadhalika Wootherspoon alisema kati ya mengi aliyonayo, anatamani kumwambia Rais afanye kila liwezekanalo ili kuhakikisha Watanzania hao wanarudishwa nchini kama Nigeria ilivyofanikiwa.
 
“Hata kitengo cha Haki za Binadamu cha Umoja wa Mataifa kinaeleza wazi kuwa, mfungwa ana haki ya kuhukumiwa katika nchi yake. Lakini nashangaa kuona kwa nini suala hili limekuwa gumu kufanikiwa hapa,” alisema.
 
Akihutubia taifa katika sherehe za kilele cha mbio za Mwenge mwaka jana mkoani Tabora, Rais Kikwete alisema serikali imefanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na uingizwaji wa dawa hizo, hali aliyosema imesaidia kuwakata wasafirishaji wanaotumia njia mbalimbali kusafirisha dawa hizo.


Wootherspoon alisema anaamini kuwa Rais Kikwete ni mkarimu, mwelewa na amejaribu kulivalia njuga suala hili la dawa za kulevya, lakini imekuwa vigumu kwake kufanikisha kutokana na mazingira.
 
“Nia yangu kubwa ni kuwafanya vijana wasiende tena nchi za mashariki ya mbali. Huko kuna hatari ya kunyongwa, si kuzuri. Wasikubali pia kutumiwa na hawa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya. Ombi langu ni kutaka waache kufanya biashara hiyo,” alisisitiza.
 
Tatizo bado kubwa
Wafungwa hao ambao wengi wanatumikia kifungo cha maisha na wengine kati ya miaka 20 hadi 25, wanalalamika kuwa matajiri wanaowatuma hawachukuliwi hatua za kisheria, licha ya wao kuwataja kwa majina na kuweka wazi ushahidi kwa viongozi wa Serikali wanaowatembelea magerezani, China.
 
Hata hivyo, Nzowa alisema kuwa tayari magwiji wa dawa za kulevya waliokuwa wanaipa serikali wakati mgumu, wameshatiwa nguvuni na kilichobaki ni hukumu tu.
 
Bila ya kuwataja vigogo hao, Kamishna Nzowa anasema kesi zao tayari zimeshafikishwa mahakamani na kuwa wengi walishikwa na vithibiti, hali inayofanya kesi zao kuwa nyepesi kukamilika.
 
"Tulifanya kila tuwezalo tukawamata magwiji wenyewe, ambao wanawatumia vijana kubeba dawa hizo. Kwa sasa asilimia kubwa tayari tumewakamata lakini bado kazi haijamalizika kama tunavyodhani. Huu mtandao ni mkubwa,” alisema.











Mimi ni Msafi: Profesa Muhongo

 
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano aliouitisha leo hii ofisini kwake, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Uwaziri baada ya kutuhumiwa kuwa yeye ndiye tatizo linaloendeleza malumbano baina ya Serikali na Bunge kuhusu fedha za akaunti ya Tegera Escrow.
 
“Nimejiuzulu bila kushinikizwa na mtu yeyote. Mimi ndiyo nitamaliza mjadala huu wa sakata la escrow, nchi ina mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kujadiliwa lakini watu wamekazana na escrow.
 
 "Nimemuandikia Rais barua rasmi ya kujiuzulu wadhifa wangu. Nimemuomba rais kuachia ngazi ili niipe nafasi serikali yangu kufanya kazi... Nitaendelea kuwa mbunge na mshauri. 
 
“Sidhani kwamba cheo cha mtu mmoja cha uwaziri ni muhimu kuliko hawa masikini ambao wanateseka mchana na usiku.Kwa hiyo nimesema ni sehemu ya suluhisho.
 
“Nimemuomba Mheshiwa Rais kwamba tafadhali naomba niachane na nafasi ya Uwaziri kusudi taifa lisengo mbele.Hakuna sababu ya kuendelea kulumbana, tunapoteza muda na mali zetu, tunapoteza nguvu zetu wakati ambapo malumbano hayana mwisho” alisema Profesa Muhongo.

Kujiuzulu kwake kumetokana na shutuma zilizomwandama za jinsi alivyoshughulikia suala hilo na Wizara yake ikiwa ni pamoja na uchowaji wa fedha kiasi cha shilingi bilioni 306/= kutoka kwenye akaunti hiyo.

Prof. Muhongo amezidi kusisitiza kuwa yeye hakuhusika na chochote kile katika hilo:
"Sikuwahi kuchukua rushwa na sihongeki... Mimi nashangaa leo watu kila kona wananiona mimi ni mwizi, yaani kama mimi ndiyo nimechukua mabilioni ya escrow wakati ukweli upo wazi.
 
"Wakati Wizara ya Nisharti inaingia kwenye mkataba huo mimi sikuwepo kwenye nafasi ya Uwaziri, lakini leo watu bado wananiona mimi ni mwizi. 
 
"Acha niaachie ngazi nafasi hii ya uwaziri kwani imekuwa ni shida sana, mimi ni mtu msomi nimepata tuzo sehemu mbalimbali duniani, nasifika kwa kutoa ushahuri wenye tija, lakini leo naonekana mwizi, wakati historia yangu inaonesha mimi ni mtu msafi sina doa na wala sijawai hata kumwibia mtu, lakini watu wananiona mimi mwizi” , Alisema Muhongo na kuendelea kueleza kuwa, baada ya kutafakari sana aligundua kwamba amenyooshewa kidole yeye binfasi, ni kwa sababu hiyo ameamua kujiuzulu kwa kuzitaja sababu mbili, kuwa:-


  1. Ana matumaini kuwa kuachia kwake ngazi, mjadala wa ‘escrow’ utakuwa umefikia tamati.
  2. Anafanya hivyo ili kukiweka safi Chama Cha Mapinduzi ambacho kimekuwa kinanyooshewa kidole.
"Uamuzi huu nimeufanya kwa sababu zifuatazo kwanza nataka Serikali ibaki kushughulikia matatizo ya wananchi badala ya Serikali kukaa inashughulikia suala la Escrow. 

"Ninaachia ngazi za Uwaziri kwa sababu ninataka kamati za CCM ziendelee kutatua kero za wananchi kuliko kukaa kwenye vikao masaa mengi wanazungumzia masuala ya Escrow. 
 
"Vilevile naachia ngazi kwa sababu kule Bungeni mimi nataka niwe mbunge wa kawaida, na si ubunge wa kawaida tu lakini nafasi ya Uwaziri nitawaachia wengine. Hii nayo itatoa fursa kwa bunge letu kutumia muda wake vizuri na rasilimali zake vizuri kwa manufaa ya wananchi. 
 
"Naachia nafasi hii kwa sababu Watanzania wamechoka, Escrow haina tija kuijadili kila siku asubuhi mapaka jioni badala ya umasikini wao, hebu tuwaachie wananchi kuliko kuendelea na malumbano yasiyokuwa na mwisho."
 
Amesema kwa namna moja ama nyingine, sakata hilo si tu kuwa limekuwa likikigharimu Chama bali pia baada ya kutafakari aliwasiliana na mkuu wake wa kazi, Rais Jakaya Kikwete na familia yake na watu wake wa karibu kuwataarifu kuwa anajiuzulu.

Muhongo amesema kuwa sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne:-
  • Mvutano wa kibiashara
  • Mvutano wa kisiasa
  • Mvutano wa uongozi na madaraka
  • Ubinafsi.
Amesema akiwa katika nafasi hiyo, aliweza kufanya mengi ikiwa ni pamoja na kuwapeleka vijana wengi nje kusomea masuala ya gesi, nishati na sayansi kwa ujumla kwani ili Taifa liendelee, linahitaji kuwa na wataalamu katika sekta hiyo muhimu.

“Nimeshirikiana na Makamu wa Rais, nimeshirikiana na Waziri Mkuu na kusaidia kuwaletea wananchi maendeleo hadi leo tukaweza kusimama na kusema asilimia 40 ya Watanzania wanatumia umeme”

Alilishukuru Baraza la Mawaziri, Bunge, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ushirikiana wao walioutoa kwake na kueleza kuwa yeye daima atawatumikia wananchi.

Waziri Muhongo aliteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini mwezi Mei mwaka 2012 baada ya kuteuliwa kuwa mbunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Jakaya Kikwete.

Muhongo anakuwa mtumishi wa tatu kuachia nafasi yake kutokana na kuhusishwa na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fredrick Werema kujiuzulu wadhifa huo huku Rais akitangaza kumvua Uwaziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka. Pia baadhi ya watumishi wa Serikali kutoka taasisi mbalimbali wakifikishwa mahakamani kutokana na tuhuma zinazohusishwa na sakata hilo.

Ameahidi kuwaeleza Watanzania ukweli wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow na kujiuzuru kwake ili kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa Tanzania na watu wake.

Breaking News: Rais Kikwete afanya Mabadiliko katika Baraza la Mawaziri... Sitta, Mwakyembe wabadilishiwa Wizara!







 

Waziri wa Nishati na Madini mpya, George Simbachawene.
*****
Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo mchana, Rais Jakaya Kikwete ametangaza marekebisho ya Baraza lake la Mawaziri.

Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao leo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais,  Ombeni Sefue alitaja mawaziri hao wapya ambao wameapishwa leo jioni na wizara zao kwenye mabano kuwa ni: George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).

Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).

Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini). 

Friday, January 23, 2015

CCM yarejesha amani Sudan Kusini....Makundi hasimu yaafikiana, Yatia Saini mkataba wa Amani jijini Arusha

Baada ya miezi mitano ya mazungumzo ya kurejesha amani Sudan Kusini yaliyoratibiwa na chama tawala, CCM, hatimaye Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na hasimu wake, Riek Machar wamesaini makubaliano ya kusitisha mapigano, yaliyoibuka tangu mwaka 2011.
 
Kutokana na machafuko hayo, zaidi ya raia 20,000 wa Sudan Kusini, wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya milioni moja wakikosa makazi.
 
Walisaini makubaliano hayo juzi usiku jijini Arusha, huku marais wa ndani na nje ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, wakishuhudia.
 
Wengine walioshuhudia makubaliano hayo ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa , Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Salva Kiir, Riek Machar na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal.
 
Kutokana na makubaliano hayo ya kihistoria yenye lengo la kurejesha amani ya taifa hilo changa, lililojitenga kutoka Jamhuri ya Sudan yenye makao yake makuu Khartoum, Rais Kikwete aliwapongeza Salva Kiir, Machar na kundi jingine la tatu ambalo baadhi ya viongozi walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini humo na kuwaambia kuwa makubaliano hayo zaidi ya 40, wahakikishe wanayazingatia ili amani na upendo vitawale nchini mwao.
 
Makubaliano hayo ambayo awali yalikuwa yasainiwe juzi saa 8:00 mchana, yalisainiwa saa 2:30 baada ya makubaliano rasmi.
 
Baadhi ya makubaliano hayo ni pamoja na kufanyia marekebisho katiba ya chama tawala nchini humo cha SPLM, kupunguza madaraka ya Rais, kuongeza idadi ya wajumbe katika kamati kuu ya chama, kukubali kuwajibika wote kwa yote yaliyotokea na kuwaomba msamaha wananchi wa Sudan Kusini kwa kuwasababishia machafuko na vita.
 
Mengine ni haki ya kila mwanachama kugombea uongozi, kuleta mabadiliko ya kidemokrasia katika chama, utawala bora na uwazi katika chama na kutumia makubaliano ya Arusha kuharakisha mazungumzo ya Addis Ababa (Inter Governmental Authority Development (IGAD).
 
Mara baada ya maazimio hayo kusomwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, aliwaomba kutimiza kwa dhati maazimio waliyojiwekea na kuyatekeleza kwa faida ya nchi yao.
 
Rais Kikwete aliyeungana na marais wenzake na viongozi wengine wa kimataifa, kushuhudia tukio la kihistoria la utiaji saini ya makubaliano ya amani na kusitisha mapigano katika nchi mpya ya Sudan Kusini; alisema “Nawapongeza kwa hatua hii mliyofikia mlipokuja kuniomba kuwasaidia kutatua tatizo lenu la vita.
 
 “Nilijiuliza maswali mengi, lakini nashukuru nimeshirikiana na wenzangu wa CCM kuhakikisha amani Sudan ya Kusini inapatikana kupitia chama, hivyo nawasihi kuhakikisha mnasimamia haya mliyoyasaini ili kuleta maendeleo kwa nchi sambamba na kuleta amani na furaha ndani ya nchi yenu”.
 
Kikwete alisema kila kiongozi kabla ya kufanya kitu ni lazima atafakari mara mbili jambo lolote analotaka kufanya, kuwa lina faida kwa wananchi wa nchi hiyo au la.
 
“Lakini mkiyatekeleza makubaliano haya, kila kitu kwenu kitakuwa rahisi na hakuna litakaloshindikana kwenu na kuna usemi wa Kiswahili usemao kuzaa si kazi, kazi kulea mwana , hivyo nawasihi mkayasimamie haya,” alisema.
 
Rais Kenyatta aliwapongeza kwa kukubali kusaini makubaliano hayo na kuwakaribisha kwake pale watakapohitaji msaada wowote kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya nchi hiyo.
 
Kwa upande wa Rais Museveni, aliungana na wenzake kuwapongeza kwa kufikia hatua hiyo na kusema nchi hiyo ni ndugu wa karibu na Uganda na hivyo imekuwa furaha kuona sasa wanakwenda kutulia bila mapigano.
 
“Hata hivyo napenda kuwapongeza hawa wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukubali kuratibu mazungumzo haya hadi kufikia hapa na nasema ni vyema ukiona ndugu yako amekosea, Waswahili husema hatuwezi kuambizana ukweli kitu ambacho kinatugharimu,” alisema.
 
Baada ya hatuba hizo za wosia kwa wapinzani hao ndani ya chama kimoja, Rais Salva Kiir na mpinzani wake, Riek Machar ambaye ndiye aliyekuwa Makamu wa Rais kabla ya mtafaruku, walionekana wenye furaha muda wote na kupongezana kwa kupeana mikono mara kwa mara, huku wakishangiliwa na wapambe wao waliofurika ndani ya ukumbi wa Ngurudoto, jijini Arusha.
 
Wapinzani hao wote kwa pamoja waliahidi kutimiza kwa vitendo makubaliano hayo na kupeana ushirikiano katika mambo yote na kuwashukuru wote waliohusika kusuluhisha ugomvi huo hadi kufikia hatua hiyo.
 
Alikuwepo pia Rebecca Nyandeng De Mabior, mjane wa kiongozi wa kwanza wa chama cha SPLM, John Garang, ambaye ndiye aliyeongoza harakati za kupigania uhuru, kuelekea kujitenga kwa nchi hiyo, kutoka kwa iliyokuwa Jamhuri ya Sudan.
 
Mazungumzo ya awali ya vikundi vinavyozozana katika chama cha SPLM yaliongozwa na ujumbe mzito wa ngazi ya juu wa CCM ili kutafuta suluhu ya mgogoro ndani ya chama hicho, kinachotawala nchini Sudan Kusini.
 
Ujumbe huo uliongozwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na Kinana.
 
Kwa upande wa SPLM, mazungumzo hayo yaliongozwa na Taban Deng Gai, Daniel Awet Akot, na Deng Alor Kuol.
 
Miongoni mwa makundi hayo ni kutoka chama cha SPLM, kundi kutoka kwa wafungwa wa kisiasa, pamoja na kundi lililojitenga kutoka chama cha SPLM.
 
Chama hicho kiligawanyika makundi matatu na kusababisha jeshi kwa upande wake, kumeguka katika makundi hayo na kusababisha wananchi nao kugawanyika katika makundi hayo matatu .
 
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Umoja wa Afrika (AU), Norway, Misri, Umoja wa Mataifa (UN) na Ethiopia.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Thursday, January 22, 2015

WATUMISHI WA RAS NJOMBE WAPATA MAFUNZO YA UKIMWI MAHALA PA KAZI
















Hali ni Tete kwa Vigogo Escrow.......Wengine waliopata Mgawo kupelekwa Mahakamani leo, Ngeleja, Lissu watunishiana misuli

 
HALI inazidi kuwa tete kwa vigogo kadhaa wa Serikali juu ya sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya kuwapo taarifa kuwa wengi watafikishwa mahakamani.
 
Iwapo leo vigogo ambao majina yao yamekuwa yakitajwa tangu juzi watafikishwa mahakamani, wataongeza idadi baada ya juzi watumishi wawili wa Serikali kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
 
Jana asubuhi baadhi ya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), walionekana wakiranda katika viwanja vya mahakama hiyo.
 
Mmoja wa maofisa hao alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya kuwapo kwao eneo hilo, alisema wapo kwenye maandalizi ya kuwapandisha kizimbani vigogo wengine.
 
Hata hivyo, ilipotimu saa 7 za mchana, ofisa huyo alisema kuna baadhi ya nyaraka za watuhumiwa zilikuwa zinarekebishwa kabla ya kufika mahakamani.
 
Baadhi ya watuhumiwa ambao jana walipigiwa simu na kutakiwa kufika Takukuru, inaelezwa hawakupokea simu kwa hofu ya kuburuzwa mahakamani. Hadi tunakwenda mitamboni harakati hizo zilikuwa zimekwama.
 
Watumishi waliofikishwa mahakamani juzi ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Majunangoma ambaye alisomewa mashtaka ya kupokea rushwa ya Sh milioni 323.4 zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta Escrow kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeering James Rugemalila.
 
Kabla ya Rugonzibwa kufanya kazi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikuwa mwanasheria wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (RITA), ambako alihusika na mufilisi wa Kampuni ya IPTL.
 
Rugonzibwa, aliichunguza IPTL, alisimamia watumishi wake wakati kampuni hiyo iko katika mufilisi na alisimamia mashauri mbalimbali yanayoihusu.
 
Mshitakiwa mwingine, ni Theophillo Bwakea ambaye alifikishwa mahakamani kwa kosa la kupokea rushwa ya Sh milioni 161.7 kutoka kwa Rugemalila.
 
Bwakea ni Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), na kabla ya kufanya kazi huko, alikuwa Wizara ya Nishati na Madini, kitengo cha kusimamia umeme, ambako anadaiwa alishiriki kutunga sera ya kampuni binafsi kuuza umeme Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na ilipoanza kutumika, Kampuni ya kufua umeme ya IPTL ilikuwa ya kwanza kupata zabuni. 
 
Ngeleja agoma
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja, amewagomea wajumbe wa kamati hiyo waliomtaka ajiuzulu kutokana na kutajwa kuhusika na mgawo wa fedha za Escrow.
 
Pamoja na hatua hiyo, wajumbe walimtaka Ngeleja ajizulu au akae pembeni ili kumpisha makamu mwenyekiti aongoze vikao jambo ambalo alilipinga.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ambaye ni mjumbe kwenye kamati hiyo, alisema tangu kuanza kwa vikao hivyo Januari 13, mwaka huu, Ngeleja amekuwa akiviendesha kwa nguvu licha ya wajumbe kumtaka akae pambeni.
 
“Amekuwa akiendesha vikao tangu juzi na hata juzi aliendesha na kuondoka saa 4 na kumwachia makamu wa kamati hii kumshikia,” alisema.
 
Alisema juzi baada ya Ngeleja kukaa na kuanza kuendesha kikao hicho, alimtaka kuachia kiti hicho kama ambavyo maazimio manane ya Bunge yalivyowataka wenyeviti waliotajwa kuhusika katika kashfa hiyo ya Tegeta Escrow ambapo yeye anadaiwa kupewa mgawo wa Sh bilioni 40.4 kinyume na sheria.
 
Lissu alisema pamoja na kumshauri kuachia ngazi, bado Ngeleja aligoma kwa madai akifanya hivyo ataonyesha wazi kuwa alihusika katika kashfa hiyo.
 
“Ngeleja alisahau katika azimio la Bunge, halikusema wale waliotuhumiwa walikuwa wezi, lakini akashindwa kujua katika azimio jingine Bunge lilitaka vyombo vya uchunguzi kuchunguza ili watakaobainika wachukuliwe hatua ambazo zitathibitisha kama walihusika au la,” alisema Lissu.
 
Alisema sheria ya maadili ya uongozi wa umma, inawataka viongozi wa umma kutojihusisha na migongano ya kimaslahi na vitendo vya rushwa.
 
“Kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma, Ngeleja baada ya kutajwa katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akihusishwa kupokea fedha hizo, ilitosha atangaze kujiuzulu,” alisema Lissu.
 
Alisema kama Ngeleja, ataendelea kukiuka uamuzi wa Bunge, suala hilo watalirudisha bungeni ili lijadiliwe upya.
 
Zitto
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, alimsihi Ngeleja kutekeleza maamuzi ya Bunge kwa kuachia nafasi hiyo.
 
“Namsihi Ngeleja kama kijana mwenzangu atekeleze maamuzi ya Bunge na aache kumtega Spika Anne Makinda,” alisema.
 
 
SOURCE MPEKUZI

Popular Posts