Saturday, January 24, 2015

Jeshi lawataka watu watambue ujenzi maeneo ya jeshi nikinyume na sheria.




Jeshi la wananchi limewataka watu wachache wanaovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi ya kijeshi ikiwemo mafunzo zana hatari za kijeshi na mabomu katika eneo la Tondoroni na Kiluvya 'B' kutambua kufanya hivyo ni kosa kisheria na litaendelea kuwaondoa katika maeneo hayo kutokana na kukiuka taratibu na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa jeshi la wananchi meja Joseph Masanja amekanusha madai ya wananchi wa Tondoroni la kuibiwa mali zao na kusisitiza serikali ilishawalipa wananchi hao fidia mara mbili kufuatia tathimini iliyofanyika mwaka 1987/88 na ya mwaka 1992/93 ambapo malipo yao yalifanyika juni 11 mwaka 2003 na 2006 na wananchi wengine walilipwa mwaka 2012 kutokana kesi madai na 144/1996.
 
Aidha baadhi ya viongozi wa wanakijiji cha Tondoroni wamefika katika studio za ITV na Redio One wakiwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo barua kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kisarawe na wizara ya ardhi zinazoonyesha kijiji cha Tondoroni kilipata hati ya usajili wa kudumu namba 539 ya mwaka 1993, na kusisitiza serikali iliwalipa wananchi 145 huku wananchi 1404 mpaka sasa hawajalipwa.
 
Mgogoro eneo la Tondoroni lililopo katika wilaya ya Kisarawe, kati ya jeshi la wananchi na wanakijiji umeibuka baada ya serikali kuchukua maeneo mbalimbali ikiwemo kijiji cha Mloganzila, Kiluvya B, na kijiji cha Tondoroni lenye hekta elfu 4197 kwa ajili ya matumizi ya jeshi ambapo yalipimwa kwa mujibu wa sheria.
















No comments:

Post a Comment

Popular Posts