Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za moto
wameuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya watu hao kujaribu
kuwakimbia askari polisi katika mtaa wa sikukuu- Ilala jijini Dar es
salaam.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam
Suleimani Konda amesema majambazi hao walikuwa na silaha moja aina ya
Smg na risasi 6 na baada ya kugundua kufuatiliwa na polisi walifyatua
risasi kujihami ambapo mbali na watu hao kuuwawa na wananchi jeshi hilo
linamshikilia mtu mmoja aliyeokolewa na polisi katika mapigano hayo
akiwa na hali mbaya na amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili
chini ya ulinzi mkali wa polisi kwa mahojiano zaidi.
Aidha kamishna Kova amebaini kufuatia msako mkali
unaofanywa na jeshi la polisi katika jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa 113 kwa makosa mbalimbali,silaha za moto 6,sare za
jeshi, cd mbili zenye mafunzo ya kigaidi pamoja na magari mawili ya
wizi ambapo amesema msako huo bado unaendelea ili kumaliza kabisa
matukio ya uhalifu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment