HALMASHURI ZA MKOA WA NJOMBE ZATAKIWA KUTENGA
MAENEO YA KWA AJILI YA SKAUTI.
Na,Christopher Philemon,Ofisa Habari Mkoa wa
Njombe.
Halmashauri
za Mkoa wa Njombe zimeagizwa kutenga maeneo ya kupanda miti kwa ajili kusaidia
vikundi vya Skauti vilivyopo katika Shule za Msingi na Sekondari zilizopo
katika Halmashuri zao.Pia wakuu wa Wilaya za katika Mkoa huo wamegizwa kuwa
walezi wa Skauti katika wilaya zao.
Maagizo
hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr.Rehema Nchimbi leo tarehe 12
Januari 2015 aliyasema hayo kwenye sherehe ya kusimikwa kuwa mlezi wa Skauti
Mkoa wa Njombe .
Katika
Sherehe hizo zilizofanyika Ikulu ndogo ya Njombe ,Dr.Rehema Nchimbi aliweza
kuuwapisha Makamishna watano wa wilaya za Makete,Ludewa,Njombe na Wanging’ombe.
Mkuu
huyo wa Mkoa amewataka Skauti katika Mkoa wa Njombe kuwa Mfano wa kuigwa katika
masomo,nidhamu na kufanya kazi kwa umoja na upendo katika maisha yao ya kila siku na kuwataka
vijana wengine na wazee kujiunga na Skauti kwani Skauti sio Jeshi bali ni
vikundi vilioundwa kwa utaratibu maalum kwa ajili ya kufundisha
Elimu,Upendo,nidhamu na mazoezi ya kukabiliana na maisha ya kila siku ya
Mwanadamu.
Sarah
Dumba Mkuu wa wilaya ya Njombe alisema kuwa Skauti katika Mkoa Njombe wamekuwa Msaada mkubwa katika matukio
mbalimbali kama vile maafa,sherehe na matukio mengine wamekuwa wametoa msaada
mkubwa katika matukio hayo.
Kamishna
wa Skauti Mkoa wa Njombe Tutsiwene K.Mahenge amesema kuwa kwa mkoa wa Njombe
kunazaidi ya Skauti elfu tatu( 3000) ambao waanafunzi wa Shule za Msingi na
Sekondari na kusema kuwa skauti hao huwa wanudhuria vipindi madarasani kama
kawaida na skauti hao wanafanya mazoezi siku za Jumamosi.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Dr.Rehema Nchimbi akiveshwa Skafu ya kuwa Mlezi wa Skauti
Mkoa wa Njombe na mmoja wa Skauti Mkoa wa Njombe.
|
No comments:
Post a Comment