Mkoa wa Njombe kupata zaidi ya bilioni tatu kwa ajili ya Miradi ya kuboresha huduma ya
maji Mjini Njombe,mradi huyo ni Nyenga na Mradi wa Ujenzi wa Mtandao wa Maji
maeneo ya maji pamoja na eneo la Ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe,hayo
yamesemwa na naibu waziri wa Moses Makala Kwenye
ziara yake ya siku mbili iliyoanza jana ya kutembelea Miradi na vyanzo
vya maji katika Mkoa wa Njombe.
Naibu waziri alisema kuwa mpaka sasa
Mkoa wa Njombe umepokea billion mbili ( 2,177,138,890) kwa ajili ya kusambaza maji maeneo ya
Airport,Kambarage,Igeke,Mji mwema,Nazareti,Magereza na Nzengelendete.
Alisema kuwa wakandarasi tayari wanaendelea
na kazi ya kujenga Manteki matatu yenye
lita135,000 katika maeneo la Mji mwema na Airport huduma ya maji inapatika kwa
kutumia chanzo cha Nyenga che uwezo kwa kusambaza maji eneo la Njombe Mjini.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi na
usafi wa mazingira Njombe ( Njuwasa ) bwana Daudi Majani amemweleza naibu
waziri kuwa miradi wa Nyenga utakamilika
ifikapo mwezi wa tatu mwaka 2015 na kufanya Mji wa Njombe kuongezea huduma ya maji kutoka asilimia 43%
hadi kufikia asilimia 79%.
Aliandelea kusema kuwa kwa ongezeko
hilo la huduma ya maji kwa asilimia 79% itafanya malamka kuongeza idadi ya wateja wake kutoka 4,450
hadi kufikia 5,450 na wateja wa
kufungiwa dira za maji kuongezeka kutoka asilimia 67% ya sasa na kufika kwa
asilimia 90% ya wateja wote.
Naibu waziri amemaliza ziara
yake ya siku mbili mkoani Njombe kwa
kukutana na wadau wa maji katika mkoa huo kwa kuwataka watunze vyanzo vya maji
ili mkoa huo uwendele kuwa na vyanzo vingi vya maji ili kuondoa tatizo la maji
katika makoa wa Njombe.
Naibu waziri wa Maji Moses Makala
wapili kutoka kulia akiapata maelezo ya matumizi ya kuunganisha bomba kwa
kutumia plastic welding kutoka kwa mhandisi wa mamlaka ya maji mkoa wa Njombe
Abiud Njangale,jana kwenye eneo la Air port ambapo maradi wa usambaji wa maji
Mkoa wa Njombe unaendelea.( Picha Christopher Philemon)
PICHA ZA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI MKOANI NJOMBE
No comments:
Post a Comment