NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Mwigulu Nchemba amekubali kuitikia
wito wa kusitisha ziara zake za kichama katika mikoa na wilaya
mbalimbali nchini, kama alivyoagizwa na Katibu Mkuu wa chama hicho,
Abdulrahman Kinana.
Katika
barua yake ya Januari 18, mwaka huu, Kinana alimwagiza Mwigulu ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi
mkoani Singida, kusitisha mara moja ziara zote na kwamba endapo atataka
kufanya hivyo, atalazimika kutoa taarifa na kupata kibali.
Akizungumza
jana na Mpekuzi, Mwigulu alikiri kupokea barua hiyo, na kusema hana
tatizo na kusitisha ziara zake za kichama, kwani ni maagizo halali ya
mamlaka ya juu yake kichama.
“Haya
ni maelekezo, na siku zote kwa kuwa nafanya kazi kwa mujibu wa Katiba,
sioni tatizo kupokea maelekezo rasmi ya kiofisi…aliyeniagiza ni kiongozi
wangu katika chama, nitafanya hivyo,” alisema kiongozi huyo kijana, lakini machachari katika ulingo wa siasa.
Katika
siku za hivi karibuni, amekuwa akipasua anga kwa kutumia helikopta
katika ziara zake alizofanya mikoa ya Tanga na Morogoro.
Mwigulu
alisema amekuwa akipokea mialiko mingi ya kichama, hivyo anajikuta
akitumia muda wake wa ziada wa siku za mwishoni mwa wiki kufanya ziara,
lengo likiwa kutenganisha muda wa utendaji wake katika chama na
serikalini.
“Ndiyo
maana nilikuwa nafanya ziara za kichama siku za mwisho wa wiki pekee…na
baada ya Morogoro pia nimealikwa Kigoma, Mafia (Pwani), Kagera, mikoa
ya Kusini na Njombe. Kwa ujumla mialiko ni mingi, lakini nitaifanya kwa
kufuata maelekezo.
“Sitavunja sheria za chama wala za nchi hata siku moja, nitawatumikia wananchi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa,” alisisitiza Mwigulu.
“Sitavunja sheria za chama wala za nchi hata siku moja, nitawatumikia wananchi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa,” alisisitiza Mwigulu.
Barua hiyo ambayo Kinana alimwandikia Mwigulu tarehe 18 Januari mwaka huu, mwaka huu ilisomeka hivi:
“Umekuwa
ukifanya ziara nyingi katika mikoa na wilaya bila ushirikishwaji kamili
wa Makao Makuu, Mikoa na hasa Kamati za Siasa. Wewe pia umeonesha kwa
kauli na mienendo yako kujiandaa kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM.
Ziara hizi zina mwelekeo wa kampeni, jambo ambalo ni kinyume na maadili
ya Chama. Nakuagiza kuzisitisha ziara zote. Iwapo utataka kufanya ziara
yoyote ya Kichama itabidi kwanza uniarifu na upate kibali changu.
Nakuagiza utekeleze agizo hili mara moja”.
Lakini,
amekuwa akisisitiza amekuwa akiombwa kufanya hivyo na makundi ya watu
mbalimbali, wakiwemo wanasiasa, wasomi, wakulima na wafanyakazi, vijana,
wazee, wanawake na wanaume
No comments:
Post a Comment